Wafuasi wa Etienne
Tshisekedi kiongozi wa upinzani nchini DR Congo aliyefariki
wamekongamana katika mji mkuu wa Kinshasa ili kuonyesha mshangao wao wa
kifo cha kiongozi huyo.
Akiwa mpinzani maarufu wa viongozi
waliokuja na kuondoka nchin humo alitarajiwa kuongoza baraza la serikali
ya mpito kwa makubaliano ya rais Kabila kujiuzulu.Kiongozi huyo mwenye umri wa miaka 84 alifariki nchini Ubelgiji ambapo alienda wiki iliopita ili kufanyiwa ukaguzi wa kimatibabu.
Waziri wa habari amesema kuwa atafanyiwa maziko ya kitaifa.
Bw Tshisekedi alirejea mjini Kinshasa mwezi Julai katika makaribisho ya shujaa baada ya kukaa miaka miwili mjini Brussels kwa matibabu ya kiafya.
Kifo chake kinajri wakati muhimu wa DR Congo pamoja na ghasia za maandamano wakati ilipotangazwa kwamba rais Kabila atasalia madarakani hadi mwezi Aprili 2018.
Mwandishi wa BBC nchini DR Congo Anne-Marie Dias Borges anasema kuwa Tshisekedi alikuwa mtu maarufu mjini Kinshasa na kupewa jina la utani la 'Sphinx of Limete'.
Limete ni nyumbani kwake karibu na mji wa Kinshasa.
- Kipi kitarajiwe katika makubaliano ya amani?
Mazungumzo hayo ambayo bado hayajaisha yanahitaji serikali ya mpito pamoja na tarehe ya uchaguzi.
Bw Tshisekedi alitarajiwa kuongoza kamati ya mpito. Amekuwa akipigania demokrasia
Kwa zaidi ya nusu karne sasa taifa lote liliungana nyuma yake dhidi ya uongozi wa kiimla wa Mobutu Sese Seko ama uongozi wa Kabila baba na mwanawe.
Lakini wakati huo bw Tshisekedi alikuwa mnara wa kivyake.
Msimamo wake wakati mwengine huenda ulikuwa kikwazo kwa maendeleo ya kidemokrasia.
Katika kipindi cha miaka mitatu iliopita Bw Tshisekedi amekuwa akiugua ,mwanawe Felix amekuwa akichukua jukumu kubwa zaidi.
Hatma ya chama cha Union for Democracy and Social Progress UDPS inayumbayumba.
Viongozi wengine wachanga wa upinzani sasa wanaweza kupata fursa ya kuingia katika mazungumzo hayo ya mpito ambayo yanatarajiwa kuendelea chini ya uongozi wa viongozi wa makanisa nchini humo.
- Je, watu wamepokea vipi kifo chake?
Waombolezaji waliokongamana katika nyumba ya mwanawe mjini Kinshasa wanasema wana wasiwasi kuhusu hali ya baadaye.
''Mtu huyo alijitolea maisha yake pamoja na ujana wake wote.Mtu huyu alitufanya tufungue macho, alikuwa shujaa wetu''.
''Alikuwa taa ya Afrika. Alikuwa maarufu.Tumepoteza mtu muhimu sana'', mwanamke mmoja aliambia BBC.
Mwengine anasema wafuasi wake walikuwa wanamjua kuwa mtu ambaye ilikuwa vigumu kumhonga.
''Alikuwa mpinzani wa kihistoria.Mandela alikuwa wa kwanza na Tshisekedi alimfuata''.
Waziri wa maswala ya kigeni nchini Ubelgiji Didier Reynders alimtaja Tshisekedi kama mwanasiasa maarufu.
Ubelgiji inajiunga na raia wa DR Congo katika wakati huu wa huzuni ili kuona kwamba kazi yake inazaa matunda, kilisema chombo cha habari cha AFP.
- Ufanisi wake ni nini katika miaka 57 ya siasa?
Alisomea sheria chini ya ukoloni nchini Ubelgiji.
Harakati zake za kisiasa zilianza wakati wa uhuru wa taifa hilo mwaka 1960 ambapo alikabidhiwa nyadhfa za juu katika serikali ya kati mbali na utawala wa Kasaian uliokuwa mfupi.
Mnamo terehe 14 mwezi Novemba 2011, akiwa waziri wakati wa serikali ya dikteta Mobutu Sese Seko bw Tshisekedi alijimwaga katika siasa za upinzani 1980 wakati Mobutu alipoamua kufutilia mbali uchaguzi wote.
Akiwa kiongozi wa chama cha muungano wa Demokrasia pamoja na chama cha Social Progrees, amekuwa mpinzani wa serikali zote tangu wakati huo.
Wakati Mobutu alipolazimishwa kutengeza serikali ya muungano na upinzani, bw Tshisekedi alikuwa waziri mkuu mara mbili katika kipindi cha miaka miwili.
Alijiuzulu nyakati zote hizo alipokosana na Mobutu.
Chama cha Bw Tshisekedi hakikushiriki katika vita wakati wa vita vilivyozuka baada ya utawala wa Mobutu kuanguka 1997, na hivyobasi kupata umaarufu mkubwa kutoka kwa raia walioathirika na mapigano hayo.
Baada ya kususia uchaguzi mwaka 2006, ambao anadai ulifanyiwa udanganyifu ,bw Tshisekedi aliamua kujitokeza na kuhakikisha kuwa anashinda.
Kwa wengine aliamua mapema kujitangaza kuwa rais kabla ya kupigwa kwa kura hiyo.
No comments:
Post a Comment