Mwigizaji mashuhuri Angelina Jolie
alizua mjadala mkali alipokuwa akivumisha filamu yake mpya nchini
Cambodia alipokaanga na kuwala buibui akiwa pamoja na watoto wake.
Mwigizaji huyo alisema walikuwa na "ladha tamu sana".Kula wadudu ni jambo lililohusishwa kwa muda mrefu na uigizaji, katika vipindi vya runinga kama vile I'm a Celebrity... Get Me Out Of Here.
Lakini je, tunafaa kuwa kama Angelina na kuanza kuwala wadudu?
Kwanini tunafaa kula wadudu?
Inakadiriwa kwamba kufikia mwaka 2050, idadi ya watu duniani itafikia bilioni tisa.
Ndipo tuweze kuwalisha, itabidi uzalishaji wa chakula uongezeke maradufu.
Idadi ya watu duniani inapoopanda, kuna juhudi za kutafuta njia mbadala za kupata chakula - hasa protini - badala ya vyakula vya kawaida kutoka kwa mifugo na samaki.
Kula wadudu ni moja ya njia hizi mbadala.
Hili linasifiwa sana kwani wataalamu wanasema ni endelevu kimazingira, wana virutubisho vingi na wanaweza kupatikana kwa urahisi, kwa gharama nafuu na katika hali nzuri.
Maanufa ya kula wadudu ni gani?
"Wadudu ndio chakula halisi chenye virutubisho karibu vyote," anasema Shami Radia, mwanzilishi mwenza wa Grub, duka linalouza wadudu wanaoliwa.
"Wana protini, madini mengi na asidi za amino na kwa hivyo ni faida sana kuwala."
Wadudu pia huwa bora kwa mazingira ukilinganisha na ufugaji.
Wanaweza kula taka, hawatoi gesi zinazochangia ongezeko la viwango vya joto duniani, hawahitaji maji mengi na huhitaji eneo kubwa la shamba kuwafuga.
Wadudu pia wana kiwango cha juu sana cha kubadilisha mali ghafi kuwa kawi au chakula kwa sababu hawahitaji kudhibiti joto katika miili yao kwa kutumia damu kama wafanyavyo mifugo na wanyama wengi.
Kwa kawaida, wadudu wanaweza kubadilisha kilo 2 za lishe kuwa sehemu ya mdudu.
Ng'ombe atahitaji kula lishe ya kilo 8 ndipo aweze kuongeza kilo 1 katika uzani wake.
Ni wadudu wa aina gani wanaoliwa?
Kuna karibu wadudu aina 1,900 ambao wanaweza kuliwa duniani, kwa mujibu wa Shirika la Chakula Duniani (FAO).Wengi wa wanaoliwa ni mende, viwavi, nyuki, nyigu, nzige, kumbikumbi, nge, vipepeo na kerengende.
Licha ya kwanda wadudu hawa wanapatikana kwa wingi, ni aina chache sana ya wadudu hawa wanaoliwa na jamii Afrika Mashariki.
No comments:
Post a Comment