·
wazee Singida wamtoa thamani
·
atuhumiwa kumkimbia kigwangala
Ufisadi maliasili
·
yabainika hana cha kupoteza kibunge,
kifamilia
Na Ibrahim Malinda
Baadhi ya wazee wa heshima mkoni
Singida anakotokea ambako pia anatokea Lazaro Nyalandu ambaye amejivua
uanachama wa chama cha mapinduzi hivi karibuni wamewata watanzania hasa wakazi
wa mkoa huo kumpuuza mbunge huyo wa zamani kwa kusema kuwa kitendo chake
alichokifanya si cha kiungwana na wala hakina uwezo wa kufanywa na watu wa
asili ya mkoa huo
Mmoja wa wazee hao Shabani Mughwai
amesema kuwa kama kweli Nyalandu alikuwa anataka kujiondoa na kubalki na
heshima kwa wana singida kamwe asingeweza kwenda kufanyia tukio hilo mkoani
arusha hata kama ni nchi moja.
‘’sasa yeye amekuwa mbunge wetu
zaidi ya miaka 20, kilichomfanya ashindwe kujiuzulu akiwa hapa na kutueleza
yaliyomsibu ili tujue nini cha kumsaidia kama wazee wake ni kipi..hana busara
hata kidogo na ndio maana akaenda kujiuzulu akiwa arusha, tena hotelini lakini
kama angekuwa na busara angekuja kujiuzulu hapa sasa tunaelewa kwanini katibu
mkuu wake Kinana alimwita waziri mzigo’’, anasema Mughwai
‘’tunasikia kwamba ana uraia wa nchi mbili,
kwamba yeye nusu mtanzania na nusu mtu wan chi nyingine, pengine ndio maana
ameamua kutudharau sisi kwa sababu hana cha kupoteza hapa nchini na hata
asipokuwa mwakilishi wetu bado ana uhakika wa kusafiri na kuishi nje ya nchi
hata kama nchi yetu ikiingia kwenye machafuko.. tena mpaka watoto wake tunajua
kuwa nao hawajazaliwa Tanzania. Tunamuombea mungu kwa hilo lakini tunamtaka
asitufarakanishe’’. Aliongeza mzee huyo
Aiza mmoja wa ndugu wa karibu wa
mbunge huyo wa zamani ambaye ameomba kutotajwa gazetini kwanza amesema kuwa
mbunge huyo hastahili kupongezwa eti kaacha ulaji wa kujiuzulu ubunge badala
yake hakuwa na cha kupoteza kwani tayari alishakopa mpaka sehemu ya kiinua
mgongo chake
‘’Lazaro hakubakisha kitu, alikopea
mshahara, posho , marupurupu mpaka na kiinua mgongo, kwa hiyo hakuna chochote
anachopoteza zaidi ya kulitia hasara taifa kumlipia deni lake katika mabenki’’.
Alsema
Juzi gazeti hili liliripoti kuwa aliyekuwa waziri wa Maliasili na Utalii aliyehudumu katika serikali
ya awamu ya nne, Lazaro Nyalandu ambaye pia ni mwanachama wa muda mrefu wa
Chama Cha Mapinduzi(CCM), amejivua uanachama wa chama hicho na hivyo
kupoteza nafasi zake zote ikiwemo ubunge wa Singida Kaskazini na Ujumbe wa
Halmashauri Kuu(NEC) ya CCM.
Kitendo cha kujiondoa CCM kimeenda
sambamba na kutoa rai kwa viongozi na wanachama wa CHADEMA kuwataka wafikirie
kama itafaa kumpokea katika chama hicho ili aendeleze kile alichokiita
kuendeleza Demokrasia na utawala wa sheria.
JAMVI LA HABARI limejulishwa kwamba
Nyalandu hakuwa na namna zaidi ya kujiuzulu na kuhama chama kama sehemu ya
kinga yake baada ya kujiona dhahiri kwamba haendani na kasi, dhamira, malengo ,
utashi na misimamo ya Rais na Mwenyekiti wa CCM Dk. John Pombe Magufuli ambaye
mara zote amekuwa akitangaza hadharani kuwa hana mswalia mtume na aina yoyote
ya viongozi wabadhirifu, wajanja wajanja na walioshiriki kulitia hasara taifa kwa
namna yoyote ile.
Aidha, kitendo cha Nyalandu tangazo
la kufuta vibali vyote vya uwindaji na kwamba serikali haitamchekea mtu yeyote
hata kama alikuwa Waziri inasema kuwa ni miongoni mwa viashiria vya Nyalandu
kuachia ngazi na kukimbilia Chadema.
Hivi karibuni CCM imekuwa
ikisisitiza utaratibu wa kujiendesha chenyewe bila kutegemea ufadhili wa
wanachama na wafanyabiashara na kusisitiza kutokuwepo kwa viongozi wenye vyeo
zaidi ya kimoja na kuondoa kili kilichokuwa kikijengeka kama Umungu mtu ndani
ya chama.
Taarifa zaidi zinasema kwamba
kuondoka kwa nyalandu kunachagizwa na ukweli kwamba umri wake bado ni mdogo na
ameshakaa jimboni kwake kwa zaidi ya vipindi vinne na hakuna jambo lolote la
msingi aliloweza kulifanya kwa wananchi anaowaongoza na kujiona kuwa
ameshachuja kisiasa hivyo kuamua kwake kuhama chama kutamsaidia kurudisha mvuto
alioupoteza jimboni humo.
"Kaka asikudanganye mtu, Lazaro
huku kwetu zama zake zilishapita, na hata mwaka juzi ni heshima tu ya yeye
kugombea Urais ndio iliyomfanya ashinde ubunge, lakini 2020 hata angegombea
udiwani kama Mimi asingeshinda, amechuja mno". Alisema Diwani mmoja ambaye
jina lake linahifadhiwa.
"" unajua siasa ni
mahesabu, sasa huyu bwana kila akipiga hesabu zake anaona hazilipi na
zisingelipa kweli. Angefanyaje zaidi ya kuhama na Rais wetu hataki utani na
wawakilishi wa aina yake?"". aliongeza
Diwani huyo aliongeza zaidi kuwa ni
kwa sababu tu Nyalandu hana aibu, lakini kama angekuwa na aibu asingeweza
kujipeleka Chadema chama ambacho kimekuwa kikimtuhumu kila uchao kipindi akiwa
waziri kuwa anahusika na ubadhilifu katika sekta hiyo.
"Unakumbuka maneno ya Peter
Msigwa kuwa Nyalandu anafadhili ujangili na ubadhirifu katika vitalu?, sasa kwa
tabia ya Chadema na unafiki wao nao watamsafisha kama walivyomsafisha Edward
Lowassa, . Nyalandu alitakiwa atoe majibu ya tuhuma za Msigwa kwanza kabla
hajapokelewa". Aliongeza
Alipoulizwa na Gazeti hili atoe
maoni yake juu ya kitendo cha Nyalandu, Mwanaharakati na Mwenyekiti wa CCM tawi
la mtoni Bokorani, Joseph Yona alisema kuwa watu aina ya Nyalandu ni wa
kuwaogopa kama ukoma
"Mtu yeyote mwenye akili timamu
kama mimi na wewe ataelewa kuwa Nyalandu anahangaikia tumbo lake, CCM
aliyoihudumu kama waziri ndio ile ile anayoilaumu leo na kutangaza kuihama,
tofauti ni kuwa kipindi anahudumu alikuwa anaiona inafaa na ina maana, Leo
hayupo serikalini anaiona haina tena thamani, huyu ni mganga njaa tu hana
lolote". Alisema
" ningemuona mwanaume wa kweli
kama angehama kabla ya Rais kukamilisha uteuzi wa mara ya pili wa baraza lake
la mawaziri, lakini kasikilizia weee, kaona hayumo na imebaki miaka michache na
uwezekano wa kupata nafasi hana amejidai kuhama, awadanganye hao hao Chadema
waliozoea mizoga ya kisiasa sio sisi timamu". Aliongeza Yona
Aidha, katika mitandao ya kijamii
kumekuwa na mijadala mikubwa kuzungumzia kuhama kwa waziri huyo wa zamani huku
taarifa zikielezwa kuwa wiki iliyopita Waziri wa Maliasili na Utalii, Dr.
Hamisi Kigwangalla, akizungumza na wadau wa Wizara yake alisema kuwa baadhi ya
mawaziri na wabunge wa awamu ya nne wangepaswa kuwa jela kwa ufisadi na
ushiriki wao kwenye ujangili. Leo Nyalandu amekimbia. Ifuatayo ni historia ya
kashfa moja ya Nyalandu.
Kampuni ya Kimarekani ya Friedkin
Conservation Fund (FCF) ambayo inamiliki kampuni tanzu za uwindaji wa kitalii
za Mwiba Holdings Ltd, Tanzania Game Trackers Safaris (TGTS) ni miongoni mwa
watuhumiwa wa ujangili
Uchunguzi unaonesha kumekuwapo
matukio kadhaa ya wafanyakazi wa Mwiba kukamatwa wakiwa wameua wanyamapori na kukutwa
na nyara za Serikali.
Vyanzo vya habari kutoka ndani ya
Wizara ya Maliasili na Utalii vimesema mara zote kesi zinazoihusu kampuni hizo
zimekwama kutokana na kile kinachoelezwa kuwa ni urafiki wao wa karibu na
aliyekuwa Waziri wa Maliasili na Utalii, Nyalandu.
Urafiki wa Nyalandu na wamiliki wa
kampuni hizo ulikuwa mkubwa kiasi cha kumpatia moja ya helikopta zake aitumie
kwenye mbio za kuwania urais, kabla ya kushindwa na kujielekeza kwenye ubunge.
Helikopta ya kampuni hiyo ndiyo
aliyoitumia wakati wote wa kampeni zake za ubunge
Nyalandu alimwamuru Kaimu Mkurugenzi
wa Idara ya Wanyamapori wa wakati huo, Paul Sarakikya, kutoa Leseni ya Rais kwa
familia ya Tom Friedkin (mmiliki wa kampuni hizi) kuwinda wanyamapori 700
katika vitalu vinane na eneo la wazi la Makao. Leseni hizo zilitolewa bure bila
kulipiwa hata senti.
Miongoni mwa wanyamapori waliokuwa
kwenye orodha ya kuuawa ni tembo walio katika hatari ya kutoweka.
Pia Nyalandu alikiuka sheria kwa
kupuuza ukomo wa idadi ya vitalu vitano kwa kampuni moja. TGTS imemilikishwa
vitalu vinane pamoja na eneo la wazi; hali ambayo ni ukiukwaji wa kifungu cha
38(7) cha Sheria ya Wanyamapori.
Kampuni hiyo pia ilipewa vitalu na
Nyalandu kinyemela, ilhali sheria ikiagiza kuwa kitalu kinapobaki wazi sharti kitangazwe
kwanza na waombaji washindanishwe katika mfumo na utaratibu ulio wa haki na
uwazi [Kanuni ya Uwindaji wa Kitalii 18(1).
Pamoja na kutoa Leseni ya Rais,
Wamarekani hao walileta watoto wadogo, chini ya umri wa miaka 18 kuwinda; jambo
ambalo ni kinyume cha kifungu cha 43(3) cha Sheria ya Wanyamapori Namba 5 ya
mwaka 2009.
FCF na kampuni tanzu imekuwa
ikiendesha shughuli za utalii kwenye eneo la Makao WMA tangu 2011 baada ya
Mwiba Holdings Ltd kumilikishwa eneo jirani na WMA ya Makao kwa ajili ya shamba
la mifugo na wanyama (Makao Ranch).
Kampuni ya Mwiba Holdings Ltd chini
ya TGTS Ltd ambazo zinamilikiwa na Friedkin Conservation Fund (FCF) imekuwa
ikiendesha shughuli za utalii kwenye eneo la Makao WMA tangu 2011 baada ya
Mwiba Holdings Ltd kumilikishwa eneo jirani na WMA ya Makao kwa ajili ya shamba
la mifugo na wanyama.
Hata baada ya kumalizika Mkataba
wake na JUHIWAPOMA, kampuni ya Mwiba Holdings Ltd iling’ang’ania na kuendelea
kukalia eneo la Makao WMA kwa mabavu na kinyume cha sheria.
No comments:
Post a Comment