Paris Saint- Germain wanakaribia
kukamilisha usajili wa mshambuliaji wa Monaco Kylian Mbappe, 18, na
Fabinho kwa pauni milioni 200. Mbappe pekee atagharimu pauni milioni
128. PSG pia watamtoa na Lucas Moura katika mkataba huo. (Sky Sport)
Barcelona wamekubali kuwa Liverpool hawatowauzia Philippe Coutinho, 25, mwezi huu. (Mirror)Kiungo wa Real Madrid Mateo Kovacic, 23, amekubali kwa kauli kujiunga na Liverpool kuziba nafasi ya Philippe Coutinho iwapo ataondoka kwenda Barcelona. (Daily Mirror)
Liverpool bado wanataka kumsajili Virgil van Dijk na watakuwa tayari ikiwa Southampton watabadili msimamo wao kuhusu beki huyo. (Liverpool Echo)
Diego Costa, 28, ameambiwa na Atletico Madrid atafute suluhu na Chelsea kwanza kabla ya kununuliwa kwa pauni milioni 25. (Sun)
Kiungo wa Juventus Claudio Marchisio anataka kuondoka Italia na kujiunga na Chelsea. (Corriere della Sera)
Manchester City wanakaribia kukata tamaa ya kumsajili beki wa West Brom Jonny Evans, 29, na badala yake watapanda dau la pauni milioni 20 kumtaka beki wa Middlesbrough Ben Gibson, 24. (Independent)
Tottenham wanajiandaa kupanda dau la pauni milioni 20 kumtaka kiungo wa Everton Ross Barkley, 23, ingawa wanakabiliwa na ushindani kutoka kwa Chelsea pia. (Telegraph)
West Ham tayari wanatafuta kocha wa kuziba nafasi ya Slaven Bilic ambaye amekuwa na mwanzo mbovu wa msimu. (Mirror)
Manchester United wanamtaka kinda wa Fulham Ryan Ssesegnon, 17, ambaye pia anasakwa na Tottenham. (Sky Sports)
Valencia wanakaribia kukamilisha usajili wa mkopo wa kiungo wa Manchester United Andreas Pereira. (Cadena Ser Valencia)
Bayern Munich wanafikiria kumsajili mshambuliaji wa Paris Saint-Germain Julian Draxler ambaye hatma yake iko mashakani baada ya kuwasili kwa Neymar. Draxler pia ananyatiwa na Arsenal, Liverpool na Manchester United. (Westdeutsche Allgemeine Zeitung)
Meneja wa Leicester Craig Shakespeare amesema hatma ya Riyad Mahrez, 26, na Danny Drinkwater, 27, pengine haitafahamika mpaka siku za mwisho za dirisha la usajili. (Leicester Mercury)
Beki wa kati wa Southampton ameonekana akifanya mazoezi na kikosi cha chini ya miaka 23 baada ya kuwasilisha maombi ya kuondoka. (Express)
Chelsea hawatopanda dau la kumtaka Virgil van Dijk hadi pale Southampton watakapokuwa tayari ingawa klabu hiyo imesema beki huyo hauzwi. (Telegraph)
Chelsea huenda wakaweza kumsajili Antonio Candreva, 30, kwa sababu Inter Milan inatafuta fedha za kutaka kumsajili Suso, 23, kutoka AC Milan. (Gazzetta dello Sport)
Galatasaray wanataka kumsajili beki wa Arsenal Kieran Gibbs. (The Times)
Crystal Palace wamepanda dau la pauni milioni 15 kumtaka beki wa Tottenham Kevin Wimmer, ambaye pia anasakwa na West Brom na Stoke. Spurs wanataka pauni milioni 20. (Daily Mail)
Habari zilizothibitishwa tutakujuza mara zitakapothibitishwa. Kwa orodha kamili ya wachezaji waliokamilisha rasmi usajili bofya link hii: http://www.bbc.co.uk/sport/football/transfers
Tetesi nyingine kesho tukijaaliwa. Uwe na wiki njema.
No comments:
Post a Comment