WADHAMINI WETU

WADHAMINI WETU

Thursday, September 29, 2016

UpinzaniZambia unakanusha kugawanyika baada ya uchaguzi

VOA
      Aliyekuwa mgombea urais wa UPND, Hakainde Hichilema akizungumza na wafuasi wake.

Msemaji wa chama kikuu cha upinzani nchini Zambia cha United Party for National Development-UPND anakanusha kwamba chama hicho kimegawanyika baada ya kushindwa uchaguzi wa urais uliofanyika Agosti ambapo Rais Edgar Lungu aliyepo madarakani aliibuka mshindi.
Chama hicho cha upinzani kimemfuta uanachama makamu wake wa rais anayesimamia masuala ya siasa, Canius Banda. Pia msemaji msaidizi wa chama cha UPND, Edwin Lifwekelo alijiuzulu.
Vyombo vya habari nchini Zambia pia vimemkariri Edward Mumbi, mshauri maalumu kwa mgombea urais wa chama cha UPND, Hakainde Hichilema, kwamba amejiuzulu nafasi hiyo kwenye chama akielezea ni kutokana na sababu za kifamilia.

No comments:

Post a Comment