WADHAMINI WETU

WADHAMINI WETU

Thursday, September 29, 2016

HONGERA TENA MAGUFULI - MCHANGE


Jana wakati unazindua na kukabidhi ndege mbili 'mpya' ATCL nimekusikiliza kwa Makini mno Rais MAGUFULI,
nimefurahishwa zaidi na Dhamira yako ya kutaka kulifikisha taifa sehemu fulani.
Ulipotangaza Kununua ndege mbili kubwa ambapo moja kubwa na nyingine kubwa zaidi ni kama ulikuwa unausemea moyo wangu.
Mimi na watanzania wengine wengi wetu ni wajasiriamali wadogo.
Tunapojichanga changa tukipata vidola elf 5 tunakimbilia china kuchuuza na kuleta vibiashara hapa nyumbani kuganga njaa.
Mimi ni Muafrika zaidi, siamini katika mashirika ya ndege ya kiarabu kama emirates au Qatar, Wala ya kizungu
Kwa sababu hiyo mara zote ninaposafiri kimataifa hasa kuelekea China au Hong Kong Mimi husafiri na Ethiopian Airlines.
Nachukuliwa DSM mpaka Bolle International Airport Addis Ababa.  Kusubiri ndege ya kunipeleka kituo cha mwisho.
Pale nakutana na watu wa mataifa mbali mbali ya Africa hasa Africa magharibi.
Wakenya wenzetu wako sensitive Sana na utaifa wao 9/10 husafiri kwa ndege yao Kenya Airways - KQ.
Mara zote nikiwa Bolle kuanzia nashuka mpaka na connect ndege nasononekaga Sana.  Hakuna walichotuzidi kimuonekano, lakini wao wamewekeza Sawa Sawa katika ndege.  Mpaka unaona wivu.
Jana MAGU umegusa ndoto yangu, ndoto ya Mimi kutoka moja kwa moja nyumbani,  kwenda Airport na nikipaa, nikitua nipo China au popote nitakapokuwa ninaenda.  Hongera Sana.
Ndoto hii na itimie hata kesho Baba,  ndoto ya watu wa Malawi,  Zambia,  Congo,  Uganda, Burundi na kwengineko kuacha kwenda umbali mrefu mpaka Addis au Joburg kuunganisha badala yake Kuja Dar,  Shukrani Sana.
Ndoto ya kuwa na ndege ambayo wasafiri wake watasoma vitabu vya kitanzania wakiwa angani,  watatazama miziki ya kitanzania wakiwa angani,  watakula chakula cha kitanzania na watazungumza lugha ya kitanzania - hii si ndoto ya kubezwa hata kidogo.
Ndoto ambayo itanifanya nisisafiri tena masaa 19 kufika China Bali masaa nane na nusu tu mpaka tisa Sawa na ndugu yangu aendae Arusha kwa Basi akitokea Dar - ndoto nzuri Sana hii.
Hii ni Ndoto itakayonisaidia zaidi kupunguza gharama za Usafiri mpaka asilimia 40 ya ninazolipa Sasa kwenda ughaibuni.
Ndoto hii itanisaidia kuhakikisha usalama wa mizigo yangu, maana hatari ya kupotea au kuchelewa kutokana na connections itakuwa imepungua mno kwa kuwa ni moja kwa moja.
Ndoto itakayowafanya watalii Kuja moja kwa moja Tanzania Kuona vivutio vyetu,  hakukuwa na haja ya mtalii kupitia Kenya halafu Kuja mikumi Kuona simba ambao angeweza kuwaona Tsavoy Kenya.
Hii ni ndoto itakayonifanya nijivunie zaidi kuwa mtanzania maana kwa wasiojua, moja Kati ya kielelezo chepesi cha taifa kimataifa ni shirika la ndege.
Hongera Sana kwa Dhamira hii,  Hongera tena kwa kututia moyo na matumaini yaliyopotezwa na serikali ambayo wewe mwenyewe pia ulikuwemo kwa zaidi ya miaka 20 lakini si haba unatusitiri Sasa.
MUNGU AKUTIE NGUVU INSHAALLAH.
Ndimi
Habib Mchange

No comments:

Post a Comment