Diambond Platnumz.
Msanii Diamond Platnumz ambaye ameshiriki kukifanyia kampeni chama cha mapinduzi katika chaguzi mbili mfululizo, wiki hii amefunguka kuhusiana na serikali ya chama hicho na kuitaka isijisahau hasa kuwasahau watu walioshiriki kuhakikisha inakaa madarakani na kuboresha miundombinu ya maeneo mbalimbali na kuacha kupendelea maeneo maalum tu jijini Dar es salaam.Akihojiwa katika kipindi cha kijamii cha The weekend chat show cha Clouds Tv, Diamond Platnumz msanii maarufu nchini Tanzania ameonyesha kusikitishwa kwake na kitendo cha serikali kushindwa kutengeneza barabara za maeneo ya wanaoishi watu wa kawaida kama temeke, tandale na kwake madale tegeta na badala yake wanaendelea kutengeneza kila siku maeneo yanayosemekana kuwa ni daraja la kwanza na kuwasahau watanzania wengine.
''unajua mtu umeshiriki kuhamasisha watu ili chama fulani kishinde, lakini mwisho wa siku mambo yanayokuhusu hayatiliwi uzito, inazinguaga sana''. alisema msanii huyo.
''unajua mimi ninapoishi tegeta kule barabara mbovu sana, kila siku wanaweka udongo wanatoa wanaweka wanatoa, tunaharibu shock ups tu, ukizingatia tumeshiriki kunadi chama kuwashawishi watu wachague halafu mambo yatakuwa mazuri lakini hamna, inazingua sana kwa hiyi kama ningekuwa waziri wa miundombinu ningehakikisha barabara zinatengemaa maeneo yote''. aliongea msanii huyo
No comments:
Post a Comment