WADHAMINI WETU

WADHAMINI WETU

Thursday, September 29, 2016

Upinzani Sudan Kusini waapa kuangusha utawala wa Kiir

http://gdb.voanews.com/6868A570-13E1-4F60-AC9C-13DA97F8B543_w987_r1_s.jpg  Kundi la upinzani huko nchini Sudan Kusini ambalo limeapa kuuangusha utawala wa Rais Kiir

Maafisa wa kundi la South Sudan Democratic Movement Cobra Faction ambalo zamani liliongozwa na David Yau Yau kwa mara nyingine wameapa kufanya vita dhidi ya serikali ya Rais Salva Kiir kwa sababu wanaishutumu haijatekeleza kwa upande wake matakwa ya mkataba wa amani uliotiwa saini mwaka 2014.
Yau Yau alitia saini mkataba wa amani na Rais Kiir mwezi mei mwaka 2014 ambao ulitoa njia ya kutambua eneo la Greater Pibor kuwa na mamlaka yake yenyewe.


Wakati huo huo Yau Yau aliteuliwa kuwa naibu waziri wa ulinzi lakini baadhi ya viongozi wengine wa SSDM-Cobra Faction wanasema utawala wa Kiir ulipuuza mikataba mingine yote ya majimbo.
Kiongozi mpya wa kundi la SSDM-Cobra Faction ni Luteni Jenerali Khalid Botrus Bora ambapo msemaji wake Kernoy Philip Kadal alifanya mkutano na waandishi wa habari mjini Nairobi nchini Kenya hapo Jumanne na kusema kundi litaungana na wanamgambo wengine katika juhudi za kuuangusha utawala wa Kiir.

No comments:

Post a Comment