BBC
Kiungo wa Manchester City, Yaya
Toure amesema wachezaji na mashabiki wanaweza kuumia kufuatia hatua ya
Shirikisho la Soka Duniani (FIFA) kuvunja kikosi kazi kilichoundwa kwa
ajili ya kupambana na vitendo vya ubaguzi wa rangi katika soka.
Toure
mwenye umri wa miaka 33, alikuwa mmoja wa wajumbe katika kikosi kazi
hicho kilichoundwa mwaka 2013 kusaidia kutokomeza ubaguzi. Katibu mkuu wa FIFA, Fatma Samba Diouf Samoura amesema kikosi kazi hicho kilikuwa na kazi maalumu ambayo tayari wameimaliza.
Hata hivyo, hatua hiyo imekosolewa vikali na wadau mbalimbali, akiwemo Toure ambaye alifanyiwa vitendo vya kibaguzi na mashabiki wa CSKA Moscow Octoba mwaka 2013.
Nyota huyo wa zamani wa kimataifa wa Ivory Coast amesema hatua hiyo ya FIFA itaweza kuwaumiza mashabiki na wachezaji kama mipango sahihi isipowekwa.
No comments:
Post a Comment