Michuano ya klab bingwa barani ulaya
inaendelea katika hatua ya makundi ambapo Usiku wa kuamkia leo michezo
michezo nane ilipigwa katika viwanja tofauti.
PSG ikiwa ugenini iliibuka na ushindi mnono wa 3-1 dhidi ya Ludogorets Razgrad ya nchini Bulgaria.
Besiktas imeenda sare ya 1-1 dhidi ya Dynamo Kyiv. Huku SSC Napoli ikiibuka na ushindi wa 4-2 dhidi ya Benfica.
Borussia Moenchengladbach nayo ikiwa nyumabi imekubali kichapo cha 2-1 dhidi ya Barcelona. Na mchezo wa kushangaza wa funga nikufunge ulikuwa kati ya Celtic na Manchester City, ambazo zilienda sare ya 3-3.
Atletico Madrid nayo ikiwa nyumbani iliibuka na ushindi mwembamba wa 1-0 dhidi ya Bayern Munich. Na FC Rostov ikiwa nyumbani ililazimishwa sare ya 2-2 dhidi ya PSV Eindhoven
No comments:
Post a Comment