WADHAMINI WETU
Friday, September 30, 2016
BREAKING NEWS: MBOWE AVUNJA UKUTA RASMI, AMSHUTUMU LIPUMBA MGOGORO CUF, AMVAA MSAJILI WA VYAMA
Mwanachama wa Chadema Ben Saa nane ameandika taarifa hizi katika mtandao wa Jamii forums.
akiripoti mkutano wa Mbowe na waandishi wa habari uliofanyika leo tarehe 30.09.2016 katika makao makuu ya chama hicho kinondoni ufipa.
-Tayari Waandishi wa Habari wameketi
-Viongozi wakuu Wakiongozwa na Mhe.Freeman Mbowe wanaingia Ukumbini
Hotuba kwa Taifa itaanza hivi Punde
Saa 12:15 baada ya İtifaki kuzingatiwa, Mwenyekiti Taifa anaanza kuhutubia
Anawapa pongezi wanahabari kwa kufika kwa wingi .Anasema
- Jana kamati ndogo ya kamati kuu imekutana tena ili kufanya marejeo kuhusu yalipofika majadiliano ya Viongozi wa Dini na Rais baada ya kukiomba Chama kisitishe Operesheni UKUTA
-Hadi jana na hadi sasa viongozi wa Dini hawajaleta Taarifa yoyote kuhusu kama waliweza kukutana na Rais
-Sisi kama Chama Cha Siasa tumetekeleza wajibu wetu
-Tunawaheshimu viongozi wa Dini na Tutaendelea kuwaheshim
-Sasa kama chama cha Siasa tutaendelea sasa kutekeleza wajibu wetu
-Kazi ya siasa sio kazi ya siku moja.Tutaifanya kazi hii endelevu ya kupambana na Utawala kandamizi unaowaumiza wananchi kwa kukanyaga sheria na katiba na pia utawala unaokwepa wajibu wake lakini hautaki kukosolewa.
Maisha magumu kwa Watanzani lakini Mtawala asiye na Mbinu mbadala hataki wananchi wapaze sauti
-UKUTA ni Fikra. Yaani fikra za kupambana na ukandamizaji wa haki na demokrasia.Mapambano haya hayahusishi CHADEMA pekee.
Kwa muktadha huu tuna wajibu wa kufanya siasa ndani ya wigo uliowekwa nchini na pia kimataifa
-Tanzania sio kisiwa.Ndio maana chama kiliona Umuhimu wa kutuma ujumbe Mzito kwenye ziara maalumu nchi za Ulaya .Nchi za Ujerumani na Denmark kuendelea kuujulisha Ulimwengu juu ya ukandamizaji mkubwa wa haki za binadamu na Demokrasia kinyume na jinsi ambavyo serikali imekua ikijipamba kuwa ya amani na Utulivu
Hiyo ilikua ziara ya awamu ya kwanza
Bado Ujumbe Mwingine utatumwa kwenye nchi nyingine kama Uingereza,Marekani,Canada , Malaysia,Japan na hata ndani ya Umoja wa Afrika na kwenye mtangamano wa kikanda kama SADC na EAC
Tunataka utawala ujue mipaka yetu haiishii Namanga na Tunduma
Tutatumia Taasisi za kimataifa
Kurugenzi yetu ya Sheria inaendelea na kazi nzuri ya kutumia Mahakama za ndani na za kimataifa kupeleka mashauri yetu
-Viongozi wetu mbalimbali wanakabiliwa na kesi mbalimbali zinazoitwa kesi za Uchochezi
-Tumesikia Juzi polisi katika kujihalalishia uovu wao walipojua CCM sasa wanakaribia kuanza vikao vya ndani wanatangaza kuruhusu Mikutano ya ndani
-Sisi tunaandaa mikutano ya kisiasa nchi nzima
-Ukuta wa Oktoba Mosi utasogezwa mbele kwa Tarehe Maalumu
-Rais anatumia jeshi kupambana na Sisi lakini hakuweza kuwatumia kwenye Tetemeko Kagera na kuwaacha raia wetu wakiteseka
-Leo anatumia jeshi kuumiza Raia na vituko vingine eti kufagia na wengine kupanda Miti
-Rais aliyekwepa mikutano ya kimataifa kwa kisingizio cha Tetemeko la Ardhi Kagera hakufika,Hakupeleka jeshi ila alikaa İkulu akisubiri Ripoti
MİGOGORO İNAYOPANDİKİZWA
-Prof.Lipumba amekituhumu CHADEMA kuhusika na migogoro ndani ya CUF
Sikusudii kumjadili Lipumba.Maana sitaki kumpa nafasi na umuhimu aliokuwa nao zamani
He's politically İrrelevant.
CHADEMA kitashirikiana na chama chochote chenye dhamira ya dhati
CUF tunaheshimu maamuzi yao ya vikao halali
-Natoa Rai kwa Wanachama wa CHADEMA nchi Nzima kupuuza kauli za Prof.Lipumba na tuache kumpa ushirikiano wowote kwa kuwa ni msaliti wa mageuzi anayetafuta kuangamiza Upinzani
MSAJİLİ WA VYAMA VYA SİASA
-Jaji Mutungi amechochea mgogoro CUF na hatuna sababu za kumuheshimu
-Atambue kuwa tutasimama na CUF na ajue yeye sio Msajili wa kwanza.
Mbinu zake na Watawala zitashindwa
-Serikali inatumia nguvu kubwa sana na taasisi nyingine kununuliwa
-Kwa mfano TWAWEZA .Upo ushahidi kuwa walipewa pesa na serikali kupika Utafiti siku moja kabla ya UKUTA kwa bahati mbaya hawakupika kwa kiwango cha kuifanya ripoti ionekane kuwa na sifa za kiutafiti
-Kwa hiyo ndugu wanahabari sisi kama Chama tumebadilisha Tarehe ya kuanza Kufanya maandamano na mikutano
Sasa wale walojiandaa kushambulia na kuua watu wasubiri
Sisi tunabadili mbinu tukihusisha mbinu za kimapambano na kidiplomasia
-Mmeona matokeo ya Mbinu hizi sasa Jumuiya ya Kimataifa imeanza kuona ukandamizaji wa Demokrasia nchini na Udikteta Uchwara ulioshamiri
Tulipowapa Muda viongozi wa Dini wao watawala walidhani tumelala kumbe tumevuka mipaka na kuingia anga za kimataifa
-Sasa serikali inahaha na kutapatapa baada ya kushitakiwa kwenye Baraza la Haki za Binadamu la Umoja wa Mataifa
Sasa tutaendelea kufanya vikao vya kimkakati nchi nzima na pia mikutano
Tutaendelea kuhabarishana kadiri tunavyopiga hatua katika maandalizi na Mikakati yetu ambayo haitawapa fursa watawala kujipanga
Asanteni
Mwisho:Sasa Mwenyekiti Taifa na Viongozi wakuu anaongea na Baadhi ya Vyombo vya Habari vya Kimataifa kisha ataelekea kwenye kikao nyeti cha Ndani,Kikao cha Kimkakati
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment