waziri wa TAMISEMI George Simbachawene
Na Mwandishi wetu
Waziri
wan chi ofisi ya Rais tawala za mikoa na serikali za mitaa mheshimiwa George
Simbachawene ametakiwa kuingilia kati tabia za baadhi ya watendaji wa
halimashauri mbalimbali hapa nchini kutokana na watendaji hao kulalamikiwa
kutokusimamia sharia katika masuala kadhaa hasa yanayohusu manunuzi na
kusababisha mgogoro na mgongano wa kimaslahi kunakopelekea kudorora kwa
utolewaji wa huduma za msingi za kijamii na maendeleo.
Akizungumza
na gazeti hili mmoja wa watumishi wa wizara hiyo ameshauri kuwa ni vema suala
hilo akaachiwa waziri mwenyewe kwa sababu yeye ndie msimamizi wa moja kwa moja
wa wizara hiyo na kwamba maamuzi yake ndio huwa ya mwisho na akiamua kuchukua
nidhamu kwa muhusika wala haitazuilika.
Kadharika
madiwani kadhaa wa halimashauri ya wilaya urambo ambapo wiki iliyopita gazeti
hili lilitipoti kuhusiana na kadhia ya mhandisi mkuu wa ujenzi wa wilaya hiyo
kujihusisha na tabia zinazoendana ama kuonekana kukiuka taratibu za kimanunuzi
na ukiukwaji wa sharia wa wazi.
‘’sisi
kwenye kikao tutamjadili na kuliazimia swala lake, lakini pia tutamtaka waziri
simbachawene amuwajibishe haraka iwezekanavyo, maana sina imani kama mkurugenzi
anaweza kutengua nafasi yake’’. Alisema diwani mmoja ambaye jina lake
linahifadhiwa
‘’unajua
huyu bwana alishawahi kufikishwa mpaka Takukuru kuhusiana na masuala hayahaya,
lakini inaonyesha kwamba ama amenogewa ama amewazidi ujanja hao mambwana wa
Takukuru, hivyo Simachawene anaweza kutusaidia kabisa kabisa kumalizana na huyu
bwana’’, aliongeza diwani huyo
Hayo
yanatokea wakati wiki iliyopita gazeti hili lilipoti kuhusiana na kuwepo kwa
tafiti zikimuonyesha Rais wa jamhuri ya muungano
wa Tanzania Dk. John Pombe Magufuli kuwa kiongozi anayependwa zaidi na wananchi
wake hasa kutokana na tabia yake ya kusimamia sawa sawa sheria na kutumbua
majipu kwa kuwaondoa wabadhilifu serikalini na katika taasisi mbalimbali za
umma,baadhi ya wasaidizi wake katika ngazi za halimashauri wanaweza kumkwamisha
kutokana kutokusoma alama za nyakati hasa katika kipindi hiki cha utawala wa
awamu ya tano wenye kauli mbiu ya hapa kazi tu.
Tuhuma
nzito za mgogoro wa kimaslahi zinamkabili
Mhandisi mkuu wa halimashauri ya wilaya urambo mkoani tabora bwana
Makori Kisare zikimuhusisha na kujilipa mamilioni ya shilingi kupitia kampuni
ambayo inahusishwa naye kuwa mbia ya Mispa
Constraction Co. Ltd yenye makao yake makuu mkoani mara.
Taarifa
za uhakika ambazo gazeti limezipata zinasema kuwa mhandisi huyo wa wilaya
amekuwa akiisababishia hasara serikali kwa kupokea kazi zilizofanywa chini ya
kiwango kutokana na tabia yake ya kuitumia kampuni yake hiyo kuomba kazi ambazo
yeye mwenyewe anashiriki kuziandaa na kuzitangaza na hatimaye kampuni yake hiyo
kushinda zabuni hizo hivyo kuingia katika mgogoro wa kimaslahi.
Taarifa
hizo zinasema kuwa kampuni yake hiyo iliyosajiliwa
tarehe 22 mwezi wa tisa mwaka 2010 ikiwa na namba ya usajili74055 ya sanduku la
barua 669 musoma mkoani mara, mpaka sasa imekuwa ikifanya kazi katika maeneo
kadhaa hapa nchini hasa katika halimashauri ambazo ama amewahi kufanya kazi au
ana maswahiba zake wanaofanya kazi hapo, mifano ikiwa ni halimashauri za urambo na Dodoma na
Jamvi
la habari linaweza kuthibitisha kuwa, mhandisi huyo baada ya Kuteuliwa kuwa
Mhandisi ujenzi Wilaya ya Urambo alianza jipatia kazi kupitia Kampuni hiyo kwa
kutumia cheo chake cha ukuu wa Idara ya Ujenzi, jambo linalosababisha
kukosekana kwa ufanisi na uwajibikaji kwa kuwa muwajibishaji ndie anayefanya
kazi.
Baadhi
ya miradi ambayo hata hivyo imeonyeshwa kufanywa chini ya kiwango ni ule wa ujenzi wa mitaro uliopo Urambo mjini wenye thamani ya Shilingi Milion
Sabini na tano (75million) na kuendelea kujipatia kazi nyingine ya matengenezo
ya Barabara kuelekea standi mpya yenye thamani ya Milion themanini na tano
(85million).
Sambamba
na hayo mhandisi huyo analalamikiwa na baadhi ya wasaidizi wa idara yake katika
halimashauri hiyo kwa kuipendelea wazi
wazi kampuni yake huku akijua navunha utaratibu na taratibu za manunuzi
zinazoelekeza kwamba inapokuwa walioomba kazi wengi wanasifa zinazofanana, basi
aliyeomba kwa kiwango cha chini cha malipo ndiye atapaswa kupewa kazi hiyo, na
kinyume chake ameamua kujipa kazi huku kampuni yake ikiwa imependekeza gharama
kubwa.
Akizungumza
kwa ombi la kutoandikwa gazetini mmoja wa watendaji wa ofisi hiyo amesema
anashangaa kuona mabadiliko haya ya kiutendaji tangu kuingia kwa mkuu huyo mpya
wa idara.
‘’Hebu
fikiria, katika mradi wa kazi ya utengenezaji
wa Barabara na mitaro ya Urambo mjini (Majengo ya Tabora) ilitender kwa
Shilingi milioni Miamoja na Tisini na Tisa (199million) na wakati nyingine
zalitenda kwa milion miamoja sabini na
tatu (173million) na kwa milioni miamoja na themanini (180million), lakini
aliamua kujipa yeye kazi hiyo licha ya kwamba gharama zake zipo juu’’. Alisema
‘’akikupenda
bossi, au kama unakula naye vizuri wala hupati shida, ona alivyowapa kazi
marafiki zake wa wengine Nebrix japo wameshindwa kufikia kiwango’’ aliongeza
Taarifa
zinaonyesha kwamba Mhandisi huyo
anatuhumiwa kutokuzingatia sharia wala kanuni za manunuzi na kwamba mfano wa
zabuni ya za Kuweka vifaa vya Maabara aliamuru apewe Nebrix Ltd kazi ambayo kwa
kiwango kikubwa imeshindwa kufainya vema
kwa kupasuka pasuka kwa mipira ya gas na maji ( Value for Money) lakini licha
ya hayo aliendelea kuipatia kampuni ya hiyo
miradi yote ya Wilaya ya Urambo huku wadadisi mambo wa halmashauri husika wakivujisha
kwamba kampuni hiyo
ilitumika kama daraja la yeye kujikwapulia fedha hizo, na hata wazabuni wengine
walipo omba kazi hizo walikataliwa na akapewa mtu mmoja kwa Wilaya nzima.
Alipotafutwa
na gazeti hili kupitia namba yake ya simu yake ya mkononi ambayo pia inaonekana
kwenye taarifa za wasifu wa kampuni hiyo, mhandisi huyo amekanusha kuwa mmoja
wa wamiliki wa kampuni hiyo na kwamba alitoka huko miaka kadhaa nyuma na sasa
sio tena muhusika.
‘’kuhusu
mispa kama mispa kwanza sikuwa mmiliki, nilikuwa mshauri tu, mimi nilikuwa
mmiliki wa kampuni nyingine kabisa ila mispa nilikuwa mshauri tu wa masuala mbalimbali
na kwa sasa sina uhusiano nayo’’. Alinukuliwa bwana Makori.
Kupatikana
kwa majibu hayo ya bwana makori kunaibua maswali kadhaa ikiwemo ya kwamba Mispa
ilijua kwamba makori ndie mkuu wa idara ya ujenzi wa wilaya ya urambo na wakati
anaipatia kazi alikuwa anajua au hajui kama ile ni kampuni anayodai kuwahi kuwa
mshauri wake na kama alitangaza maslahi yake popote.
‘’Mkuu
ameshawahi kubadilisha vipuli vizima vya magari ya serikari na kuviuza kwa bei
ya chini kwa rafiki zake na kuweka
vipuli vibovu ambavyo baada ya siku chache hufa kabisa na kuandikia madokezo
ili vinunuliwe vingine, tukio ambalo pia limewahi kutokea katika halimashauri
jirani ya kaliua ambapo liliwahi kukamatwa fulushi likwa na Engine mbovu ya
Land Cruizer amboyo ilikua ipo tayari kubadilishwa, hilo lilishuhudiwa na
watumishi kazaa ila Mkurugenzi alie kuwepo ambae sasa amehamishiwa Jijini
Arusha ambapo aliamua kulizima suala
hilo, huu ni kama ugonjwa wa kila halimashauri hapa nchini’’.
Malalamiko
kama haya ya urambo, yanasemwa kuwa ndio tabia ya watendaji na watumishi wa
serikali na mashirika ya umma wa maeneo mengi (gazeti hili linayo mifano mingi)
na kwamba kazi nyingi zinazotangazwa hutangazwa tu kugelesha lakini kampuni zao
wenyewe na ambazo nyingine hazina hata ofisi hupewa kazi hizo na kusababisha
ufanisi wa chini ya kiwango.
Juhudi
za kumtafuta mkuu wa mkoa wa tabora mheshimiwa Agrey Mwanri kulizungumzia suala
hilo zinaendelea na na katika kumsaidi na kuunga mkono jitihada za Rais Dk.
John Pombe Magufuli kurudisha nidhamu serikalini na kuwafikishia watanzania
maendeleo kwa kuwapatia huduma zinazostahili kwa wakati bili upendeleo, gazeti
hili litaendelea kuujulisha umma hatua kwa hatua kuhusiana na jambo hilo na
mengine yanayofanana na hili..
No comments:
Post a Comment