WADHAMINI WETU

WADHAMINI WETU

Thursday, February 2, 2017

BREAKING NEWS: RUSHWA SAKATA LA UDA, MADIWANI NA WABUNGE WA UKAWA WALIOHONGWA KUSHITAKIWA KAMATI KUU YA CHADEMA

  • Meya wa UKAWAUbungo athibitisha kuzifahamu tuhuma za Rushwa
  • asema atakiomba chama chake kuwafanyia uchunguzi madiwani na wabunge wote wanahusika.
 Tokeo la picha la meya kibamba

Meya wa Ubungo Boniface Jacob akiwa na Mbunge wa Kibamba John John Mnyika katika Picha ya Maktaba.

Na Mwandishi wetu:

wakati kukiwa na taarifa za mameya wote wa UKAWA wanaongoza katika halimashauri za manispaa mbali mbali zilizopo jijini Dar es salaam kuitwa Dodoma kwenda kujadili kwa mapana tuhuma zilizoibuliwa kuhusu uuzwaji wa shirika la UDA, mameya hao ni  wale wa Ubungo, Ilala na emya wa jiji la Dar es salaam.

mjumbe wa kamati kuu wa CHADEMA ambaye pia ni mstahiki meya wa manispaa ya ubungo Boniface Jacob amekiri kuzipata na kuzifahamu  hizo taarifa za wajumbe wa halimashauri ya jiji kupokea rushwa ya kati ya shilingi milioni moja mpaka milioni tatu kwa madiwani wa vyama vyote na shilingi milioni tano tano kwa wabunge wa vyama vyote kutoka kwa wamiliki wapya wa shirika la usafiri Dar es salaam UDA ili kuhalalisha uuzwaji usiofuata misingi ya kisheria wa shirika hilo na kupokea shilingi bilioni 5.8 kama mgao wao wa asilimia 51% na kuahidi kuzifikisha rasmi katika vikao halali vya chama chake cha chadema ili chama hicho kiwachukulie hatua stahiki wajumbe wote watakaobainika kujihusisha na vitendo hivyo ambavyo haviendani na misingi ya chama chao ya kupambana na Rushwa.

''nimezisikia na zimesambaa sana hizo taarifa hata kabla hujaniuliza, na kwa kweli zinatuvunjia heshima sisi kama wawakilishi wa wananchi na wana chadema, kwa hiyo nimeamua kukiandikia barua chama changu kupitia katibu mkuu kiitishe uchunguzi rasmi ili kujiridhisha juu ya tuhuma hizo ambazo si nyepesi'' alisema Boniface alipoulizwa na  JAMVI LA HABARI kwa njia ya Simu .

''mimi binafsi na mjumbe wa kamati kuu ya chama, hivyo nina nafasi ya kuliiingiza hilo kwenye kikao muhimu  ili lichukuliwe hatua, lakini kwa madiwani wa vyama vingine sina uamuzi nalo maana wao pia wana utaratibu wao katika vyama vyao, lakini kwa CHADEMA hatutamwangalia mtu usoni, chama kitachunguza na atakayebainika kuchukua rushwa hiyo atawajibika ipasavyo''. aliongeza mstahiki meya Boniface.

hivi karibuni JAMVI LA HABARI lilipoti juu ya kuwepo kwa tuhuma za wawakilishi hao wa wananchi wa jiji la Dar es salaam kuhongwa ili kuridhia utakatishwaji wa matumizi ya fedha hizo.

taarifa za uhakika zinasema upande wa vigogo wa UDA sasa wanahaha kuhakikisha kuwa taarifa za wao kugawa fedha kwa madiwani na wabunge ili kuhalalisha mradi wao hazimfikii Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli kwa kuwa wanafahamu zikimfikia na akifanya uchunguzi na akajiridhisha hawezi kuhalalisha biashara hiyo kutokana na msimamo wake uliojizolea umaarufu kwa wananchi wa kupambana na Rushwa na kuchukia aina yote ya ufisadi.

''jamaa wanahaha kuhakikisha namba moja hazipati hizi taarifa za chini ya carpet, unajua walijitahidi sana kuficha na kuwarubuni wasaidizi wa rais kuwa hakuna shida kwenye mradi ule na kwamba kutokuunga mkono ni kuchelewesha juhudi za maendeleo, sasa lilipoibuka hili wamepagawa, wanajua kabisa Rais hawezi kubali''. kilisema chanzo kimoja cha habari kilicho karibu na wamiliki hao wa UDA
 Tokeo la picha la magufuli
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli

No comments:

Post a Comment