Rex Tillerson aapishwa na Makamu wa Rais Mike Pence mbele ya Rais Donald Trump.
Rex Tillerson ameapishwa Jumatano usiku kuwa Waziri wa Mambo ya Nje
wa Marekani masaa machache baada ya kuthibitishwa na Baraza la Seneti.
Makamu wa Rais Mike Pence alimwapisha Tillerson katika ofisi ya Oval
ya ikulu ya White House ambako tukio hilo lilishuhudiwa na Rais Donald
Trump.Tillerson alimshukuru Trump kwa kumpa kile alichokiita “nafasi kunjufu,” na kusema kuwa siku zote atayasimamia maslahi ya Wamarekani.
No comments:
Post a Comment