Mheshimiwa Habib Mnyaa pichani
Wajumbe wote 112 wamepiga kura za ndio
kuazimia kumfukuza uanachama kwa mujibu na mamlaka ya kikatiba
yaliyoelezwa katika katiba ya CUF ukurasa wa 29 ibara ya 18(1)(ix)
kuhusu wajibu wa Mkutano Mkuu wa Tawi kama ilivyoeleza kuwa;
THE CIVIC UNITED FRONT
(CUF –Chama Cha Wananchi)
TAARIFA KWA UMMA
Imetolewa leo Tarehe 7/2/2017
MOHAMED HABIBU MNYAA AFUKUZWA UANACHAMA
Leo
tarehe 7/2/2017 Mkutano Mkuu wa Tawi la Chanjaani, Jimbo la Mkoani
wilaya ya Mkoani-Pemba, umefanya maamuzi ya kumfukuza uanachama wa CUF
Mohamed Habibu Mnyaa kutokana na kukiuka katiba ya chama Ibara ya 12
(6)(7)(16) kutokana na kuwa na mwenendo usiofaa wa kuwagawa wanachama,
kueneza taarifa za upotoshaji dhidi ya viongozi na Chama, kufanya
vitendo vya hujuma za kutaka kukidhoofisha Chama, kudharau na kushindwa
kuhudhuria na kutoa ushirikiano kwa tawi lake kila alipotakiwa kufanya
hivyo. Mkutano Mkuu wetu wa leo umehudhuriwa na wajumbe halali 112 kati
ya wajumbe wote halali 113.
Wajumbe wote 112 wamepiga kura za ndio
kuazimia kumfukuza uanachama kwa mujibu na mamlaka ya kikatiba
yaliyoelezwa katika katiba ya CUF ukurasa wa 29 ibara ya 18(1)(ix)
kuhusu wajibu wa Mkutano Mkuu wa Tawi kama ilivyoeleza kuwa;
“Kumchukulia
hatua za nidhamu mwanachama au kiongozi yeyote wa tawi hilo, ikiwa ni
pamoja na kumpa onyo, karipio, karipio kali, kumsimamisha uanachama au
uongozi wa Chama kwa muda, na hata kumuachisha au kumfukuza uanachama wa
Chama”
Mohamed Habibu
Mnyaa alijiunga na CUF katika tawi hilo tarehe 28 septemba mwaka 1999 na
kukabidhiwa kadi yenye Namba ya usajili 029033. Mohamed ambaye amewahi
kuwa Mbunge wa Jimbo la Mkanyageni kwa muda wa vipindi viwili 2005-2015,
amekuwa na mwenendo huo mbaya na usiofaa kwa Chama na viongozi wake
tangu alipokosa ridhaa ya wanachama na Maamuzi ya vikao vya Chama
kumpitisha kugombea kwa mara nyingine tena katika nafasi ya ubunge mwezi
August, mwaka 2015. Mohamed amefukuzwa uachachama akiwa ni mwanachama
wa kawaida wa tawi la Chanjaani asiyekuwa na wadhifa wowote mwingine
ndani ya Chama.
Kwa mujibu wa Katiba ya CUF ibara ya 108(5) kuhusu Nidhamu ya chama na Muda wa kukata Rufaa inaeleza kuwa;
“
Mwanachama au kiongozi yeyote aliyeamua kukata Rufaa kwa jambo lolote
lile, basi atafanya hivyo kwa ngazi iliyo juu ya kikao kilichotoa
maamuzi ambayo hakuridhika nayo katika kipindi kisichozidi siku kumi na
nne (14) tokea siku uliotolewa uamuzi huo” ni hiyari yake kuona kama
inafaa kukitumia kifungu hiki au kutokitumia.
Tunatoa
wito kwa wanachama wote wa tawi la Chanjaani, kuzingatia wajibu wao wa
kikatiba na kuheshimu taratibu, kanuni na kulinda nidhamu na heshima ya
Chama chetu ndani ya Chama na ndani ya jamii kwa ujumla. Uongozi wa tawi
hautasita kutekeleza matakwa ya katiba pale itakapobainika kwa
mwanachama yeyote kwenda kinyume na maamuzi na misimamo ya Chama.
HAKI SAWA KWA WOTE
KOMBO MOHAMED MAALIM
KATIBU WA TAWI LA CHANJAANI, JIMBO LA MKOANI-PEMBA
Mawasiliano: 077 815 3414
No comments:
Post a Comment