Chini ya wiki mbili tangu Donald
Trump aapiswhe kuwa rais wa Marekani, taarifa kuu kutoka Marekani tangu
wakati huo zimehusiana na siasa.
Amri za Trump na mabadiliko kwa sera za Marekani vimeonekana kugubika masuala mengine yanayoibuka Marekani.Kabla ya Trump kuapishwa, mashabiki wengine walidai kuwa Beyonce angetoa albamu mpya wakati Trump akiapishwa.
Hata hivyo Beyonce hakutoa albamu bali alitangaza kupitia mtandao wa Instagram kuwa angetoa vitu tofauti,
Ukweli ni kwamba Beyonce ana ujauzito wa mapacha.
Picha ya Instagram ilimuonyesha Beyonce akiwa amepiga magoti kando na maua akionekana kuwa mjamzito.
Taarifa hizo za Beyonce zilionekana kuwavutia watu kutoka mitandao mingine.
Watu wengine wamekuwa wakitoa maoni yao kuhusu majina watakayopewa watoto wa Beyonce, wenginewakisema waitwe Yellow na Red Ivy. Binti wa umri wa miaka mitano wa Beyonce na Jay Z aliopewa jina la Blue Ivy Carter.
No comments:
Post a Comment