WADHAMINI WETU

WADHAMINI WETU

Thursday, February 2, 2017

Kiongozi wa upinzani DRC Etienne Tshisekedi afariki dunia

Tshisekedi alikuwa kiongozi maarufu wa upinzani kwa miongo kadhaaTshisekedi alikuwa kiongozi maarufu wa upinzani kwa miongo kadhaa.

 Kiongozi wa upinzani nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, Etienne Tshisekedi, amefariki dunia mjini Brussels nchini Ubelgiji akiwa na umri wa miaka 84.
Tshisekedi alikwenda mjini Brussels mwishoni mwa mwezi jana kwa ajili ya matibabu.

bwana Tshisekedi alikuwa mmoja wa wanasiasa wakongwe waliokuwa mstari wa mbele kupigania demokrasia ya nchi yake.Tshisekedi alikuwa na mvuto mkubwa kwa wananchi wa DRCTshisekedi alikuwa na mvuto mkubwa kwa wananchi wa DRC.

Alisimama kidete katika utawala wa aliyekuwa kiongozi wa nchi hiyo Rais Mobutu Sese Seko, ambae utawala wake ulidumu kwa miongo kadhaa kabla ya kupinduliwa.

Etienne Tshisekedi pia alikuwa mpinzani wa Rais Laurent Kabila, ambae aliingia madarakani mnamo mwaka 1997, na mwanae, Rais Joseph Kabila, ambae hivi sasa ndio anatawala nchi hiyo.

No comments:

Post a Comment