na mwandishi wetu.
Ni
kama Rais wa Jamhuri ya muungano wa
Tanzania Dk. John Pombe Magufuli, anakibarua kizito kunusuru upotevu
unaoweza
kujitokeza wa usimamizi wa mali za chuo kikuu cha Dodoma zenye thamani
ya zaidi ya shilingi bilioni 400 taarifa ya mdhibiti na mkaguzi mkuu
wa hesabu
za serikali,CAG ya mwaka 2014/2015 inaeleza.
Taarifa hiyo inaeleza kuwa serikali
kupitia mashirika ya mifuko ya hifadhi za jamii ilijenga chuo hicho kikuu
kikubwa kuliko vyote katika ukanda huu wa afrika mashariki kwa mkataba wa
ujenzi,ubunifu, umiliki na uendeshaji wa pamoja na kwamba baada ya kukamilika
mali za chuo hicho zilitakiwa kumilikiwa na mashirika hayo ndani ya miaka kumi
lakini mpaka taarifa hiyo inatoka jambo hilo halikuwa limefanyika.
‘’Shirika la Hifadhi ya Jamii (NSSF),
Mfuko wa Pensheni kwa Wafanyakazi wa Umma (PSPF), Mfuko wa Pensheni kwa
Wafanyakazi wa Serikali za Mitaa (LAPF), Mfuko wa Bima ya Afya (NHIF) na Mfuko
wa Pensheni wa PPF yalitumia jumla ya Shilingi bilioni 415.4 kujenga Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM), chini ya makubaliano
ya buni, jenga, endesha, na kisha hamisha miliki baada ya miaka kumi (10)’’. Inasema sehemu ya taarifa hiyo ya CAG
Totauti na ilivyotarajiwa, taarifa hiyo
inasema kwamba mpaka sasa majengo hayo hayajaingizwa kwenye kumbukumbu za chuo hicho wala mashirika hayo na hivyo
kuhatarisha upotevu wake,
‘’Majengo haya hayapo kwenye vitabu vya
Chuo Kikuu cha Dodoma wala katika vitabu vya Mifuko ya Hifadhi ya Jamii husika.
Japokuwa Mlipaji Mkuu wa Serikali amejibu kuwa majengo haya yataingizwa kwenye
vitabu vya Chuo Kikuu cha Dodoma katika mwaka wa fedha wa 2013/2014, bado UDOM
imepewa Hati Yenye Mashaka kutokana na kutokuwepo kwa majengo hayo kwenye
vitabu vyake.’’ Imeongeza taarifa hiyo
Kufuatia
uchunguzi huo, mdhibiti na mkaguzi mkuu huyo wa serikali anaendelea kusisitiza umuhimu
wa majengo hayo kuingizwa kwenye vitabu vya chuo hicho cha UDOM kama alivyopendekeza
awali ili kukiondolea chuo hicho shaka ya kuendelea kutopata hati safi.
Hayo yanatokea huku kukiwa na msuguano
wa chinichini baina ya wafanyakazi wa taasisi mbalimbali hapa nchini na
serikali juu ya swala la Fao la kujitoa ambapo serikali imebadili sharia ili
kuzuia fao hilo.
Sambamba na hilo la fao la kujitoa,
wachambuzi wa mambo wanasisitiza kuwa kuna haja ya serikali kusimamia sawa sawa
faida zinazotakiwa kutokana na ujenzi wa chuo hicho kwa kuwa ujenzi wake
umetokana na fedha za watanzania na hivyo wafanye kila linalowezekana kukamilisha
umiliki huo wa mali ili kuhakiki ulinzi wa pesa zao.
‘’unajua kibiashara, UDOM ni uwekezaji
wa pesa zetu, sasa na kila uwekezaji lazima uzalishe faida, na kama mpaka sasa
hawajakamilisha umilikishaji wa mali hizo kwa mashirika yetu maana yake
uwekezaji huo hautatulipa na pesa zetu zitapote bure, serikali inatakiwa
ichukue hatua za makusudi kwenye hilo’’. Alisema Omari kihampa mwanachama wa
moja ya mifuko ya hifadhi za taifa.
‘’bilioni 415 ni nyingi sana aisee,
pamoja na kuipongeza serikali kujenga chuo kupitia fedha zetu lakini lazima
fedha hizo zituhakikishie usalama wetu tukistahafu, kuacha kuendelea hivi
ilivyo itakuwa ni kuzipoteza’’. Ananukuliwa Mariam Jamlisheed mtumishi wa
wizara moja hapa nchini.
No comments:
Post a Comment