''kama mradi wa UDA ni mradi halali,
sasa ilikuwaje wabunge na madiwani wahongwe pesa ili kuuhalalisha(kukubali
matumizi ya billion 5.8), unawezaje kuhonga ili upokelewe fedha zako
ulizonunulia kitu halali mpaka vyombo vya habari vinaandika?''.........
·
Amshangaa kupinga Rushwa lakini anabariki
UFISADI UDA
·
Asisitiza
Rais Kapotoshwa Makusudi
·
Amtaka Kujitafakari
Na mwandidhi wetu -
JAMVI LA HABARI
Wakati kukiwa na taarifa kadha wa kadha mkanganyiko juu ya
hatma ya Sakata la UDA kuelekea kutekelezwa kwa agizo la Rais Dkt John Pombe
Magufuli la kulitaka Jiji la Dar es salaam Kukutana haraka na kupanga matumizi
ya mgao wao wa shilingi bilioni 5.8 kama malipo ya mauzo ya Hisa zao asilimia
51 ambazo jiji lilikuwa linazimiliki.
Kumekuwepo na taarifa za uhakika zinazosema kwamba
mwenyekiti wa chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA mheshimiwa Freeman
Mbowe kuunda kamati maalum ya wataalam wa chama hicho kupitia na kuhakiki
mchakato mzima wa uuzwaji wa hisa hizo na ushiriki wa madiwani na wabunge wake
katika kile kinachoitwa kupokea rushwa ya kati ya shilingi milioni moja mpaka
tano ili kubariki uuzwaji huo.
Mmoja wa wajumbe wa baraza hilo la jiji ambaye pia ni
mstahiki meya wa manispaa ya Ubungo Boniface Jacob ameonyesha masikitiko yake
namna Rais Magufuli alivyopotoshwa juu ya jambo hilo na kwamba namna
alivyohutubia siku ya uzinduzi wa mradi ule hakika Rais ametumika kuhalalisha moja
kati ya UFISADI mkubwa kuwahi kutokea katika historia ya taifa letu.
Akizungumza na JAMVI LA HABARI mstahiki Boniface Jacob
amesema kuwa haelewi na kwanini Rais Magufuli ameamua kupingana na msimamo,
tabia na utambulisho wake mbele ya jamii wa kuwa mpinga Ubadhilifu na mkataa
rushwa huku akitajitanabaisha kama
mtetezi wa rasilimali wa Taifa.
‘’ukimsikiliza Rais Magufuli utaona namna gani ambavyo
anatamani kuwa katika jumuiya ambayo haina ujanja ujanja, Rushwa , Ubadhilifu
na Ufisadi wa aina yoyote, na ndio maana hakuna anayepingana naye kwenye hilo,
lakini ukiangalia namna alivyo li-adress suala la UDA unaweza ukajiuliza mara
mbilimbili ni Magufuli huyu huyu au mwengine’’. Alisema Mstahiki Boniface
‘’Watanzania wanaomuamini Rais Magufuli sidhani kama
wanafahamu Rais wao ametumika Kubariki mradi wa Kifisadi namna hii, Rais
amezungukwa na wajanja wachache waliogawana mali za masikini wa Tanzania
waishio DSM, (Shirika la UDA), na sasa wanafaidi mali hizo huku waliotoka jasho
kuzitafuta wakiendelea kubaki masikini’’. Aliongeza Meya Jacob
Kadharika Meya Jacob alisema kuwa haingii akilini kuwepo kwa
taarifa za rushwa na kuhongwa kwa wabunge na madiwani wa vyama vyote
vinavyoongoza jiji hilo ili kupitisha mradi huo na wao chadema kuchukua hatua
huku chama kinachoongozwa naye Rais kikiendelea kuvuta miguu.
‘’sisi tulipozipata taarifa za kutolewa Rushwa kwa wajumbe
wetu, mara moja chama kimeanzisha uchunguzi wa ndani na kamati ya wataalam
imeundwa na mwenyekiti wa chama, sasa tunashindwa kuelewa mpaka sasa Rais na mwenyekiti
wa CCM amechukua hatua gani’’. Aliongeza
‘’hivi nikuulize swali, kama mradi wa UDA ni mradi halali,
sasa ilikuwaje wabunge na madiwani wahongwe pesa ili kuuhalalisha(kukubali
matumizi ya billion 5.8), unawezaje kuhonga ili upokelewe fedha zako
ulizonunulia kitu halali mpaka vyombo vya habari vinaandika?, maana yake hapo
kuna walakini na siamini kama Magufuli aliyejipambanua mpiga madili dili hili
halioni’’. Alisema Diwani huyo machachari wa kata ya Ubungo
Alipoulizwa juu ya thamani halisi ya shirika hilo la UDA
alisema kuwa anaendelea kujumlisha mali halisi za shirika hilo na kuzitathmini
na kesho atatoa taarifa kwa umma inayoonyesha mali halali za shirika hilo na
thamani yake ambapo kwa kifupi anasema mali hizo ni zaidi ya mara hamsini mbele
ya fedha ambazo Simon Group wamenunulia shirika hilo.
No comments:
Post a Comment