WADHAMINI WETU

WADHAMINI WETU

Monday, February 6, 2017

JINSI ''UKIMWI WA KICHAWI' UNAVYOTENGENEZWA


IMESIMULIWA  NA  DOKTA. MUNGWA  KABILI………….0744  000  473

Wachawi  wana  uwezo  wa  kutengeneza  magonjwa  mbalimbali kama  vile  ugumba, udhaifu  wa  nguvu  za  kiume, kifafa, upofu, ukichaa, kiharusi, ukimwi nakadhalika.

Hapa  mgonjwa  akienda  kupimwa  hospitali  anakutwa  hana  tatizo  wala  ugonjwa  wowote  lakini  anakuwa  anaonyesha  dalili  zote  za  ugonjwa  husika.  Ukiona  hali  hiyo  basi  ujue  ugonjwa  wako  umetengenezwa   na  wachawi.

Mara  nyingi,ingawa  si  mara  zote, kabla  wachawi  hawajamtupia  mtu  ugonjwa  husika, hujidhihirisha  kwanza  kwa  kutumia  njia  zao  za  kichawi  kama  muhusika  hana  maradhi  wanayo  taka  kumsababishia.

Kama  wakigundua  mhusika  tayari anaugua  maradhi wanayo  taka  kumsababishia, basi  humtengenezea  ugonjwa  mwengine, na  ndumba  ambazo  zingetumika  kumsababishia  maradhi  mhusika, huelekezwa   kwa  mtu  mwingine (  Katika  ulimwengu  wa  wachawi, ndumba  zina  gharama  kubwa  sana,  hivyo  huwa  hazitumiki  bila  sababu  wala  faida )

Kwa  mfano  huko  vijijini, kama  wachawi  wanataka  kumtengenezea  mtu  ugonjwa  wa  kisukari, watataka  kwanza  wajue  kama  mtu  huyo tayari  ana  maradhi  ya  kisukari  au  bado  hajaanza  kushambuliwa  na  kisukari.

WACHAWI  WANAJUAJE  KAMA  MTU  FULANI  ANA  MARADHI  YA  KISUKARI

Kujua  kama  mtu  Fulani  ana  maradhi  ya  kisukari,  wachawi  watafuatilia  mienendo  ya  mtu  huyo kwa  lengo la  kupata  sehemu  atakayo  kojoa.  Siku  wakibahatisha  kumuona  mhusika amekojoa  mahali, basi  watakwenda  hadi  kwenye  eneo  alipokojoa na  kusubiri  kwa  muda  wa  kuanzia  dakika  arobaini  hadi  lisaa  limoja.  Ndani  ya  muda  huo,  KAMA  WATATOKEA  SISIMIZI, basi  ujue  mtu  huyo  ANA  KISUKARI  lakini  KAMA  SISIMIZI  HAWATATOKEA  basi  ujue  mtu  huyo  HANA  MARADHI  YA  KISUKARI. Baada  ya  kipimo  hicho  ndipo  watachukua  hatua  stahiki, za  ama  kumsababishia  maradhi  ya  kisukari  ama  vinginevyo (  KUHUSU  NAMNA  WACHAWI  WANAVYO  TENGENEZA  “KISUKARI  CHA  KICHAWI”  NITAELEZEA  SIKU  ZIJAZO.)

Ukimwi  wa  Kichawi : Katika  ulimwengu wa  kitabibu, “ ukimwi  wa  kichawi” ni  pale  mtu  anapo  onyesha  dalili  zote  za  muathirika  wa  ukimwi, lakini  vipimo  vya  hospitali  vinaonyesha  mtu  huyo  yupo   ( HIV-NEGATIVE)  yaani  bado  hajaathirika .

Hapa  mgonjwa  husika, atapimwa  vipimo  vyote  vya  hospitali  na  vyoote  vitaonyesha  hajaathirika, lakini  ataendelea  kuonyesha  dalili zote  za  mgonjwa  wa  ukimwi . Mgonjwa  huyu  ataendelea  kuugua  na  kuteseka  bila  kupata  nafuu  yoyote  licha  kutumia  dawa  mbalimbali, na  mwisho  wa  siku  atapoteza  maisha  yake.

Zipo  njia  kuu  mbili  wanazo  tumia  wachawi  kusababisha  maradhi  ya  aina  mbalimbali  kwa  watu  mbalimbali. Njia  ya  kwanza, ni  kwa  njia  ya  kuwalisha  dawa  mbalimbali  za  kichawi, ambazo  husababisha  maradhi  ya  aina  mbalimbali ( WACHAWI  WANA  MAARIFA  MAKUBWA  SANA  JUU  YA  MITI  MBALIMBALI  INAYO  SABABISHA  MARADHI NA  MATATIZO  MBALIMBALI )

Njia  ya  pili  ni  kwa  njia ya  majini. Hapa mgonjwa  husika, atasababishiwa  maradhi  ya  aina  Fulani  kwa  kutumiwa  majini  majini  ambayo  yameapishwa  kwenda  kufanya  makazi  yao  kwenye  damu  ya  mtu  aliekusudiwa  na  kusababisha  maradhi  Fulani  kwa  mtu  huyo, hadi   pale  umauti  utakapo  mkuta.

Katika  kutengeneza “ ukimwi  wa  kichawi “ pia  zipo  njia  kuu  mbili  zinazo  tumiwa  na  wachawi.  Njia  ya  kumlisha  mkusudiwa ndumba za  kichawi  ambazo  husababisha  mtu kuugua  maradhi  yanayo  fanana  dalili  zake  na  maradhi  ya  ukimwi  na  njia  ya  pili  ni  kumtupia  majini  ambayo  yatamfanya  augue  maradhi  yanayo  fanana  na  ukimwi.

Leo  tutaangalia  njia  ya kwanza, yaani  njia  ya  kumlisha  ndumba  za  kichawi  mtu  aliye  kusudiwa. Tutaangalia  njia  wachawi  wanavyo  weza  kumlisha  mtu  uchawi, utakao  msababishia  maradhi  ya  ukimwi  na  jinsi  unavyo weza  kujikinga  dhidi  ya  husda  hiyo, na  kwa  wale  ambao tayari  wameshalishwa  uchawi  huo, jinsi wanavyo  weza  kusaidiwa  kupata  tiba  ya  kuondoa  maradhi  hayo  ya  kichawi  mwilini.

Zipo njia  zaidi  ya  arobaini  ambazo  wachawi  wanaweza  kuzitumia, kutengeneza  uchawi  na  kumlisha  mtu, ambao  utamsababishia  kuugua  maradhi  ambayo  dalili  zake  zinafanana  na  ukimwi. Leo  tutaingalia  njia  moja  wapo  kama  ifuatavyo

JINSI  WACHAWI  WANAVYO  TUMIA  MAJI  YA  KISIMA  KUTENGENEZA  “ UKIMWI  WA  KICHAWI “

Awali  ya  yote, wote  tunapaswa  kufahamu  kwamba  katika  ulimwengu  wa  tiba  za  jadi “ MAJI”  yanaweza  kutumika  kama  TIBA  na  wakati  huo  huo, yanaweza  kutumika  kama  “ UCHAWI  WENYE KUDHURU”

Maji  yenyewe  kama  yenyewe, bila  kuchanganya  na  kitu  chochote  kile, yanaweza  kutumika   kama  tiba  ya  magonjwa  karibu  yoote  unayo  yafahamu,  kuanzia  kisukari, kifafa, ugumba, udhaifu  katika  nguvu  za  kiume, kuongeza  urefu  wa  maumbile  ya  kiume ( HAPA  HUTUMIKA  MAJI YAITWAYO  MAJI  YA  FATIRU ), fangasi  za  sehemu za  siri, magonjwa  ya  ngozi,  nakadhalika. 

Sio  tu katika  kutibu  magonjwa  na  maradhi  mbalimbali, maji  pia hutumika  kama  tiba  dhidi  ya  matatizo  mbalimbali  ya  kimaisha kama  vile kuondoa  nuksi, mikosi  nakadhalika.

Vile  vile  maji  yanaweza  kutumika  katika  kutengeneza  uchawi  wenye  kudhuru, wa  aina  mbalimbali.

( KATIKA  SIKU  ZINAZO  KUJA, NITAWEKA  SOMO  KUHUSU  TIBA  MBALIMBALI  ZA  JADI  KWA  NJIA  YA  MAJI  BILA  KUSAHAU,  JINSI  WACHAWI  WANAVYO  TUMIA  MAJI  KUTENGENEZA  UCHAWI  WENYE  KUDHURU  WA AINA   MBALIMBALI )

Katika  ulimwengu  wa  tiba  za  jadi, maji  ya  mtoni, baharini, ziwani, kisimani, kwenye  dimbwi  nakadhalika, huweza  kutumika  eidha  kama  tiba  ya  magonjwa  mbalimbali au  kama  uchawi wa  aina  mbalimbali.

Kinacho  yapa  maji  hayo  kuwa  na  nguvu  ya  kitabibu, ni njia  zilizo  tumika  kuyachukua  maji  hayo. Kila  maji  yanatumika  katika  tiba  yake  na  uchawi  wake. Maji  ya  mtoni  yana tiba  zake  na  uchawi  wake, maji  ya  ziwani, maji  ya  baharini, kisimani  nakadhalika. 
Mfano mdogo, maji  ya  mtoni  yanaweza  kutumika  katika  kutengeneza  uchawi  unaoitwa  “ NSUNKWA”  ambao ni  maalumu  kwa ajili  ya  kumuhamisha  adui yako, aende  kuishi  mbali  na  wewe.

Kila aina  ya  maji  yana  taratibu  yake  namna  ya  kuyachukua  na  kuyatumia  katika  eidha  tiba  au  uchawi.

Leo  tutaona  jinsi  wachawi  wanavyo  tumia  maji  ya  kisima, katika  kutengeneza  maradhi  ya  ukimwi.

Katika  kutengeneza  ukimwi  wa  kichawi, wachawi  hufanya  kama  ifuatavyo :

Kwanza  wanachukua  maji  ya  kisima  kisicho  kauka .Pili  wanachukua  kitovu  cha  mtoto mchanga  kilichodondoka  chenyewe ( Kuweni  makini  sana  na  vitovu  vya  watoto  wenu )  
Tatu  wanachukua  “ Tegelo” ; Kwa  wale  wasio  fahamu Tegelo  ni  mfuko wa  chakula  cha  kuku  na  chakula  chake.  Tegelo  na  kitovu  cha  mtoto, vinachanganywa  na dawa  zingine za  aina  kumi  na  tatu ( sitazitaja  zote  kwa  sababu  za  kimiiko  ya  kazi  yangu: kuna  watu wabaya  wanaweza  kujifunza  kitu  hapo na  kwenda  kuwaumiza  watu )

Vikishachanganywa  vinachomwa  vyote  kwa  pamoja, kisha  vinaenda  kupikwa  njia  panda usiku wa  manane  kwenye  hayo  maji  ya  kisima, pamoja  na  mafuta  ya  usiku.  Baada  ya  hapo  linafanyika  tambiko  maalumu  kisha  vitu  hivyo  vinaenda  kuzikwa  kaburini  kwa  muda  wa  siku  saba.  Baada  ya  hapo uchawi  huo  utakuwa  umekamilika.

 JINSI  WANAVYO  TEGA  UCHAWI  HUO :  Uchawi  huo  hupitia  kwenye  chakula ( sana  sana  “ mboga  yenye  mchuzi “), au  kinywaji.

Mtu  atakae  lishwa  uchawi  huu  ataanza  kuonyesha  dalili  za  ugonjwa  wa  ukimwi, kulingana  na  muda  alio nuiziwa, kama  amenuiziwa  aanze  kuugua  baada  ya  miezi  sita, basi  baada  ya  miezi  sita  kweli  ataanza  kuugua  maradhi hayo, kama  ni  mwezi mmoja  ni mwezi  mmoja.

Mkilishwa  mke  na  mume, basi  mke  na  mume  wote mtaugua  maradhi  hayo. Mkilishwa  familia nzima, basi familia  yote  mtaugua  maradhi  hayo  mmoja  baada  ya  mwingine. Ndio maana  baadhi  ya  familia  unakuta  watu wote   ni waathirika.

Na  kama  mtalishwa  kwenye  sherehe , au msiba, basi  watu  wote  mtaugua  maradhi  ya  ukimwi, isipokuwa  tu  wale  wenye  kinga  zao.

                                   TIBA   YAKE.
Zipo  tiba  za  aina  nyingi  ambazo  zinatibu  maradhi  haya  ya  kutengenezwa. Leo  tutaangazia  tiba  moja  wapo.

Kama una muuguza  mgonjwa  ameugua  maradhi  haya  kwa  muda  mrefu,  bila nafuu  yoyote. Ameenda  kupima  hospitali  akaambiwa  hajaathirika lakini  bado  anaendelea  kuonyesha  dalili  za  mtu  aliye  athirika, basi  fanya  kama  ifuatavyo:

  •   Moja  chukua  dawa  inaitwa  Mlali, pili chukua  dawa  inaitwa  Hangachalo,. Tatu  chukua  dawa  inaitwa  Tarigula, Nne  chukua  dawa  inaitwa  Mwinula, Tano; chukua  dawa  inaitwa  Mzima

  • Dawa  hizi  zitachemshwa  pamoja na  kisu  kikiwa  kimesimama ndani, kisha  unampa mgonjwa  wako  anakuwa  anakunywa mara  tatu  kwa  siku  asubuhi  mchana  na  jioni  kwa  siku  thelathini., Na  nyingine  unakuwa  unampiga  nayo mgongoni  kila  anapokuwa  anakunywa.

Atatapika  uchawi  wote,na  ndani  ya  siku  arobaini, inshaalah  uchawi  na  sumu  yote  itakuwa  imetoka  mwilini  na  atarejea  katika  hali  yake  ya  kawaida.

KINGA :  Kinga  ni bora, kuliko  tiba. Kujiepusha  na  shari  kama  hii, unatakiwa  uwe  na  kinga  bora.

Zipo  kinga  nyingi  bora, ila leo  nitaelezea  kuhusu  kinga  moja. Kinga  hii  inatengenezwa  kwa mchanganyiko  wa    miti na  vizimba  zaidi  ya  mia  moja  na  ishirini . Moja  kati  ya  vizimba  vilivyopo  katika  kinga  hii, ni mti mmoja  ambao  haupatikani  popote  pale  duniani  isipokuwa  mkoa  wa Kigoma  tu.

Ukiwa  na  kinga  hiyo, na  ikatokea  umelishwa  uchawi  wa aina  yoyote  ile  utautapika, na  aliye  kuwekea  uchawi  huo, atapata  madhara  makubwa.

IMESIMULIWA  NA  Dokta.MUNGWA  KABILI.. 0744- 000 473

BREAKING NEWS: RC MAKONDA ACHOCHEA MOTO VITA DAWA ZA KULEVYA

Tokeo la picha la MAKONDAPaul Makonda, Mkuu wa Mkoa wa DSM 
Leo  mkuu wa mkoa wa Dar es salaam Paul Makonda amezungumza akiwa kituo cha kati cha Polisi Dar es salaam pembeni ya Kamishna Simon Sirro kuhusu ishu ya dawa za kulevya inayoendelea kwenye headlines.

Mambo  aliyoyasema mkuu wa mkoa Paul Makonda leo ni kutoa siku kumi kuanzia kesho February 7 2017 kwa Wenyeviti wa mtaa, Wazazi na Watumiaji na Wafanyabiashara.

  • Natoa siku 10 kwa kila Mwenyekiti wa Mtaa kwenye mitaa yote Dar es salaam kutoa taarifa za mtaa wake juu ya dawa za kulevya.
 
  • Natoa siku 10 kuanzia kesho kwa Wazazi, kama wewe ni mzazi unaishi na mtoto anatumia dawa za kulevya na unaishi nae, njoo utoe taarifa….. tukikukamata baada ya siku kumi na mwanao anahusika tutaamini na wewe ulikua sehemu ya kumfanya mtoto wako atumie dawa za kulevya.
 
  • Natoa siku 10 kwa Wafanyabiashara na Watumiaji wa dawa za kulevya, waje wenyewe Polisi kwa kamishna, kama umekua ukifanya biashara ya dawa za kulevya na umeacha njoo Polisi, nguvu tunayo, uwezo tunao…. hakuna kiunga tutashindwa kufika, hizi kelele nyingine zinatupa hamasa

Friday, February 3, 2017

BREAKING NEWS: ZITTO KABWE AIBUKIA UINGEREZA, ATETA NA KIONGOZI WA UPINZANI WA BUNGE LA UINGEREZA

  • Kuonekana kwake kwajibu Hofu na tuhuma za kujificha
  • akialika chama cha Labour katika mkutano mkuu wa Kidemokrasia wa ACT WAZALENDO
  • Labour yamthibitishia Kushiriki
Na Mwandishi wetu :  
 wakati kukiwa na sintofahamu ya kutoonekana hadharani kwa mbunge wa Kigoma mjini na kiongozi wa chama cha ACT WAZALENDO mheshimiwa Kabwe Zuberi Ruyagwa Zitto ambaye pia ametunukiwa heshima ya kiuongozi wa kimila wa kigoma kwa kuitwa MWAMI.
 Image may contain: 2 people, people standing and indoor
leo amevunja ukimya na kuiondoa taharuki hiyo iliyojengeka tangu tarehe 21 mwezi january mwaka huu alipotafutwa kukamatwa na polisi mkoani shinyanga wilaya ya kahama kwa kuonyesha picha zake akiwa nchini uingereza.

katika ukurasa wake wa facebook kiongozi huyo ameandika
 
''Leo asubuhi nimefanya mazungumzo na Kiongozi wa Chama cha Labour cha Uingereza Ndg. Jeremy Corbyn katika Ofisi ya Jimboni kwake Islington Kaskazini.
Tumezungumza kuhusu ujenzi wa Ujamaa duniani katikati ya wimbi la siasa Kali za mrengo wa kulia zinazoendelea sasa.
Image may contain: 2 people, people standing and shoes
Pia tumejadiliana wimbi la kubana uhuru wa mawazo na demokrasia Afrika na Tanzania hususan.
Nimempa rasmi mwaliko wa kuhudhuria mkutano wa kidemokrasia wa kuadhimisha miaka 50 ya Azimio la Arusha utakaofanyika jijini Arusha tarehe 25 Machi 2017. Chama cha Labour kimekubali kuhudhuria mkutano huo. Image may contain: 1 person
Ndg. Corbyn pia amenialika kwenye mkutano mkuu wa Labour ambapo Seneta Bernie Sanders atahudhuria pia''.

Zitto Kabwe

hivi karibuni mshauri wa chama hicho na mhadhiri mashuhuli nchini Tanzania Prof. Kitila mkumbo alitoka hadharani na kusema kuwa kiongozi Kabwe yupo salama na hajapotea taarifa iliyotanguliwa na ile ya kiongozi huyo kutokubali kukamatwa na polisi bila kufuata utaratibu wa kiuongozi taarifa ambayo ilisambazwa na naibu katibu mkuu wa chama hicho bwana Msafiri Abdulahman Mussa Bin Salim wa  Mtemelwa, Ipombo Nyamangalo Nkumba  Sesiamali Lwigalwike.

NB: PICHA MBALI MBALI ZINAMUONYESHA ZITTO KABWE AKIWA NA KIONGOZI HUYO WA CHAMA CHA LABOUR

Je, kifo cha Tshisekedi kitaathiri mazungumzo ya amani DR Congo?


Waombolezaji DR Congo Waombolezaji DR Congo
Wafuasi wa Etienne Tshisekedi kiongozi wa upinzani nchini DR Congo aliyefariki wamekongamana katika mji mkuu wa Kinshasa ili kuonyesha mshangao wao wa kifo cha kiongozi huyo.
Akiwa mpinzani maarufu wa viongozi waliokuja na kuondoka nchin humo alitarajiwa kuongoza baraza la serikali ya mpito kwa makubaliano ya rais Kabila kujiuzulu.
Kiongozi huyo mwenye umri wa miaka 84 alifariki nchini Ubelgiji ambapo alienda wiki iliopita ili kufanyiwa ukaguzi wa kimatibabu.
Waziri wa habari amesema kuwa atafanyiwa maziko ya kitaifa.
Bw Tshisekedi alirejea mjini Kinshasa mwezi Julai katika makaribisho ya shujaa baada ya kukaa miaka miwili mjini Brussels kwa matibabu ya kiafya.
Kifo chake kinajri wakati muhimu wa DR Congo pamoja na ghasia za maandamano wakati ilipotangazwa kwamba rais Kabila atasalia madarakani hadi mwezi Aprili 2018.
Mwandishi wa BBC nchini DR Congo Anne-Marie Dias Borges anasema kuwa Tshisekedi alikuwa mtu maarufu mjini Kinshasa na kupewa jina la utani la 'Sphinx of Limete'.
Tshisekedi alivutia umati mkubwa katika mikutano yakeTshisekedi alivutia umati mkubwa katika mikutano yake
Limete ni nyumbani kwake karibu na mji wa Kinshasa.
  • Kipi kitarajiwe katika makubaliano ya amani?
Kifo cha Tshisekedi kinajiri wakati ambapo upinzani na serikali uko katika meza ya kujadiliana kuhusu kuondoka kwa rais Kabila baada ya miaka 16 mamlakani.
Mazungumzo hayo ambayo bado hayajaisha yanahitaji serikali ya mpito pamoja na tarehe ya uchaguzi.
Bw Tshisekedi alitarajiwa kuongoza kamati ya mpito. Amekuwa akipigania demokrasia
Kwa zaidi ya nusu karne sasa taifa lote liliungana nyuma yake dhidi ya uongozi wa kiimla wa Mobutu Sese Seko ama uongozi wa Kabila baba na mwanawe.
Lakini wakati huo bw Tshisekedi alikuwa mnara wa kivyake.
Msimamo wake wakati mwengine huenda ulikuwa kikwazo kwa maendeleo ya kidemokrasia.
Katika kipindi cha miaka mitatu iliopita Bw Tshisekedi amekuwa akiugua ,mwanawe Felix amekuwa akichukua jukumu kubwa zaidi.
Hatma ya chama cha Union for Democracy and Social Progress UDPS inayumbayumba.
Viongozi wengine wachanga wa upinzani sasa wanaweza kupata fursa ya kuingia katika mazungumzo hayo ya mpito ambayo yanatarajiwa kuendelea chini ya uongozi wa viongozi wa makanisa nchini humo.
  • Je, watu wamepokea vipi kifo chake?
Mashahidi wanasema kuwa huku habari za kifo chake zikiendelea kusambaa mjini Kinshasa siku ya Jumatano jioni, ghasia zilizuka kati ya kundi moja la wafuasi wake na maafisa wa polisi ambao walitumia vitoa machozi.
Waombolezaji waliokongamana katika nyumba ya mwanawe mjini Kinshasa wanasema wana wasiwasi kuhusu hali ya baadaye.
''Mtu huyo alijitolea maisha yake pamoja na ujana wake wote.Mtu huyu alitufanya tufungue macho, alikuwa shujaa wetu''.
''Alikuwa taa ya Afrika. Alikuwa maarufu.Tumepoteza mtu muhimu sana'', mwanamke mmoja aliambia BBC.
Mwengine anasema wafuasi wake walikuwa wanamjua kuwa mtu ambaye ilikuwa vigumu kumhonga.
''Alikuwa mpinzani wa kihistoria.Mandela alikuwa wa kwanza na Tshisekedi alimfuata''.
Waziri wa maswala ya kigeni nchini Ubelgiji Didier Reynders alimtaja Tshisekedi kama mwanasiasa maarufu.
Ubelgiji inajiunga na raia wa DR Congo katika wakati huu wa huzuni ili kuona kwamba kazi yake inazaa matunda, kilisema chombo cha habari cha AFP.
  • Ufanisi wake ni nini katika miaka 57 ya siasa?
Akiwa mzaliwa katika jimbo la kati la Kasai mnamo mwezi Disemba mwaka 1932, bw Tshisekedi akiwa na umri wa miaka 79 alikuwa kiongozi wa upinzani mwenye umri mkubwa.
Alisomea sheria chini ya ukoloni nchini Ubelgiji.
Harakati zake za kisiasa zilianza wakati wa uhuru wa taifa hilo mwaka 1960 ambapo alikabidhiwa nyadhfa za juu katika serikali ya kati mbali na utawala wa Kasaian uliokuwa mfupi.
Mnamo terehe 14 mwezi Novemba 2011, akiwa waziri wakati wa serikali ya dikteta Mobutu Sese Seko bw Tshisekedi alijimwaga katika siasa za upinzani 1980 wakati Mobutu alipoamua kufutilia mbali uchaguzi wote.
Mobutu Sese Seko Mobutu Sese Seko
Akiwa kiongozi wa chama cha muungano wa Demokrasia pamoja na chama cha Social Progrees, amekuwa mpinzani wa serikali zote tangu wakati huo.
Wakati Mobutu alipolazimishwa kutengeza serikali ya muungano na upinzani, bw Tshisekedi alikuwa waziri mkuu mara mbili katika kipindi cha miaka miwili.
Alijiuzulu nyakati zote hizo alipokosana na Mobutu.
Chama cha Bw Tshisekedi hakikushiriki katika vita wakati wa vita vilivyozuka baada ya utawala wa Mobutu kuanguka 1997, na hivyobasi kupata umaarufu mkubwa kutoka kwa raia walioathirika na mapigano hayo.
Baada ya kususia uchaguzi mwaka 2006, ambao anadai ulifanyiwa udanganyifu ,bw Tshisekedi aliamua kujitokeza na kuhakikisha kuwa anashinda.
Kwa wengine aliamua mapema kujitangaza kuwa rais kabla ya kupigwa kwa kura hiyo.

Thursday, February 2, 2017

Msanii Beyonce atarajia kujifungua mapacha

BeyoncePicha ya Instagram ya BeyoncePicha ya Instagram ya Beyonce

Chini ya wiki mbili tangu Donald Trump aapiswhe kuwa rais wa Marekani, taarifa kuu kutoka Marekani tangu wakati huo zimehusiana na siasa.
Amri za Trump na mabadiliko kwa sera za Marekani vimeonekana kugubika masuala mengine yanayoibuka Marekani.
Kabla ya Trump kuapishwa, mashabiki wengine walidai kuwa Beyonce angetoa albamu mpya wakati Trump akiapishwa.
Hata hivyo Beyonce hakutoa albamu bali alitangaza kupitia mtandao wa Instagram kuwa angetoa vitu tofauti,Beyonce, mumewe Jay Z na binti wao Blue IvyBeyonce, mumewe Jay Z na binti wao Blue Ivy

Ukweli ni kwamba Beyonce ana ujauzito wa mapacha.
Picha ya Instagram ilimuonyesha Beyonce akiwa amepiga magoti kando na maua akionekana kuwa mjamzito.
Taarifa hizo za Beyonce zilionekana kuwavutia watu kutoka mitandao mingine.
Watu wengine wamekuwa wakitoa maoni yao kuhusu majina watakayopewa watoto wa Beyonce, wenginewakisema waitwe Yellow na Red Ivy. Binti wa umri wa miaka mitano wa Beyonce na Jay Z aliopewa jina la Blue Ivy Carter.

Trump amkatia simu waziri mkuu wa Australia

Trump na TurnbullTrump na Turnbul

Mawasiliano ya simu kati ya Rais wa Marekania Donald Trump na waziri mkuu wa Australia Malcolm Turnbull, yamezua maswali kuhusu makubaliano ya kuwachukua wakimbizi.

Gazeti la Washington Post liliripoti kuwa bwana Trump alitaja mawasiliano hayo kuwa mabaya zaidi kati ya yale aliyoyafanya na viongozi wa dunia siku hiyo, ambapo aliikata simu hiyo.
Bwana Trump kisha aliandika kwenye mtandao wa twitter kuwa atafanyaia uchunguzi makubaliano hayo.

Makubaliano hayo yaliyoafikiwa wakati wa utawala wa Rais Obama, yatasababisha hadi watafuta hifadhi 1,250 wanaoelekea Australia kupewa hifadhi nchini MarekaniAustralia imekataa kuwakubali wakimbizi wengi wao wakiwa ni wanaume kutoka Iran, Afghanistan na Iraq na badala yake wamewazuilia katika vituo vilivyvo kwenye visiwa vya Nauru na Papua New Guinea.
Waziri mkuu Turnbull amekuwa akitaka kujua hatma ya makubaliano hayo baada ya Trump kusaini amri ya kuzuiwa kwa muda wakimbizi kutoka nchi saba zilizo na waislamu wengi kuingia nchini Marekani.
Bwana Turnbull baadaye alsema kuwa alikasirishwa kuwa mawasiliano hayo yaliwekwa hadharani.
Alikiambia kituo kimoja cha redio mjini Sydney kuwa ripoti kwamba Trump alikata simu si za ukweliTrump aliandika kwenye TwitterTrump aliandika kwenye Twitte

MAREKANI : Tillerson aapishwa kuwa Waziri wa Mambo ya Nje

Rex Tillerson aapishwa na Makamu wa Rais Mike Pence mbele ya Rais Donald Trump 
 Rex Tillerson aapishwa na Makamu wa Rais Mike Pence mbele ya Rais Donald Trump.

Rex Tillerson ameapishwa Jumatano usiku kuwa Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani masaa machache baada ya kuthibitishwa na Baraza la Seneti.

Makamu wa Rais Mike Pence alimwapisha Tillerson katika ofisi ya Oval ya ikulu ya White House ambako tukio hilo lilishuhudiwa na Rais Donald Trump.

Tillerson alimshukuru Trump kwa kumpa kile alichokiita “nafasi kunjufu,” na kusema kuwa siku zote atayasimamia maslahi ya Wamarekani.