msanii Rama Dee akiwa na Lady Jay Dee katika picha ya maktaba
Rama
Dee ni mmoja kati ya wasanii bora wa Rnb ambaye mara nyingi amekuwa na
misimamo tofauti na wasanii wengi ambao wanafanya aina hiyo ya muziki.
Katika kile ambacho kinaendelea juu ya sakata la madawa ya kulevya, Rama Dee ameingia katika kundi la wasanii wachache ambao wameweka mitazamo yao hadharani juu ya ukamataji wa wasanii na kuwekwa ndani.
Rama
Dee amesema “Mimi kama msanii,Siungi mkono wasanii kuwekwa ndani Ila
ninge muunga mkono Kama angeweza kuziba mirija ya Wauzaji Papa kuwafikia
wasanii na watanzania kwa ujumla!
"Toka
nipo mdogo wauza unga wanafahamika na majina yao yapo kwenye
mitandandao lakini sijawahi ona wakikamatwa wala kuonyeshwa kwenye
vyombo vya habari! Hata hao polisi pia sijaona picha zao!
"Wasanii
ni watu Kama watu wengine tu…so unapo anza kuaribu biashara zao kwa
sababu tu upo na power ya uongozi sidhani kama ni busara! :
"Ushauri wangu kaa na viongozi wenzio ambao walikutangulia kwenye uwongozi uliza why walishindwa then anzia hapo!
"Unajuwa haya mambo unaweza ona ya kawaida Ila yanaweza kuharibu maisha ya watu kuliko hata huwo Unga! Haswa wasanii. :
"Namuunga
mkono Nape kuwa kuna njia za kutumia ambazo zinalinda sheria ya
mtuhumiwa! Ila ukitumia nguvu bila Akili ni sehemu mojawapo ya kuwapatia
pesa Wanasheria bila msingi wowote! :
"Kukamata
watu kwa kuhisi ni utaratibu mbaya sana! Kumbuka kuna watu wapo na
chuki za maendeleo ya watu wengine.Unaweza ukasikia hata Tale anauza
unga ambae ni rafiki yako, sijuwi utafanyaje hapo.
"Mimi
naona plan yako imeanzia sehemu si sahihi rudi nyuma Anza tena ni hayo
tu, halafu hakuna movement nzuri Kama movement ya kutumia power ya
wasaniii na jamii kiujumla.
"Fanya kazi yako Mh. makonda waache wasanii watafute mkate wao wa kila siku! Rama Dee!"
No comments:
Post a Comment