Na. Mwandishi Wetu, - JAMVI LA HABARI
Mwanaharakati Philipo Mwakibinga ambaye ni Mratibu wa taasisi ya watetezi wa rasilimali
wasio na mipaka maarufu WARAMI ambae
pia amepata kuwa Rais katika serikali ya wanafunzi chuo kikuu cha Dodoma UDOM
ameibuka na kuibua maswala mazito yanayohusiana na diplomasia ya kimataifa na
uchunguzi wa kipolisi kuhusiana na kifo cha aliyekuwa balozi wa Libya nchini Tanzania
Ismail Nwairat ambaye taarifa zilitolewa zikisema kuwa amejiua kwa kujipiga
risasi akiwa ofisini kwake jijini Dar es salaam tarehe 2 juni 2014.
Fayez al-Sarraj, Waziri Mkuu wa Libya
Katika hali isiyokuwa ya kawaida Mwakibinga
ameitaka serikali kupitia jeshi la polisi na vyombo vingine vya dola kufanya
uchunguzi wa kina ili kujiridhisha na kuondoa utata unaoonekana kuvikabili
vichwa vya wananchi wengi wa Libya waliopo hapa nchini ambao yeye anafahamiana
nao
‘’mimi nina marafiki zangu kadhaa wa
ki Libya, tangu kutokea kwa tukio lile mpaka leo kila siku wanasononeka
kuhusiana na kifo cha balozi wao, na mimi wananitumia kama sample ya mwananchi
ambae taifa langu limeshindwa kulinda uhai wa mwana diplomasia wao’’. Anasema Mwakibinga
‘’wanasema haiwaingii akilini na
hata mimi hainiingii akilini mtu mzima mwenye hadhi ya kuwa balozi ajipige
risasi akiwa ofisini kwake mchana kweupe…kwa maslahi mapana ya taifa langu na
heshima yake kimataifa naviomba vyombo vya dola kufanya uchunguzi wa kina juu
ya swala hili’’. Aliongeza mwanaharakati huyo
Marehemu balozi Ismail Nwairat
ambaye alikuwa anakaimu nafasi hiyo aliripotiwa kupoteza uhai wake kwa kujipiga
risasi ofisini kwake.
Balozi huyo ambaye alikuwa anasifika
kwa kutoficha msimamo wake wa kupingana na serikali iliyoondolewa madarakani ya
hayati Kanal Muamar Gadafi kwa mapinduzi ya umma kwa kuiita ya kidikteta
isiyojali wala kuheshimu haki za binaadam, kifo chake kilizua sintofahamu
miongoni mwa wadau wengi wa masuala ya kidiplomasia ya kimataifa.
Taarifa ya kifo cha balozi huyo
kufariki zilisema kuwa balozi huyo alijipiga risasi ya kifuani upande wa
kushoto akiwa ofisini kwake.
Taarifa iliyotolewa na Wizara
ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa ilisema kuwa, ilipokea
taarifa kutoka kwenye Ubalozi huo kuwa aliyekuwa Kaimu Balozi wa Libya,
Ismail Nwairat amefariki dunia kwa kujipiga risasi.
Hata hivyo ubalozi wa Libya
ulisema kuwa, kifo hicho kilitokea majira ya saa 7 mchana ofisini
kwa Kaimu Balozi huyo katika jengo la Ubalozi wa Libya. Na ilitaarifiwa
kuwa Nwairat alijifungia ofisini na kujifyatulia risasi kifuani upande wa
kushoto.
“Maafisa ubalozi walivunja mlango
waliposikia mlipuko wa bunduki na kumkuta Kaimu Balozi Nwairat ameanguka chini,
walimkimbiza hospitali ya AMI Oysterbay ambako alitangazwa kuwa alikwisha kufariki
na Polisi walithibitisha kifo hicho” ilisema taarifa hiyo.
No comments:
Post a Comment