Tume ya uchaguzi nchini Angola
imesema kwamba matokeo ya awali ya uchaguzi mkuu uliofanyika siku ya
Jumatano unaonyesha chama tawala cha MPLA kinaongoza.
Inasema
kwamba MPLA imeshinda takriban robo tatu ya kura zote mpaka sasa, huku
chama kikuu cha upinzani UNITA kikiwa na asilimia 25.Waziri wa zamani wa ulinzi Joao Lourenco, anaonekana kuchukua nafasi ya Rais wa muda mrefu Jose Eduardo dos Santos.
Santos ameiongoza Angola kwa karibia miaka 40.
No comments:
Post a Comment