·
Afukuza
wabunge, Ashindwa
·
Katiba
Cuf yambeba Lipumba
·
Msajili
wa Vyama akaza Uzi, Amtaka Afate Utaratibu
Na Mwandishi Wetu.
Ni dhahiri sasa hali ya mambo inazidi kwenda kombo kwa upande
wa katibu mkuu wa Chama cha wananchi Cuf Maalim Seif Sharif Hamad katika
mgogoro wa kiuongozi unaoendelea baina yake na mwenyekiti wa Taifa wa chama
hicho Profesa Ibrahim Lipumba, Jamvi la Habari linaweza kuthibisha.
Kitendo cha mwenyekiti wa chama hicho Prof. Lipumba kuwavua
uanachama wabunge nane na madiwani wawili wa viti maalum kitendo kilichoonyesha
kufuata taratibu zote za kisheria na katiba ya ndani ya chama hicho na hatimaye
kubarikiwa na ofisi ya Bunge, Tume ya taifa ya Uchaguzi na msajili wa vyama vya
siasa, kinaelezwa kumpagawisha katibu mkuu huyo na timu yake kiasi cha kuamua
nayeye kuwavua uanachama wanachama wengine kadhaa akiwemo mbunge na naibu
katibu mkuu anayekaimu majukumu ya katibu mkuu wa chama hicho kwa sasa kutokana
nan kutokufika ofisini kwa Maalim Seif tangu mwezi septemba mwaka 2016 Magdalena
sakaya na Maftah Nachuma ambaye pia ni mbunge wa mtwara mjini.
Katika barua yake kwa msajili wa vyama vya siasa, katibu mkuu
huyo amemueleza msajili huyo kuwa baraza
kuu la uongozi la taifa lililokutana visiwani Zanzibar hivi karibuni kuwa
wajumbe 43 kati ya 45 waliokutana visiwani humo wameridhia kuvuliwa kwao
uanachama na kwamba anamfamisha msajili juu ya jambo hilo.
Katika kile kinachoitwa kufuata sheria na katiba ya chama
hicho, msajili amemjibu kwa kumkumbusha kuwa yeye kama mlezi na mtunza
kumbukumbu wa shughuli zote za vyama vyote vya siasa nchini, anafahamu kwamba
ofisi ya katibu mkuu wa chama hicho imekaimishwa kwa Magdalena sakaya na
kwamba ofisi yake inahitaji kupokea
kwanza taarifa ya kutenguliwa kwa azimio hilo lililomuweka madarakani sakaya.
Taarifa za uhakika ambazo gazeti hili inazo zinasema kuwa
kwa sasa kambi ya maalim seif imeshakata tama juu ya mgogoro huo baada ya
kujitathmini na kujigundua kwamba katiba ya chama chao inampa nguvu mwenyekiti
wa chama hicho Prof.Lipumba na hivyo kujilaumu kila kukicha.
‘’unajua mwanzoni Maalim na Julius (Mtatiro) hawakujua
kwamba Prof angekuwa na nguvu kiasi hiki, ndio maana wakampuuza, lakini laity kama
wangejua namna ya ushindani wanaokuja kukabiliana nao hasa wa kikatiba nadhani
hali isingekuwa kama ilivyo hivi sasa’’. Alinukuliwa Saidi Makame wa Darajani
Zanzibar
‘’tatizo Prof. analindwa na ibara ya 117 ya chama, sasa kila
maalim na wenzetu kadhaa tukijaribu kutafuta namna ya kumpiku, linapokuja swala
la kisheria na mahakamani ama kwa msajili huyu bwana anatushinda tu’’. Aliongeza
mwanachama huyo wa chama hicho kikuu cha upinzani Zanzibar
Kadhalika, wakati hayo yanaendelea hivi karibuni mwenyekiti
wa chama hicho alifanikiwa kusajili upya bodi ya wadhamini wa chama hicho baada
ya ile ya awali kumaliza muda wake wa mujibu wa sheria jambo ambalo limezidisha
pigo kwa timu ya maalim seif kwa sababu bodi ya wadhamini ya chama chochote cha
siasa huwa moja tu inayosajiliwa na RITA na kwa mujibu wa katiba ya CUF bodi
hiyo ndio mamlaka pekee inayoruhusiwa kufanya usimamizi wa jumla wa chama hicho
ikiwemo kushtaki na kushtakiwa jambo linalohatarisha uwepo na uhalali wa kesi
zilizofunguliwa na bodi ya awali dhidi ya Msajili wa vyama na Lipumba juu ya
masuala kadhaa.
Aidha, kukwama huko kwa maalim Seif katika kile anachokiita
mapambano ya kukinusuru chama hicho, kunamfanya sasa abadili mawazo na
kujiandaa kuhamia chama kingine kikubwa cha upinzani hapa nchini chenye ngome
yake kuu Tanzania bara.
Taarifa zaidi zinaonyesha kwamba mpaka sasa maalim na watu
wake wameshakubali kuwa kisheria hawawezi kumshinda Prof. Lipumba na kwamba
wamebakiwa na njia mbili pekee ama wahame kuhamia chama hicho kikubwa cha
upinzani Tanzania bara ama waanzishe chama chao wenyewe kipya.
Mjadala unaoendelea hivi sasa baina ya wadau muhimu wa timu
ya maalim Seif ni kwamba iwapo uamuzi utakuwa ni kuwa wanahama, je watahama na
vyeo vyao walivyokuwa navyo wakiwa CUF kama hicho cha Katibu mkuu na vya baadhi
ya vya wakurugenzi au watahamia na kuwa wanachama wa kawaida jambo ambalo
wanahisi litawapunguzia nguvu ya kufanikisha agenda yao ya kuendelea kudai
maslahi yao ya kisiasa yanayotokana nauchaguzi mkuu uliopita.
Taarifa hizo pia zinaeleza kuwa mpaka sasa majadiliano ya
kina ya namna gani Maalim na timu yake watahamia chama hicho yameshaanza na
yanaratibiwa vizuri na wanasiasa kadhaa mashughuli hapa nchini wakishirikiana
na baadhi ya wafanyabiashara wenye vinasaba na chama hicho.
Ikiwa mwanasiasa huyo atahama chama hicho na kujiunga chama
kingine kama njia ya kufikia lengo lake la kisiasa, kitakuwa ni kielelezo
mahsusi cha kudhibitiwa na Prof. Lipumba katika kuijua na kuifahamu katiba ya
chama hicho na pia ndio utakuwa mwisho wa ushirikiano wa Umoja wa Katiba ya
Wananchi UKAWA.
Alipotafutwa na gazeti hili msajili wa vyama vya siasa Jaji
Fransis Mutungi, ameendelea kusisitiza kwamba ofisi yake itaendelea kufanya
kazi za kuvisimamia vyama vyote vya siasa vilivyopo hapa nchini kama sheria
iliyoviasisi inavyosema na kuongeza kuwa kinachoendelea ndani ya Cuf ni matokeo
ya utekelezaji wa katiba ya chama hicho ambacho wameitunga wenyewe.
‘’mimi ofisini kwangu ninasajili vyama baada ya kuzipitia
katiba zao na kujiridhisha kuwa hazikiuki masharti ya sheria za nchi,
nikizipokea na kujiridhisha siongezi wala kupunguza kitu chochote zaidi ya
kuzisajili, na kama ujuavyo katiba ikishapitishwa kinachofuata ni kutekelezwa
tu’’. Alisema Msajili Mutungi
No comments:
Post a Comment