WADHAMINI WETU

WADHAMINI WETU

Wednesday, November 1, 2017

CHADEMA CHUJIO LA WACHAFU?

https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEgytdNr6n-ff4z9PVRAKX-j56yKxG71johBHy0fpLgJPpYbmMrRH0A1KlPtNYVvptTuGnq6bDBHb6SC87202GXhvnXhOYExSsxpHnQ8AHCa1imPeOWoZGxuonenpzxP26Oa-SguFDuDb_Y/s640/Lowassa-na-Mbowe.jpg

Na Mwandishi Wetu,
Kitendo cha baadhi ya viongozi wa chama cha demokrasia na maendeleo CHADEMA kumshambulia kwa tuhuma mbali mbali ikiwemo za ufisadi wa vitalu vya uwindaji, upoteaji wa tembo, matumizi mabaya ya madaraka na mengineyo waziri wa zamani wa maliasili na utalii ambaye amejivua uanachama wa chama chake cha awali CCM na kutangaza kuomba uwezekano wa kuhamia CHADEMA kimezua maswali mengi yanayoonyesha ufinyu wa usimamiaji wa misingi katika chama hicho.
Miongoni mwa viongozi waandamizi wa chama hicho ambao pia ni wabunge waliowahi kunukuliwa wakimtuhumu waziri huyo ni pamoja na Joshua nasari mbunge wa arumeru mashariki, pita msigwa wa iringa mjini na Halima mdee wa kawe

Kwa nyakati tofauti wabunge wao wakiwa ndani na nje ya bunge wamekuwa wakimtuhumu Nyalandu kuwa hana analoliweza katika wizara hiyo zaidi ya kujihusisha na udalali wa vitalu vya uwindaji kwa makampuni yanayonasibishwa naye, kusafiri na warembo nje ya nchi kwa kisingizio cha kwenda kutangaza utalii na kupiga picha zisizokuwa na maadili kama waziri na kuzisambaza mtandaoni maneno yaliyosemwa na Joshua Nasari na Msigwa

‘’Kwa CHADEMA unaweza kuwa shetani asubuhi ukiwa CCM, na jioni ukihamia tu kwao unakuwa Malaika hapo hapo, yoote waliyokutukana na kutuhumu nayo wanayasahau na kuanza kukupamba hata kama ulikuwa dhaifu kiasi gani’’. Anasema Ally Mwinyi ambaye pia ni mchambuzi wa kisiasa
Mwinyi aliongeza kuwa kwa maoni yake CHADEMA haina tofauti na chujio la uchafu na kwamba yeyote aliyechafuliwa akihamia chama hicho anakuwa msafi

‘’wewe iba utakavyoiba, tuhumiwa utakatuhumiwa, ukihamia tu chadema unasafishwa na kuwa msafi maradufu…umesahau chadema walivyomtuhumu Lowassa na mwishowe ilivyokuwa?...umesahaukwa Sumaye?, mahanga na kingunge pia?..na mwishowe waliishia kuwa viongozi pendwa wa CHADEMA?’’ aliongeza

No comments:

Post a Comment