WADHAMINI WETU

WADHAMINI WETU

Monday, January 30, 2017

RAIS DKT. MAGUFULI ALIPOHUTUBIA KATIKA KUTANGAZA JINA RASMI LA KITUO CHA AMANI NA USALAMA KILICHOPEWA JINA LA MWALIMU JULIUS NYERERE KATIKA MAKAO MAKUU YA UMOJA WA AFRICA (AU) ADDIS ABABA NCHINI ETHIOPIA

Jengo la Amani na Usalama lililopo Makao Makuu ya Umoja wa Afrika (AU) Mjini Addis Ababa nchini Ethiopia tarehe 29 Januari, 2017 limetangazwa rasmi kuwa litaitwa Mwalimu Julius Nyerere.

Jengo hilo limepewa jina hilo rasmi katika hafla ya chakula cha mchana iliyofanyika na kuhudhuriwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli pamoja na Marais mbalimbali wa Nchi Wanachama wa Umoja wa Afrika, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Mhe. Antonio Guterres, Mawaziri na Mabalozi mbalimbali wanaohudhuria Mkutano wa 28 wa Wakuu wa Nchi Wanachama wa Umoja wa Afrika unaoendelea Mjini hapa.

Akizungumza katika hafla hiyo Mhe. Rais Magufuli amewashukuru viongozi wote wa Umoja wa
Afrika kwa kuamua jengo hilo liitwe jina la Mwalimu Julius Nyerere ikiwa ni kutambua mchango wake katika kupigania Amani na Usalama na amebainisha kuwa Mwalimu Nyerere alikuwa Mwafrika halisi na kiongozi mahiri na shupavu.

“Na kwa hakika naweza kusema kuwa alikuwa mmoja wa viongozi bora kabisa ambaye amewahi kutokea katika Bara letu, katika maisha yake yote Mwalimu Nyerere alipambana ili kujenga Umoja na Mshikamano miongoni mwa Afrika, alikuwa mmoja wa waanzilishi wa umoja huu, sisi Watanzania kwa hakika tunajivunia sana Mwalimu Nyerere kuwa Baba wa Taifa” amesema Mhe. Rais Magufuli.

Mhe. Dkt. Magufuli ameongeza kuwa Mwalimu Nyerere alitoa mchango mkubwa katika kupambana na ubaguzi na unyonyaji wa kila aina, alisaidia ukombozi wa nchi nyingi za Afrika, na hata alipong’atuka katika hatamu za uongozi wa Taifa la Tanzania aliendelea kutoa mchango wake kupigania amani katika nchi za Afrika.

“Wito wangu kwenu, waheshimiwa viongozi ni kwamba, sambamba na kumuenzi Mwalimu
Nyerere kwa jengo hili, itakuwa ni jambo jema zaidi kama tutajitahidi kufuata nyayo zake pamoja na kuishi maisha ya viongozi wengine hodari wa Bara hili wakiwemo Hayati Kwame Nkhrumah, Ahmed Ben Bella, Sekou Toure, Gamal Abdel Nasser na bila kusahau shujaa wetu mwingine Hayati Nelson Mandela”

amesisitiza Rais Magufuli.

Mkutano
wa 28 wa Wakuu wa Nchi Wanachama wa Umoja wa Afrika unaendelea leo tarehe 30
Januari, 2017 hapa Addis Ababa.

Gerson Msigwa
Mkurugenziwa Mawasiliano ya Rais, IKULU

Addis Ababa
29 Januari, 2017

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.
John Pombe Magufuli akiwa na Rais wa Kenya Mhe. Uhuru Kenyatta pamoja na viongozi wa
mataifa mabalimbali wakiwa katika picha ya pamoja katika jengo jipya la kituo
cha  Amani na Usalama cha Julius Nyerere katika Makao makuu ya Umoja wa Afrika jijini Addis Ababa nchini Ethiopia. 




 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwahutubia Viongozi Wakuu wa Mataifa mbalimbali (hawapo pichani) katika Jengo jipya la Kituo cha Amani na Usalama kilichopewa jina rasmi la Mwalimu Julius Nyerere, Addis Ababa nchini Ethiopia.



 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akijadiliana jambo na Rais wa Kenya Mhe. Uhuru Kenyatta mara baada ya kutangazwa rasmi kwa Jina la Mwalimu Julius Nyerere katika kituo hicho cha Amani na Usalama.


 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akijadiliana jambo na Rais wa Rwanda Paul Kagame wakati wakielekea katika Kituo cha Amani na Usalama cha Makao Makuu ya Umoja wa Afrika kilichopewa jina la Rais wa kwanza wa Tanzania Mwalimu Julius Nyerere, Addis Ababa nchini Ethiopia. 

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akijadiliana jambo na Rais wa Rwanda Paul Kagame wakati wakielekea katika Kituo cha Amani na Usalama cha Makao Makuu ya Umoja wa Afrika kilichopewa jina la Rais wa kwanza wa Tanzania Mwalimu Julius Nyerere, Addis Ababa nchini Ethiopia. PICHA NA IKULU

AIRTEL YAKANUSHA UVUMI DHIDI YAO

Airtel Africa, a leading telecommunications company with operations in 15 countries across Africa, has refuted speculative media reports erroneously stating its possible exit from Africa. The organization has reaffirmed that it remains committed to Africa and will continue to invest in its operations to grow sustainably in Africa.

Airtel Africa’s recent 3rd quarter results were strong. The underlying Africa revenues for the quarter accelerated by 6.0 per cent Y-o-Y, the highest over the last 9 quarters. The organizations efforts to improve the quality of customer acquisitions have resulted in a reduction in customer churn to 4.9 per cent from 6.0 per cent. Data consumption and revenues have grown by 91.0 per cent & 24.0 per cent Y-o-Y respectively, led by stronger data networks. The strong focus on cost management has led to a significant underlying EBITDA margin expansion of 4.5 per cent Y-o-Y, which now stands at 24.5 per cent. Africa is now generating positive free cash and is PBT positive in constant currency.

Raghunath Mandava, Managing Director and Chief Executive Officer, Airtel Africa, said’ “All the steps taken recently with regard to human resources and infrastructure have been geared towards readying the organization to grow efficiently and sustainably in the medium to long term. The company remains committed to competing in various markets and providing more choice to customers through further investments to ensure consistent delivery of quality and value for money services to our customers. We are also accelerating our investments in new data networks and to modernize our existing networks. We are committed to launch 4 G in multiple countries.”

He added “Mergers and acquisitions continue to be the norm for any multinational organization and they affect all global organizations in equal measures as and when they happen. As a strategy, we look for opportunities to acquire or merge in opcos that are operating in a fragmented market structure with too many players in a small market. Last year, Airtel and Orange reached a mutually beneficial agreement on the assets in Sierra Leone and Burkina Faso. Similarly, Airtel also acquired assets in Uganda, CongoB and Kenya in recent times. The agreements brought together the strengths of Airtel, Warid and Essar. This has offered benefits to customers in the form of a superior and wider network, affordable voice / data services and better customer care. Away from Africa, recently, we merged with Robi in Bangladesh to create a solid and profitable No.2 player in the market.” 

The recent results demonstrate the effectiveness of Airtel’s business strategy in Africa.  The organization sees an opportunity ahead to emerge with a broader reach and sharper execution.

WAZIRI MKUU MAJALIWA AZITAKA HALMASHAURI ZIFANYE KAZI KWA WELEDI

Waziri Mkuu Kassimu Majaliwa akihutubia leo wakati wa kufungua baraza la ushauri (RCC) Mkoa wa Dodoma ambapo lilishirikisha Wizara,Idara na Wadau mbalimbali wanaoratibu ujio wa Serikali kuhamia Makao makuu Dodoma Mkutano huo umefanyika katika ukumbi wa Chuo cha mipango ya Maendeleo Vijijini Dodoma ( Picha na PMO)



WAZIRI MKUU Kassm Majaliwa amesema wakati umefika wa kuwa na watumishi wenye weledi wa kutosha kwenye Halmashauri zote nchini na pia hazitakiwi kuwa pango la wezi, wazembe au jalala la kutupa wabadhilifu walioshindikana kwingineko.


Aidha, Waziri Mkuu amesemma Serikali za Mitaa na Halmashauri zote nchini zinatakiwa zianze kujitathmini na kujipanga vizuri zaidi kuona ni kwa namna gani zitakuwa chachu ya maendeleo ya viwanda vinavyotarajiwa.

Waziri Mkuu ametoa kauli hiyo leo (Jumatatu, Januari 30, 2017) wakati akifungua Kikao cha Baraza la Mashauriano (RCC) mkoani Dodoma. Amesema kikao ni chombo muhimu na endapo kitatumika vizuri kitaweza kusaidia kusukuma maendeleo ya Mkoa na kupunguza migogoro kwenye Halmashauri.

Amesema Serikali itaendelea kuongeza kiwango cha ruzuku kwa Halmashauri zote nchini kwa kadiri uwezo utakavyoruhusu na kusisitiza kwamba fedha hizo lazima zisimamiwe vizuri na zielekezwe kwenye miradi ya maendeleo inayowagusa wananchi.

“Endapo itabainika kwamba kuna baadhi ya Sheria zinazokwamisha utendaji katika Mamlaka za Serikali za Mitaa, hatutasita kuzifanyia mapitio na hatimaye kuzibadili ili ziendane na azma yetu ya kutoa huduma bora kwa wananchi,” amesema.

Amesema Serikali ina maslahi makubwa kwa Serikali za Mitaa, sio tu kwa kuwa ni Serikali kamili katika ngazi hiyo, bali pia kutokana na ukweli kwamba kero nyingi za wananchi ziko katika ngazi hiyo.

Waziri Mkuu amesema vyanzo vingi vya mapato ya Serikali vinapatikana kwenye Halmashauri huku changamoto kubwa ikiwa ni kulegalega kwa  Halmashauri nyingi katika ukusanyaji wa mapato ya kodi na yasiyo ya kodi jambo linalozorotesha utoaji wa huduma kwa wananchi.

Hivyo Waziri Mkuu ametoa rai kwa Halmashauri hizo kuendelea kuboresha huduma kwa wananchi na kutatua kero zao kikamilifu na kwa wakati pamoja na kubuni vyanzo vipya vya mapato na kuongeza kasi ya ukusanyaji wa mapato.

Pia zihakikishe malipo yote yanafanyika kwa njia za kielektoniki na zihamasishe vijana na akina mama wajiunge kwenye vikundi vya uzalishaji mali na kuwapatia stadi za kazi na mikopo yenye masharti nafuu ili waweze kuwa chanzo cha mapato hapo baadaye.

Amesema watendaji wa Halmashauri wanatakiwa  kujiepusha na vitendo vya rushwa na ubadhilifu wa mali za umma na uzembe kazini na watakaobainika kufanya vitendo hivyo  wachukuliwe hatua kali za kisheria na kinidhamu.

“Someni taarifa ya CAG (Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa Hesabu za Serikali) na kutoa majibu ya kina ya namna mtakavyodhibiti mianya ya rushwa na ubadhilifu kama ilivyoainishwa kwenye ripoti hizo,” amesema.

Hata hivyo amesema kila Halmashauri iandae mpango wa utekelezaji wa Ilani ya CCM kwenye maeneo makubwa ya kipaumbele kama vile ujenzi wa miundombinu ya shule,  maboresho kwenye sekta ya afya (ujenzi wa hospitali, zahanati na vituo vya afya).

“Endeleeni kuwa na mahusiano mazuri miongoni mwenu, mfanye kazi kwa kuzingatia sheria, kanuni na taratibu.  Kila mmoja kwa nafasi aliyonayo atimize wajibu wake na kuzingatia mipaka ya nafasi yake. Punguzeni migogoro, matusi, dharau, bezo na vitisho. Mshirikiane na jamii ione mpo wamoja,” amesema.

RELI KATI YA DAR ES SALAAM NA RUVU YAFUNGULIWA



Uongozi wa Kampuni ya Reli Tanzania (TRL) umetoa taarifa kuwa kuanzia saa 9 alasiri leo Januari 30, 2017 njia ya reli kati ya Kituo Kikuu cha Dar es salaam na Ruvu imefunguliwa rasmi kwa shughuli za uendeshaji wa reli.

Taarifa hiyo imesema kuwa kazi ya ufunguaji njia imewezekana baada ya Wahandisi na Mafundi wa reli kuyaondoa Mabehewa yaliopata ajali l kutoka relini na pia kuikarabati sehemu iliyo haribika . Kazi hiyo imefanyika kuanzia usiku wa Januari 29, 2017 hadi mchana wa Januari 30, 2017.

Aidha treni ya abiria iliyoahirisha safari ya kuondoka kwenda bara jana imeondoka leo saa 9:05 alasiri kutoka kituo kikuu cha Dar es Salaam kwenda bara..


Wakati huo huo imefahamika kuwa msafiri mmoja aliyetambulikana kama Nd Basekena O. Bango kutoka Bujumbura Burundi akiwa anasafiri kutoka Kigoma amelazwa katika Hospitali ya Tumbi Kibaha mkoani wa Pwani kwa ajili ya matibabu zaidi. Aligunduliwa kuwa amechanika mguu wake wa kulia hivyo basi kuhitaji kushonwa mguu wake huo.


Taarifa kutoka Muhimbili zinaeleza kulazwa kwa majeruhi wawili waliopokelewa hospitalini hapo usiku wa Januari 29, 2017. Majeruhi wamefamika kuwa ni Nd. Stephania Mbona (46) kutoka Kigoma alikuwa amekuja Muhimbili kuendelea na

matibabu ya ugonjwa wa tumbo, hata hivyo alitibiwa majeraha ya kawaida na anaendelea kulazwa kwa ajili ya matibabu ya ugonjwa wake wa tumbo.



Mgonjwa wa pili Nd Alice Jovin (37) mkazi wa Salasala Dar es Salaam alikuwa anatoka Kigoma kuja Dar es Salaam amepata majeraha ya kawadia ametibiwa na alitarajiwa kuruhusiwa leo asubuhi.


Kuhusu idadi ya wasafiri treni ya Deluxe yenye uwezo wa kusafirisha abiria zaidi ya 1000 wakati inapata ajali ilikuwa na abiria 480.


Aidha imefahamika kuwa ili kufahamika hasara na sababu za ajali hiyo taarifa rasmi itatolewa baada ya uchunguzi wa Kamati maalum inayoundwa kwa mujibu wa sheria, taratibu na kanuni za uendeshaji reli za kimataifa. Taarifa hiyo itatolewa baada ya wiki mbili.



Imetolewa na Afisi ya Uhusiano:

Kwa niaba ya Mkurugenzi Mtendaji wa TRL

Ndugu Masanja Kungu Kadogosa

Januari 30, 2017

DAR ES SALAAM

Watu sita wauawa kwa kupigwa risasi msikitini.

Watu sita wameuawa na wengine wanane kujeruhiwa kwenye ufyatulianaji wa risasi katika msikiti mmoja mjini Quebec, Canada.
Ufyatulianaji wa risasi ulitokea katika Kituo cha Kitamaduni cha Kiislamu cha Quebec Jumapili usiku, polisi wamesema.
Kituo hicho kimepakia kwenye ukurasa wake wa Facebook video inayoonesha polisi wakiwa nje ya kitu hicho. Video hiyo imeambatana na ujumbe kwamba "baadhi wamefariki".
Polisi wamesema watu wawili wamekamatwa.
Mtu aliyeshuhudia ameambia shirika la habari la Reuters kwamba watu hadi watatu waliokuwa na silaha wamehusika.
Shirika hilo la habari pia limesema maafisa wa usalama waliokuwa na silaha kali wameonekana wakiingia kwenye msikiti huo.
Gazeti la Le Soleil linasema limepata taarifa kwamba mmoja wa washukiwa ni kijana wa miaka 27 mwenye "jina la asili ya Quebec", na alikuwa na bunduki aina ya AK-47.
Ufyatuaji huo wa risasi umetokea katika msikiti ulio kwenye barabara ya Sainte-Foy, moja ya misikiti miwili inayoendeshwa na kituo hicho cha utamaduni wa Kiislamu.
Shambulio lilitekelezwa wakati wa sala ya jioni.Polisi wamewakamata watu wawili
Rais wa msikiti huo Mohamed Yangui, ambaye hakuwa ndani ya msikiti wakati wa shambulio, ameambia Reuters kwamba hajafahamu kufikia sasa idadi ya waliojeruhiwa ingawa wamepelekwa hospitali mbalimbali Quebec.
"Nini kinatendeka hapa? Huu ni unyama," amesema.
Juni mwaka jana, kulipatikana karibu na mlango wa msikiti huo kichwa cha nguruwe kilichokuwa kimefungwa vizuri kama zawadi na kuandikwa "bonne appetit". Waislamu hawali nguruwe.

Waziri Mkuu wa Justin Trudeau ameandika kwenye Twitter kwa Kiingereza na Kifaransa na kusema, "Usiku huu, raia wa Canada wanaomboleza waliouawa kwenye shambulio hili la woga katika msikiti mmoja Quebec. Fikira zangu ni kwa waathiriwa na jamaa zao."

KUTANA NA Mwanamume aliyepotea njia na kuendesha baiskeli siku 30

Mwanamume huyo alisimamishwa baada ya kuendesha baiskeli kwa siku 30Mwanamume huyo alisimamishwa baada ya kuendesha baiskeli kwa siku 30

Mwanamume mmoja nchini China ambaye alikuwa na matumaini ya kuendesha baiskeli hadi nyumbani kwao kusherehekea mwaka mpya, aligundua baada ya siku 30 kuwa alikuwa amepotea njia.
Mwanamume huyo alikuwa na matumaini ya kuwasil nyumbani kwao huko Qiqihar mkoa wa Heilongjian baada ya kuanzia safari yake huk Rizhao umbali wa kilomita 1,700.
Lakini alisimamishwa na polisi wa trafiki akiwa amepotea umbali wa kilomita 500 katika mkoa wa Anhui.
Wakati waligundua, polisi walimlipia tikiti ya treni ili arudi nyumbani.
Ripoti zinasema kwa mwanamume huyo alikuwa akilala maduka ya intaneti kwa sababu hakuwa na pesa.
Mwanamume huyo hakuwa na uwezo wa kusoma ramani na hivyo alikuwa akitegemea watu kumuelekeza.
Polisi walimsimamisha kwa sababu alikuwa akitumia barabara ambayo baiskeli haziruhisiwi kuitumia.
Baada ya kugundua makosa yake, polisi na watu wote waliokuwa kituoni ambapo alisimama walichanga pesa na kumnunulia tikiti ili asafiri nyumbani.

Wanaharakati wataka ziara ya Trump Uingereza ifutwe

Maandamano ya wanawake London 21 Januari 2017Maelfu waliandamana London tarehe 21 Januari kumpinga Trump.

ofisi ya Waziri Mkuu wa Uingereza imekataa wito wa kufutiliwa mbali kwa ziara ya kikazi ya Rais wa Marekani Donald Trump nchini Uingereza kutokana na hatua yake ya kuzuia wahamiaji kuingia nchini mwake.
Taarifa zinasema Downing Street imesema hatua kama hiyo itakuwa "ya kupendeza umma tu" bila kuzingatia mambo muhimu.

Aidha, afisi hiyo imesema kwa sababu ombi la mwaliko tayari lilitumwa na likakubaliwa, kufuta ziara hiyo kunaweza "kufuta kila kitu".
Kiongozi wa chama cha Labour Jeremy Corbyn alikuwa amesema Waziri Mkuu Theresa May atakuwa anakosa kutekeleza wajibu wake kwa raia iwapo atakataa kuahirisha ziara hiyo ya Bw Trump.

Kuna ombi lililoanzishwa Jumamosi mtandaoni kutaka mkutano huo wa Trump ufutiliwe mbali.
Kufikia sasa, watu zaidi ya 900,000 wameidhinisha kuunga mkono pendekezo hilo.
Maombi ama hayo huhitaji saini 100,000 pekee kuhakikisha ombi kama hilo linajadiliwa na Bunge.
Ziara hiyo ya Bw Trump Uingereza ilitangazwa wakati wa ziara ya Bi May nchini Marekani.

Hata hivyo, hakuna tarehe maalum iliyotengwa ingawa ziara hiyo inatarajiwa kufanyika baadaye mwaka huu.
Hata hivyo, Ijumaa, Bw Trump alitia saini agizo rasmi la rais na kusitisha mpango wa Marekani wa kupokea wakimbizi kwa siku 120.
 Dallas-Fort Worth International AirportWatu wengi wamekuwa wakiandamana viwanja vya ndege vya Marekani dhidi ya marufuku hiyo ya Bw Trump.


Alipiga marufuku wakimbizi wa Syria kuingia Marekani kwa muda usiojulikana na pia akapiga marufuku watu kutoka nchi saba zenye Waislamu wengi kuingia Marekani.
Hatua hiyo imeshutumiwa vikali na viongozi mbalimbali duniani.

Afisa mmoja wa Downing Street ameambia BBC: "Marekani ni mshirika muhimu sana. Lazima tufikirie kuhusu muda mrefu ujao."
Mwanasheria mkuu wa upinzani Uingereza Shami Chakrabarti amesema msimamo wa serikali ni kama "wa kumridhisha" Bw Trump.
Bw Corbyn ametoa wito kwa wafuasi wa chama chake kuunga mkono ombi la kufutwa kwa mkutano huo.
Kiongozi wa chama cha Liberal Democrat Tim Farron pia ameunga mkono wito huo.
"Ziara yoyote ya Bw Trump nchini Uingereza inafaa kuahirishwa hadi marufuku hii iondolewe," alisema.
Meya wa London Sadiq Khan amesema ziara hiyo haifai kufanyika iwapo marufuku hiyo itaendelea kuwepo.

BREAKING NEWS: SAKATA UDA: HIVI NDIVYO MADIWANI NA WABUNGE WANAVYOTUHUMIWA KUHONGWA MAMILIONI YA SHILINGI KUFUNIKA KOMBE


  • Yabainika Fedha ziligawanywa kama njugu
  • kila Diwani alihongwa milioni 3 tu kubariki biashara
  • wabunge wote wamehongwa kasoro mdee wa kawe
  • madiwani wagombana kugombea mgao
Na. Mwandishi wetu:

wakati bado  wakazi wa jiji la  Dar es salaam wakiwa katika sintofahamu kuelekea kutimia kwa siku tano zilizotolewa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli kulitaka jiji hilo kuitisha kikao na kukubaliana kupanga matumizi ya fedha walizoingiziwa katika akaunti yao kiasi cha bilioni 5.8 zilizoingizwa na kamouni ya Simon Group wanaosemwa kununua asilimia 51 ya hisa za shirika la Usafirishaji Dar es salaam UDA, fedha ambazo halimashauri ya jiji hilo imekataa kuzitumia kwa kudai kwamba ni kidogo na kwamba kuzipokea ni kuhalalisha Ufisadi na upotevu ya mali ya wananchi wa Dae es salaam kwa kuuzwa bei ya kutupwa.

taarifa zimevuja kuwa madiwani waliokutana katika kujadili jambo hilo walikuwa tayari wamepokea rushwa ya shilingi milioni tatu kila mmoja na zawadi nyinginezo ili kupitisha jambo hilo.

''Diwani Asenga yeye alikuwa anatupigia simu na kutuambia tukakutane naye tuchukue pesa zetu za mgao, na kila mtu alikuwa akipokea kati ya shilingi milioni moja mpaka tatu''. kilisema chanzo chetu ambaye pia ni na mjumbe wa halimashauri hiyo ya jiji diwani kutokea manispaa ya temeke.
Tokeo la picha la meya wa jiji 
Meya wa Jiji la Dar es salaam Issaya Mwita. 

unajua tarehe 4 mwezi wa 12 mwaka jana tulikutana kamati ya fedha, wakala wa Kisyena aliyempa pesa kutuletea alionekana kutiliwa mashaka, hivyo tukagooma kupokea maagizo yake na kiasi chochote cha fedha kutoka kwake mpaka atakapokuja yeye mwenyewe, na huo ndio ulikuwa msimamo wetu, na tarehe nane mwezi huo huo wa 12 kisyena akaja karimjee pale, akatuhakikishia kila kitu kuwa kipo sawa na tupokee mgao wetu utakaotolewa baada ya yeye kuondoka, na alipoondoka siku mbili baadae asenga akaanza nkupigia simu wajumbe tukachukue mgao wetu huo''. kiliongeza chanzo chetu
Tokeo la picha la mabasi ya uda 
Mabasi ya Uda kabla shirika hilo halijauzwa kiutata
katika hali ya kustaajabisha chanzo chetu hicho kilihoji kama ule ni mradi halali, na biashara iliyofanyika ni halali kwanini mmiliki huyo wa UDA aamue kugawa pesa kwa wabunge na madiwani kama njugu, anaogopa nini?.

''sasa tunashangaa, kama wao wanasema kisyena hana tatizo na mradi ni halali kwanini sasa ameamua kutuhonga mamilioni yote hayo''.? alihoji.

taarifa za uhakika ambazo JAMVI LA HABARI imezipata inasema kwamba katika siku hiyo ya tarehe 8 mwezi wa 12, Kisyena alipoingia ukumbini Karimjee, aliwahakikishia wajumbe kuwa wabunge wote wajumbe wa baraza hilo la jiji ameshamalizana nao Kasoro Halima Mdee tu.

''wabunge wote tumeshamalizana kasoro Mdee peke yake'' alinukuliwa Kisyena katika kikao hicho alichoitwa kutoa uhakika.
 Tokeo la picha la mabasi ya udaMabasi mapya ya Mwendokasi yanayotokana na kuuzwa kwa UDA.
taarifa zaidi za uhakika zinasema kuwa wabunge wanaoingia katika halimashauri ya jiji ni watano kuwakilisha wilaya zao ambapo wilaya ya Temeke anaingia Mohamed Mtolea, wilaya ya ilala Mussa Zungu, Wilaya ya Kinondoni Halima Mdee, huku Ubungo ni Saed Kubenea na Kigamboni ni Dkt. Faustine Ndugulile.

taarifa za ndani ya kikao hicho cha tarehe 8 December 2016 zinasema kuwa wakati wajumbe wanauliza kuhusu wajumbe ambao wabunge kwa kisyena yeye alikuwa anajibu tayari tumeshamalizana naye...''Mtolea?? tayari kachukua 5m, Kubenea?? anajibu naye tayari kachukua 5m''. kilisema chanzo chetu.

taarifa zaidi za kiuchunguzi zinaonyesha kuwa utawanywaji huo wa fedha kwa wabunge hao na madiwani ndio kulikowafanya wabadili kisimamo yao ya awali

''wewe si unakumbuka Kubenea alivyokuwa anaqlishupalia hili jambo?, leo yuko wapi, ameufyata kimyaaa, cheza na kila kitu usicheze na fedha kaka, waswahili wamesema pesa ni sabuni ya roho''. kiliongeza chanzo chetu. 

chanzo zhetu kinasema Mgao wa mameya wa manispaa wao ulikuwa tofauti katika hizo milioni tatu tatu na tano tano za wabunge wao walikuwa na kitu kinachoitwa ''special package'

kitendo cha wabunge hao na madiwani kutuhumiwa kupokea rushwa hiyo ya mamilioni ya shilingi ili kukubali kupokea hizo bilioni 5.8 walizozikataa kwa kipindi kirefu sasa, kinatoa taswira kwamba Rais John Pombe Magufuli huenda alidanganywa na wasaidizi wake kuwa hakuna tatizo kwenye mradi huu na kwamba kwa namna Rais Magufuli alivyojitanabaisha, hakika angegundua madudu haya asingekubali kuunga mkono, taarifa za ziada zinaongeza.
Tokeo la picha la Halima mdee 
Halima Mdee mbunge pekee ambaye hakutajwa kuchukua rushwa ya shilingi milioni 5
''tumeandaa ujumbe maalum wa kwenda kumuona Rais Magufuli na kumuelezan kila kitu, tunaimani Rais wetu hawezi furahia ujinga huu, hili shirika lina thamani kubwa sana na umuhimu wake kwa jiji, halipaswi kuuzwa kwa fedha ya kununua nyanya kama hiyo, ujumbe ukimupona Rais tunaamini ataelewa na atawawajibisha wote wanaohusika na ubadhilifu huo''. aliongeza Diwani huyo ambaye kwa sasa tunamuhifadhi jina lake.

jitahada za kuwapata abunge wanaotajwa kuhongwa na madiwani zinaendelea na JAMVI LA HABARI litaendelea kuwahabarisha kwa kadri hatua zitakavyokuwa zinachukuliwa.

Wednesday, January 25, 2017

MGOGORO CUF : NANI YUPO SAHIHI?. PIGA KURA YAKO TUONE

Kwa muda kadhaa sasa kumekuwepo na sintofahamu na kurushiana maneno kwa hapa na pale baina ya pande mbili ama tatu. upande wa CUF unaoongozwa na Seif Sharrif Hamad ambaye ni Katibu Mkuu wa chama hicho,
Tokeo la picha la maalim seif
Maalim Seif Sharrif Hamad
upande mwengine ni wa Prof. Ibrahim Lipumba ambaye ni mwenyekiti wa chama hicho ambaye hapo awali alijiuzulu na katikati mwaka jana aliamua kurejea kitini kwake. na mwisho
Tokeo la picha la lipumba
Prof. Lipumba
ni upande wa serikali kupitia msajili wa vyama vya siasa ambaye yeye anasema anawatambua wote wawili kama viongozi halali wa chama hicho.

Tokeo la picha la jaji mutungi
Jaji Fransis Mutungi, Msajili wa vyama vya siasa

UPIGAJI WA KURA.
ili kupata maoni ya watanzania mbalimbali wanachama wa chama hicho na wasio wanachama, Jamvi La Habari tumeanzisha upigaji huru wa Kura utakaodumu kwa muda wa siku kumi.

namna ya kupiga Kura, ingia katika blog yetu hii ya Jamvi la habari ambayo ni www.jamvilahabari1.blogspot.com, 
kisha upande wako wa kulia juu utaona kona ya maswali inayokutaka kuchagua jibu moja tu.
kila siku tutakuwa tunatoa mrejesho wa nani yupo sahihi katika sakata hili kwa kadri ya kura zitakavyokuwa zinapigwa.

shiriki sasa kuupigia upande unaouona ni sahihi. 

MADAWA MICHEZONI: Usain Bolt kupokonywa dhahabu moja

Usain Bolt na Nesta CarterUsain Bolt na Nesta Carter.

Bingwa wa mbio za mita 100 upande wa wanaume Usain Bolt atalazimika kurudisha dhahabu moja miongoni mwa dhahabu tisa alizoshinda baada ya mwanariadha mwenza Nesta Carter kupatikana alitumia dawa za kusisimua misuli.

Carter alikuwa miongoni mwa wanariadha wanne wa Jamaica walioshinda mbio za mita 100 kupokezana vijiti katika michezo ya beijing 2008.
Ni miongoni mwa wanariadha 454 waliochukuliwa violezo vyao na kamati ya kimataifa ya Olimpiki IOC mwaka uliopita na amepatikana alitumia dawa ya aina ya methylhexaneamine.
Bolt mwenye umri wa miaka 30 alishinda dhahabu tatu katika michezo ya Olimpiki ya Rio msimu uliopita.

Alishinda dhahabu katika mbio za mita 100, 200 na 400 kupokezana vijiti na kuongeza mafanikio yake katika mbio hizo mwaka 2008 na 2012.
Carter mwenye umri wa miaka 31 alikuwa miongoni mwa wanariadha walioshinda dhahabu katika mbio hizo mjini London miaka mitano iliopita na kuisadidia Jamaica katika mbio za dunia miaka ya 2011, 2013 na 2015.

Alikuwa wa kwanza kukimbia katika mbio za rilei za 4 mara 100 mjini Beijing ambazo zilimuhusisha mwanariadha Michael Frater, Asafa Powell na Bolt.
Jamaica ilishinda kwa kuvunja rekodi ya dunia baada ya kumaliza kwa sekunde 37.10 mbele ya Trinidadad and Tobago na Japan ,ambao sasa medali zao zitaongezwa.
Brazil itajipatia medali ya shaba.

CUF WAZIDI KUZODOANA

THE CIVIC UNITED FRONT
(CUF–Chama Cha Wananchi)
TAARIFA KWA VYOMBO HABARI
Imetolewa leo Tarehe 19/1/2017
Na kurugenzi ya Habari,
Tokeo la picha la lipumba na seif
Kumekuwapo na UPOTOSHAJI mkubwa wa makusudi kuhusu Chama Cha wananchi Cuf kupatiwa RUZUKU yake na Ofisi ya Msajili.
Mwanzo Upotoshaji ulifanywa na Ndugu MTATIRO kupitia PRESS yake na wandishi wa Habari na maandiko yake mbalimbali katika mitandao ya kijamii.

Kupitia Kurugenzi yangu tulitoa ufafanuzi wa kina kuhusu swala hili na kujibu karibu hoja zote za Ndg MTATIRO.

Kwa masikitiko makubwa ameibuka Ndg Mbarala MAHARAGANDE na yeye kaja na hoja ile ile lakini katika mtindo wa kumtukana na kumdhalilisha Msajili wa vyama.
Kilicho tufanya kujibu hoja za Ndg MAHARAGANDE ni upotoshaji wa vifungu vya Katiba ya Chama Chetu.

Kwa mujibu wa Katiba ya Cuf ya Mwaka 1992 Toleo 2014 Imeeleza kila kitu kuhusu mambo ya fedha na madaraka ya viongozi. Katiba ya Cuf ipo wazi na kwa makusudi Maharagande ambae leo anajiona kua ni Msafi ameshindwa kuonyesha Ibara ya Katiba ya Cuf au kifungu kilichokiukwa na Msajili wa Vyama vya Siasa Jaji Mtungi. Katiba ya Cuf imeeleza wazi kazi za Katibu Mkuu kupitia lbara ya 93 (a) mpaka (k) lakini pia kifungu cha 2 na 3. Kazi za Katibu Mkuu ni pamoja na masuala ya usimamizi wa Fedha ambayo ipo katika kifungu (i) ibara hiyo ya 93 hakuna ubishi katika hilo, lakini ni vizuri Watanzania wakaelewa kwamba, kwa mujibu wa Katiba hii, kifungu cha 3 ibara hiyo hiyo ya 93 ambayo inaeleza Kazi za Katibu Mkuu inasema,

nanukuu
Katibu Mkuu atakapokua Nje ya Nchi au atakaposhindwa kufanya kazi zake kwa sababu yoyote ile, Naibu Katibu Mkuu anaemfuatia kwa madaraka atakua Kaimu Katibu Mkuu hadi pale Katibu Mkuu atakapokua tayari kuendelea kutekeleza Majukumu yake.

Mwisho wa kunukuu, katika hali hii ambayo Katibu Mkuu ambayo Katibu Mkuu amesusa kufika Ofisini kwa sababu anazozijua yeye, Sakaya ana kua ndie Kaimu Katibu Mkuu na anatekeleza majukumu ya Katibu Mkuu likiwemo lile la Fedha. Lakini hawa jamaa Wanaojiita Viongozi

MTOTO WA MFALME ANYONGWA

Serikali yamnyonga mwanamfalme KuwaitSerikali ya Kuwait imewanyonga wafungwa saba kwa mara ya kwanza tangu 2013Serikali ya Kuwait imewanyonga wafungwa saba kwa mara ya kwanza tangu 2013

Walinyongwa katika jela ya Central kulingana na taarifa iliotolewa na kitengo cha habari cha serikali Kuna.
Jamaa huyo kutoka familia ya kifalme alitajwa kuwa Faisal Abudallah Al Jaber Al Sabah ambaye alipatikana na hatia ya kupanga mauaji mbali na kumiliki silaha kinyume na sheria.
Wafungwa wengine walionyongwa ni pamoja na raia wa Ufilipino, Misri, Ethiopia na Bangladesh.
Walipatikana na hatia ya uhalifu ikiwemo mauaji, jaribio la mauaji ,utekaji nyara na ubakaji.

Mwanamfalme aliyekiri kuua akatwa shingo Saudia

Al Sabah alipatikana na hatia ya kumuua mwanamfalme mwengine mwaka 2010.
Mwandishi wa BBC mashariki ya kati ambaye ni muhariri wa eneo hilo Sebastian Usher alisema kuwa si jambo la kawaida kwa jamaa wa familia ya kifalme katika eneo la Ghuba kupelekwa jela ama hata kunyongwa.
''Kesi hizo huthibitisha kwamba hakuna mti asiyeweza kushtakiwa'',aliongezea.
Miongoni mwa wale walionyongwa ni Nusra al_Enezi, raia wa Kuwait ambaye alipatikana na hatia ya kuchoma moto hema wakati wa harusi ya mumewe ambaye alikuwa anaoa mke wa pili.
Moto huo uliwaua takriban watu 50.

Mtoto wa Michael Jackson asema babake aliuawa

Paris Jackson na marehemu babake Michael JacksonParis Jackson na marehemu babake Michael Jackson
Mwana wa kike wa pekee wa nyota wa muziki wa Pop marehemu Michael Jackson , Paris amesema kuwa anaamini kwamba babake aliuawa.
Katika mahojiano yake ya kwanza, Paris aliambia Rolling Stones ana hakika kwamba kifo cha babake mwaka 2009 kilipangwa.
Mwanamuziki huyo alifariki baada ya madai kwamba alikula dawa nyingi ya kupunguza maumivu.
Daktari wake Conrad Murray baadaye alipatikana na hatia ya mauaji ya kutokusudia.
Lakini mwanawe Paris anaamini kuna taarifa zaidi kuhusu habari hiyo.
Alisema kuwa mara nyengine alituambia kwamba kuna watu wanamfuata kumkamata, alisema.
Na mara nyngine alisema: 'Wataniuwa siku moja'. Alipoulizwa na Brian Hiatt iwapo anadhani babake aliuawa ,kijana huyo wa mika 18 hakusita kusema 'ndio' .
Aliendelea kusema: Watu wengi walitaka babake auawawe na kwamba alikuwa anajaribu kuwashtaki.
Kijana huyo hatahivyo hakutaja watu fulani na hakumshirikisha Conrad Murray katika tuhuma zake.

Sunday, January 22, 2017

NJAMA ZA KUMCHAFUA JAJI MUTUNGI ZAVUJA: WABUNGE KOMU NA KUBENEA WA CHADEMA WATUMIA GAZETI LAO KUFANIKISHA

  • MWANAHALISI LAPANGWA KUTUMIKA
  • LADAIWA KUOKOTEZA USHAHIDI KUMCHAFUA
  • LENGO ALEGEZE MSIMAMO SAKATA LA CUF.
 mkakati maalum umepangwa ili kumtisha, kumchafua na kumdharirisha msajili wa vyama vya siasa jaji Fransis Mutungi kupitia Gazeti la kila wiki linalomilikiwa na wabunge wa chadema Anthony Komu wa moshi vijijini na Saed Kubenea wa Ubungo la mwanahalisi taarifa za ndani za gazeti hilo zinaeleza.

mpaka sasa taarifa zinasema, msimamo wa Jaji Mutungi kuhusiana na kusimamia ipasavyo sheria ya vyama vya siasa na katiba ya CUF katika kutatua mgogoro wa kiuongozi wa ndani ya chama hicho, umewachanganya viongozi wengi wa CHADEMA na wale marafiki wao wa CUF-Maalim Seif kiasi cha kuamua kumchafua Msajili huyo kama njia ya kumtisha na kumrudisha nyuma.

taarifa za uhakika zinasema uchafuzi huo wa kitaswira unafanana na ule ambao gazeti hilo liliwahi kuwafanyia Zitto Kabwe, Edward Lowassa, Fransis Mbatia na wanasiasa wengine kwa kutekeleza kile kinachoitwa (Character Assasination)
WAKATI taarifa za kuvuja huko kwa mbinu mpya za kumkabili na  kupambana na Msajili wa vyama vya siasa nchini Jaji Fransis Mutungi zinazohusisha matusi, kejeli, na kumuhusisha msajili na ofisi yake na tuhuma za kila aina ili pengine abadili msimamo, mbinu zinazopangwa na wanaojiita kamati ya Uongozi ya chama cha CUF ambayo Ofisi ya Msajili haiitambui kamati hiyo na kusisitiza kumtambua Lipumba kama mwenyekiti na Maalim Seif kama Katibu mkuu.
Tokeo la picha la KUBENEA
Mmiliki wa Gazeti la Mwanahalisi ambaye pia ni Mbunge wa ubungo Chadema, Saed Kubenea
Taarifa za uhakika ambazo gazeti hili, imezipata ni kwamba tayari mbinu hizo zimeanza kutekelezwa na viongozi wa kamati hiyo kwa kuanzia na kusambaza habari zinazomdhalilisha msajili wa vyama katika vyombo mbalimbali vya habari na mitandao ya kijamii nchini.

Moja kati ya mkakati huo ni ile iliyosambazwa juzi na Mbarala Maharagande taarifa iliyojaa kejeli, matusi, tuhuma na dhihaka kwa msajili wa vyama vya siasa na kuacha kujibu hoja za msingi ambazo awali zilitolewa na ofisi ya msajili.

Akizungumzia taarifa hizo, Jaji Mutungi alisema kwamba yeye haogopi kuchafuliwa kwa aina yoyote kwa kuzingatia ukweli kwamba yeye ni mtumishi wa umma na anafanya kazi zake kuutumikia umma kwa mujibu wa sheria za nchi na kamwe hawezi kuyumbishwa na matusi wala kejeli zozote zinazotolewa dhidi yake na ofisi yake.

"Namimi nimezipata hizo taarifa kwamba kuna baadhi ya watu wamepanga kupambana nami kwa kunichafua, japo naendelea kuzifanyia kazi lakini kwa kifupi kabisa niwaambie waache wanichafue na wala siogopi lolote". alisema.
Tokeo la picha la anthony komuMmiliki mwenza wa Mwanahalisi ambaye pia ni Mbunge wa Moshi vijijini CHADEMA. Anthoyn Komu

"Mimi ni mtumishi wa umma na ninafanya kazi kwa mujibu wa sheria hivyo siwezi kuyumbishwa na mambo ya kitoto hayo ya kuchafuana na kurushiana tuhuma zisizo na kichwa wala miguu. Sidhani kama kumshambulia Mutungi kunaweza kuleta tija ya wao kufikia malengo yao". alisema.

Aidha, alisema mjadala wa ruzuku ya CUF aliyotoa kwa Chama hicho ameshaufunga na anashangazwa na maneno ya hayo uongo yanayozidi kusambazwa na watu wanaojiita viongozi wa CUF.

Jaji Mutungi  alisema yeye ni muumini haki na sheria, na ndio maana mamlaka za uteuzi zilimuamini na kumpa nafasi ya Ujaji.

"Natambua uadilifu wangu na sitaki niuelezee, ila nahisi tukiendelea kulizungumzia hili tutakuwa tunalikuza bila sababu za msingi. Nasisitiza tena kuwa ofisi yangu inamtambua Profesa Lipumba kama Mwenyekiti wa CUF na Maalim Seif Sharif Hamad kama Katibu Mkuu,''alisema.

Kutokana na hali hiyo, alisema kinachoendelea kufanywa na kundi la watu wanaojiita viongozi wa CUF kuzungumza mambo mengi ya uongo na kumuhusisha yeye  bila ukweli huku wakishindwa kuisoma vyema Katiba yao wenyewe inayowaongoza.

"Nasisitiza tena si Mutungi au Ofisi ya Msajili iliyoandika Katiba ya CUF, ni wao wenyewe wameiandika. Ofisi ilichofanya ni kuitafsiri katiba yao wenyewe na kutoa muongozo. Sasa tatizo liko wapi?''alisema.

Taarifa za ndani ya mkakati huo zinasema pamoja na mitandao ya kijamii,  yamepangwa pia kutumika magazeti kadhaa likiwemo gazeti moja maarufu la kila wiki linalotoka siku ya jumatatu linalomilikiwa na abunge wawili wa Chama kimoja cha upinzani hapa nchini.

Hivi karibuni, mtu anayejiita Kaimu Naibu Mkurugenzi wa Habari na Mawasiliano, Mbarala Maharagande alizungumza na waandishi wa habari huku akidai kuwa ofisi ya Msajili inasababisha mpasuko ndani ya chama hicho na ndio maana imetoan ruzuku kwa Lipumba.

JAMVI LA HABARI lilibua namna SHILINGI milioni 369 zilizodaiwa kutoroshwa kutoka hazina na kwenda katika
akaunti ya Chama cha CUF wilaya ya Temeke, Januari  5 na baadae kugawanywa  kwa
watu mbalimbali, zinaelezwa ziliingizwa kihalali kwa kufuata sheria na
taratibu zote za kiofisi kama ilivyoelekezwa na Ofisi ya Msajili wa Vyama
vya Siasa, Jamvi la Habari linaweza kuthibitisha.

Hivi karibuni, Mwenyekiti wa Kamati ya uongozi ya chama cha wananchi CUF
ambaye ofisi ya  msajili wa vyama vya siasa haimtambui, Julius Mtatiro
alikaririwa na vyombo kadhaa vya habari akilalamikia juu ya alichokiita
kuchotwa kwa fedha za ruzuku za chama hicho kitendo alichokiita kupewa
baraka na msajili wa vyama vya siasa Jaji Francis Mutungi.

Taarifa za uhakika ambazo gazeti hili limezipata, zinaonyesha kuwa hakukuwa
na tatizo lolote la kisheria, kimaadili wala kikanuni katika utoaji wa
fedha hizo ambazo ni sehemu ya fedha za ruzuku ambazo CUF wanastahili
kupata kutoka serikali kuu kwa shughuli za uendeshaji wa chama hicho.
Tokeo la picha la mutungi
Msajili wa Vyama vya siasa Jaji Fransis Mutungi.

Taarifa hizo zinasema zaidi kuwa sio kweli fedha hizo ziliingizwa katika
akaunti ya wilaya ya Temeke isipokuwa kwa sasa, Temeke ni jina tu la
akaunti hiyo kama ambavyo akaunti nyingine zinaitwa Holland, Vijana,
Kijitonyama na kadharika, na kwamba akaunti hiyo ni halali na imehuishwa
kwa kubadilishwa matumizi yake kutoka kuwa akaunti ya wilaya mpaka kuwa
akaunti maalum ya taifa kwa kufuata vikao halali vya mashauriano ya chama
hicho.

Kwa mujibu wa mtoa taarifa wetu aliye ndani ya serikali, anasema ofisi ya
msajili wa vyama vya siasa ilipata uthibitisho pasi na shaka kwamba  akaunti
hiyo ni halali kwa kukipatia chama hicho ruzuku yao kama walivyoomba
viongozi waandamizi wanaofahamika na kutambulika na msajili wa vyama.

‘’Unajua msajili hajajiingizia tu zile fedha, CUF wenyewe walileta maombi
kuwa fedha zao kwa sasa ziingizwe katika akaunti namba fulani inayopatikana
sehemu fulani, ndipo msajili alipofuatilia na kuwataka watimize masharti
yote ya kikatiba ikiwemo kufuata vikao halali vya chama chao na kuwaingizia
fedha hizo baada ya kuombwa muda mrefu kufanya hivyo’’. Kilisema chanzo
chetu

‘’Ukweli ni kwamba Msajili anaifahamu CUF moja tu,  msajili yeye haifahamu
kamati inayoongozwa na Mtatiro na wenzake, anachofahamu msajili wa vyama
vya siasa kuwa kuna CUF, ambacho Mwenyekiti wake ni Profesa Ibrahim
Lipumba, Katibu Mkuu wake, Maalim Seif Sharrif Hamad, na manaibu wake
Magdalena Sakaya na Nassoro Mazrui kila mmoja’’ kiliongeza chanzo chetu.

Taarifa za uhakika ambazo gazeti hili linazo zinaonyesha kuwa  kitendo cha
Profesa Lipumba kumtambua na kuwa tayari kufanya kazi na Katibu Mkuu wa CUF, Maalim Seif kimempa moyo msajili kuwa akuwapatia ruzuku kina Lipumba kutapelekea kazi za chama kizima kufanyika kwa kuwa mara kadhaa amekuwa akikaririwa na vyombo vya habari akimuita ofisini katibu mkuu wake
kumpangia kazi za kufanya.

Tofauti na Katibu mkuu wa CUF, Maalim Seif, ambaye ameendelea kusisitiza
kutomtambua Mwenyekiti wake Lipumba, bila kujali ukweli kwamba mamlaka
iliyomchagua haikuwahi kurudhia kujiudhulu kwake.

"katika akili tu ya kawaida, mwenyekiti wa chama ndio kiongozi mkuu wa
shughuli za kichama katika CUF, yeye anathibitisha anamtambua Katibu Mkuu
wake na yupo tayari kushirikiana naye kufanya kazi, Katibu Mkuu yeye hataki
kumtambua na anaendelea kuing’ang’ania Kamati ya Uongozi ambayo kisheria
haitambuliki, unafikiri ili chama kiendelee kupewa ruzuku na kijiendeshe,
nani angepewa ruzuku kama si Lipumba’’.  Alisema Chumi Kisyabo aliyeombwa na gazeti hili kutoa maoni yake.

‘’Kwa maoni yangu, kumpa ruzuku Lipumba ni kukifanya chama chao kiende
mbele kwa kuwa Lipumba ndio kiongozi mkuu wa chama na anawatambua wasaidizi wake wote halali akiwemo Maalim Seif, na kumpa ruzuku Maalim Seif ni kukidumaza chama na kuchochea  mgogoro kutokana na msimamo wa wake wa kutomtambua, kwa hili namuona msajili wa vyama kama mtu aliyetumia akili nyingi sana kuutatua mgogoro huu’’. Alisema.

Sakata la ruzuku la chama hicho kimeendelea kuchukua nafasi katika vichwa
vya habari mbalimbali ambapo jumapili ya Januari 15, 2017 anayejiita
Mwenyekiti wa kamati ya uongozi wa chama hicho, Mtatiro alishiriki kwa njia
ya simu mjadala kuhusu jambo hilo na Mkurugenzi wa Habari na Mawasiliano
kwa Umma, Abdul  aliyekuwepo studio katika kituo cha Star Tv jijini Mwanza
na wawili hao kushindana kwa hoja, katiba na uzoefu wao ndani ya chama
hicho huku kambaya akimtuhumu mtatiro kuwa ni mpiga madili mzoefu.

‘’Namshangaa Julius(Mtatiro) leo analalamika sisi kuingiza  fedha hizi
kwenye akaunti ya diwani wetu na anasema ni wizi, wakati yeye mwaka 2011
aliingiziwa milioni mia moja na nane (108) katika akaunti yake binafsi ,
sasa leo analalamika nini nay eye mwenyewe aliwahi kumuingizia diwani huyo
huyo milioni 46’’?. Alisema Kambaya.

Katika majibu yake,  Mtatiro alikiri kuingiziwa na kusema ziliingizwa
kwababu ya kampeni za uchaguzi mdogo igunga, japo akaunti ya wilaya hiyo ya
igunga ilkikuwepo.

Katika hatua nyingine kiongozi mwandamizi wa chama hicho na mbunge maarufu mstaafu  wa Mkanyageni, Habib Mnyaa alipiga simu studio hizo na kusema yeye kama mwanachama na kiongozi mwandamizi wa chama hicho haoni shida kwa wao kuingiziwa fedha kwenye akaunti hiyo kwa kuwa ni akaunti halali ya chama na kwamba kuziingiza kwenye akaunti binafsi ya mtu ni jambo la chama ambalo halihusiani na msajili wa vyama.

"Msajili hajaingiza fedha kwenye akaunti ya mtu binafsi, msajili ameingiza
fedha kwenye akaunti ya chama, na kwa hivyo hakuna tatizo lolote kisheria,
chama kimetumiaje hizo fedha ndio swala linaloweza kuibua mjadala, na hata
hivyo mamlaka ya ubadhilifu sio ya mtatiro ni mamlaka ya CAG, hivyo hatuna
haja ya kuwa na papara, tusubiri tuone matokeo ya msajili, kwenye hili
Msajili hana makosa na ninampongeza sana kwa kweli’’. Alisikika Mnyaa.

KASHFA YA RUZUKU YA CUF : Siri zaidi zavuja

Yabainika milioni 369 ziliingizwa katika akaunti halaliTokeo la picha la mutungiJaji Fransis Mutungi, Msajili wa Vyama vya siasa nchini Tanzania
  • L CUF Zanzibar watofautiana
  • L Habib Mnyaa apongeza uamuzi wa msajili
Na Meshack Katunzi.- JAMVI LA HABARI

SHILINGI milioni 369 zilizodaiwa kutoroshwa kutoka hazina na kwenda katika akaunti ya Chama cha CUF wilaya ya Temeke, Januari  5 na baadae kugawanywa  kwa watu mbalimbali, zinaelezwa ziliingizwa kihalali kwa kufuata sheria na taratibu zote za kiofisi kama ilivyoelekezwa na Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa, Jamvi la Habari linaweza kuthibitisha.

Hivi karibuni, Mwenyekiti wa Kamati ya uongozi ya chama cha wananchi CUF ambaye ofisi ya  msajili wa vyama vya siasa haimtambui, Julius Mtatiro alikaririwa na vyombo kadhaa vya habari akilalamikia juu ya alichokiita kuchotwa kwa fedha za ruzuku za chama hicho kitendo alichokiita kupewa baraka na msajili wa vyama vya siasa Jaji Francis Mutungi.

Taarifa za uhakika ambazo gazeti hili limezipata, zinaonyesha kuwa hakukuwa na tatizo lolote la kisheria, kimaadili wala kikanuni katika utoaji wa fedha hizo ambazo ni sehemu ya fedha za ruzuku ambazo CUF wanastahili kupata kutoka serikali kuu kwa shughuli za uendeshaji wa chama hicho.

Taarifa hizo zinasema zaidi kuwa sio kweli fedha hizo ziliingizwa katika akaunti ya wilaya ya Temeke isipokuwa kwa sasa, Temeke ni jina tu la akaunti hiyo kama ambavyo akaunti nyingine zinaitwa Holland, Vijana, Kijitonyama na kadharika, na kwamba akaunti hiyo ni halali na imehuishwa kwa kubadilishwa matumizi yake kutoka kuwa akaunti ya wilaya mpaka kuwa akaunti maalum ya taifa kwa kufuata vikao halali vya mashauriano ya chama hicho.

Kwa mujibu wa mtoa taarifa wetu aliye ndani ya serikali, anasema ofisi ya msajili wa vyama vya siasa ilipata uthibitisho pasi na shaka kwamba  akaunti hiyo ni halali kwa kukipatia chama hicho ruzuku yao kama walivyoomba viongozi waandamizi wanaofahamika na kutambulika na msajili wa vyama.

‘’Unajua msajili hajajiingizia tu zile fedha, CUF wenyewe walileta maombi kuwa fedha zao kwa sasa ziingizwe katika akaunti namba fulani inayopatikana sehemu fulani, ndipo msajili alipofuatilia na kuwataka watimize masharti yote ya kikatiba ikiwemo kufuata vikao halali vya chama chao na kuwaingizia fedha hizo baada ya kuombwa muda mrefu kufanya hivyo’’. Kilisema chanzo chetu

‘’Ukweli ni kwamba Msajili anaifahamu CUF moja tu,  msajili yeye haifahamu kamati inayoongozwa na Mtatiro na wenzake, anachofahamu msajili wa vyama vya siasa kuwa kuna CUF, ambacho Mwenyekiti wake ni Profesa Ibrahim Lipumba, Katibu Mkuu wake, Maalim Seif Sharrif Hamad, na manaibu wake Magdalena Sakaya na Nassoro Mazrui kila mmoja’’ kiliongeza chanzo chetu.
 Tokeo la picha la julius mtatiro 
Julius Mtatiro
Taarifa za uhakika ambazo gazeti hili linazo zinaonyesha kuwa  kitendo cha Profesa Lipumba kumtambua na kuwa tayari kufanya kazi na Katibu Mkuu wa CUF,  Maalim Seif kimempa moyo msajili kuwa akuwapatia ruzuku kina Lipumba kutapelekea kazi za chama kizima kufanyika kwa kuwa mara kadhaa Lipumba amekaririwa na vyombo vya habari akimuita ofisini katibu mkuu wake kumpangia kazi za kufanya.

Tofauti na Katibu mkuu wa CUF Maalim Seif  ambaye ameendelea kusisitiza kutomtambua Mwenyekiti wake Lipumba bila kujali ukweli kwamba mamlaka iliyomchagua haikuwahi kurudhia kujiudhulu kwake.
‘’katika akili tu ya kawaida, mwenyekiti wa chama ndio kiongozi mkuu wa shughuli za kichama katika CUF, yeye anathibitisha anamtambua Katibu Mkuu wake na yupo tayari kushirikiana naye kufanya kazi, Katibu Mkuu yeye hataki kumtambua na anaendelea kuing’ang’ania Kamati ya Uongozi ambayo kisheria haitambuliki, unafikiri ili chama kiendelee kupewa ruzuku na kijiendeshe, nani angepewa ruzuku kama si Lipumba’’.  Alisema Chumi Kisyabo aliyeombwa na gazeti hili kutoa maoni yake.

‘’Kwa maoni yangu, kumpa ruzuku Lipumba ni kukifanya chama chao kiende mbele kwa kuwa Lipumba ndio kiongozi mkuu wa chama na anawatambua wasaidizi wake wote halali akiwemo Maalim Seif, na kumpa ruzuku Maalim Seif ni kukidumaza chama na kuchochea  mgogoro kutokana na msimamo wa wake wa kutomtambua, kwa hili namuona msajili wa vyama kama mtu aliyetumia akili nyingi sana kuutatua mgogoro huu’’. Alisema.
 Tokeo la picha la maalim seif 
Maalim Seif Sharrif Hamad

Sakata la ruzuku la chama hicho kimeendelea kuchukua nafasi katika vichwa vya habari mbalimbali ambapo jumapili ya Januari 15, 2017 anayejiita Mwenyekiti wa kamati ya uongozi wa chama hicho, Mtatiro alishiriki kwa njia ya simu mjadala kuhusu jambo hilo na Mkurugenzi wa Habari na Mawasiliano kwa Umma, Abdul  aliyekuwepo studio katika kituo cha Star Tv jijini Mwanza na wawili hao kushindana kwa hoja, katiba na uzoefu wao ndani ya chama hicho huku kambaya akimtuhumu mtatiro kuwa ni mpiga madili mzoefu.
‘’Namshangaa Julius(Mtatiro) leo analalamika sisi kuingiza  fedha hizi kwenye akaunti ya diwani wetu na anasema ni wizi, wakati yeye mwaka 2011 aliingiziwa milioni mia moja na nane (108) katika akaunti yake binafsi , sasa leo analalamika nini nay eye mwenyewe aliwahi kumuingizia diwani huyo huyo milioni 46’’?. Alisema Kambaya.

Katika majibu yake,  Mtatiro alikiri kuingiziwa na kusema ziliingizwa kwababu ya kampeni za uchaguzi mdogo igunga, japo akaunti ya wilaya hiyo ya igunga ilkikuwepo.
Katika hatua nyingine kiongozi mwandamizi wa chama hicho na mbunge maarufu mstaafu  wa Mkanyageni, Habib Mnyaa alipiga simu studio hizo na kusema yeye kama mwanachama na kiongozi mwandamizi wa chama hicho haoni shida kwa wao kuingiziwa fedha kwenye akaunti hiyo kwa kuwa ni akaunti halali ya chama na kwamba kuziingiza kwenye akaunti binafsi ya mtu ni jambo la chama ambalo halihusiani na msajili wa vyama.

‘’msajili hajaingiza fedha kwenye akaunti ya mtu binafsi, msajili ameingiza fedha kwenye akaunti ya chama, na kwa hivyo hakuna tatizo lolote kisheria, chama kimetumiaje hizo fedha ndio swala linaloweza kuibua mjadala, na hata hivyo mamlaka ya ubadhilifu sio ya mtatiro ni mamlaka ya CAG, hivyo hatuna haja ya kuwa na papara, tusubiri tuone matokeo ya msajili, kwenye hili Msajili hana makosa na ninampongeza sana kwa kweli’’. Alisikika Mnyaa.

Monday, January 16, 2017

Korea Kusini: Mwendesha mashtaka ataka mkuu wa Samsung akamatwe

Lee Jae-yongLee Jae-yong amekuwa akisimamia Samsung tangu babake alipougua mwaka 2014
Mwendesha mashtaka maalum nchini Korea Kusini anaitaka mahakama itoe kibali cha kukamatwa kwa mkuu wa kampuni ya Samsung kutokana na mchango wake katika kashfa ya ufisadi nchini humo.

Msemaji wa afisi ya mwendesha mashtaka Lee Kyu-chul amesema Lee Jae-yong alilipa zaidi ya dola 35 milioni za Marekani kwa nyakfu zinazoungwa mkono na Choi Soon-sil, rafiki wa Rais Park Geun-hye.
Mwendesha mashtaka huyo anasema pesa hizo zilikusudiwa kuhakikishia uungwaji mkono wa mpango wa kuunganisha kampuni mbili zilizohusishwa na Samsung.

Bw Lee amekanusha tuhuma hizo. Samsung haijatoa taarifa yoyote kufikia sasa.
Bw Lee, anayefahamika kama Jay Y Lee, alihojiwa kwa zaidi ya 20 na maafisa wa mashtaka mjini Seoul wiki iliyopita.
Kwa sasa ni naibu mwenyekiti wa Samsung Electronics, lakini tangu babake, Lee Kun-hee, alipopata mshtuko wa moyo mwaka 2014, amekuwa akitazamwa kama mkuu wa kampuni hiyo.
Kashfa hiyo inatishia kumtoa madarakani Bi Park ambaye kwa sasa amesimamishwa kazi mwa muda Mahakama ya Juu inapoendelea kuchunguza tuhuma dhidi yake na mswada wa kumuondoa madarakani.
BBC

Mabilionea wanane wanamiliki mali sawa na nusu ya watu duniani





Graphic showing eight richest men
Meli kubwaMeli kubwa za kifahari ni baadhi ya vitu vinavyomilikiwa na watu matajiri zaidi
Utafiti uliofanywa na shirika la Oxfam la Uingereza unaonesha mabilionea wanane wanamiliki mali sawa na mali ya watu 3.6 bilioni kwa pamoja.
Takwimu za shirika hilo, ambazo zimepingwa na baadhi ya wakosoaji, zinatokana na maelezo na habari za kina zilizokusanywa na shirika hilo, na zinaonesha pengo kati ya matajiri na maskini ni kubwa "kuliko ilivyodhaniwa awali".
Ripoti hiyo ya Oxfam imetolewa wakati mkutano mkubwa kuhusu uchumi wa dunia unaanza mjini Davos.
Mark Littlewood, wa Taasisi ya Masuala ya Uchumi, amesema Oxfam badala yake wanafaa kuangazia njia ya kusisimua ukuaji.
"Kama shirika linalopiga vita umaskini, Oxfam wanaonekana sana kuangazia zaidi matajiri," mkurugenzi mkuu huyo wa shirika hilo la ushauri amesema.
Kwa wale ambao wana malengo ya "kuangamiza kabisa umaskini uliokithiri", sana wanafaa kuangazia hatua za kusisimua ukuaji wa uchumi, ameongeza.
Ben Southwood, ambaye ni mkuu wa utafiri katika Taasisi ya Adam Smith, amesema la muhimu zaidi si kiasi cha mali inayomilikiwa na watu matajiri zaidi duniani, bali ni hali ya maisha ya watu maskini zaidi duniani, ambayo inaimarika mwaka baada ya mwaka.
"Kila mwaka, tunapotoshwa na takwimu za Oxfam. Takwimu ziko sawa - zinatoka kwa Credit Suisse - lakini ufasiri wa takwimu hizo si sahihi."

'Mkutano wa Davos'
Mkutano unaofanyika mjini Davis, Uswizi huwavutia viongozi wengi wa kisias ana kibiashara duniani.
Katy Wright, mkuu wa mambo ya nje wa Oxfam, anasema ripoti hiyo imesaidia shirika hilo kuwauliza maswali viongozi wa kisiasa na kiuchumi.
"Tuna uhakika kwamba Davos ni mkutano tu mwingine wa kupiga gumzo miongoni mwa viongozi na watu wenye ushawishi duniani, lakini tunahitaji kujaribu na kupata mwelekeo," aliongeza.

Mabilionea wanane matajiri zaidi duniani

1. Bill Gates (US): mwanzilishi wa Microsoft (utajiri wake $75bn)
2. Amancio Ortega (Spain): mwanzilishi wa Zara na mmiliki wa Inditex (utajiri wake $67bn)
3. Warren Buffett (US): mwenyehisa mkubwa Berkshire Hathaway (utajiri wake $60.8bn)
4. Carlos Slim Helu (Mexico): mmiliki wa Grupo Carso (utajiri wake $50bn)
5. Jeff Bezos (US): mwanzilishi na afisa mkuu mtendaji wa Amazon (utajiri wake $45.2bn)
6. Mark Zuckerberg (US): mwanzilishi mwenza na afisa mkuu mtendaji wa Facebook (utajiri wake $44.6bn)
7. Larry Ellison (US): mwanzilishi mwenza na afisa mkuu mtendaji wa Oracle (utajiri wake $43.6bn)
8. Michael Bloomberg (US): mmiliki wa Bloomberg LP (utajiri wake $40bn)
Chanzo: Orodha ya mabilionea ya Forbes, Machi 2016

Mchumi wa Uingereza Gerard Lyons anasema kuangazia watu matajiri kupindukia hakutoi "taswira kamili" na kwamba badala yake watu wanafaa kuangazia "kuifanya keki ya uchumi kuwa kubwa vya kutosha".
Hata hivyo, amesema Oxfam imefanya uamuzi wa busara kufichua kampuni ambazo inaamini zinaendeleza ukosefu wa usawa na kuwa na mfumo wa biashara ambao unaangazia zaidi kutajirisha wamiliki na maafisa wakuu watendaji.
Bi Wright wa Oxfam amesema ukosefu wa usawa kwenye uchumi unachangia kuwepo kwa siasa za misimamo mikali.
  • Chris Gardner: Mtu asiyekuwa na makao aliyefanikiwa na kuwa tajiri
Alitoa mfano wa kuchaguliwa kwa Donald Trump nchini Marekani na Uingereza kupiga kura kujitoa kutoka kwa Umoja wa Ulaya.
Oxfam imekuwa ikitoa ripoti zinazokaribiana kwa miaka minne iliyopita.
Mwaka 2016 ilifichua kwamba watu 62 duniani walikuwa na utajiri sawa na wa nusu ya watu maskini zaidi duniani.
Idadi hiyo sasa imeshuka na kufikia watu wanane pekee kwa sasa takwimu sahihi zaidi zinapatikana, Oxfam wamesema.
Lakini bado hali ni ile ile, kwamba asilimia moja ya watu duniani wanamiliki utajiri sawa na watu hao wengine wote duniani kwa pamoja.
Baadhi ya watu wanane matajiri zaidi duniani hata hivyo wamekuwa wakitoa mabilioni ya dola kama hisani.
Mwaka 2000 Bill Gates na mkewe Melinda walianzisha wakfu ambao wameupatia zaidi ya $44bn.
Mwaka 2015 Mark Zuckerberg na mkewe Priscilla Chan waliahidi kutoa 99% ya utajiri wao, ambao ulikuwa sawa na $45bn kwa makadirio ya thamani ya hisa za Facebook wakati huo.

JAMII INAPASWA KUSHIRIKIANA NA SERIKALI KUANDAA MAZINGIRA MAZURI KWA WATOTO WA MITAANI.



Na, SABRINA MNZAVA

 https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEgfecdgSWAKOmc_uufduqKhZ7eReiKlMjqhIKDjiomPO8rOTUdzwey4GHyU_EAfV6cOKxeDBo9BetPn2WNYdXicPnRmohVYdVOB4LytrFZcnIFOR8FrWotlsVFOUyMq4CXbEf39X84VKMgJ/s1600/4.jpg
Watoto wa mitaani kwa sasa tatizo linalokua kwa kasi kubwa hasa maeneo mengi ya mjini. Kwa mujibu wa takwimu zilizotolewa na wizara ya afya na ustawi wa jamii kupitia idara ya Ustawi wa jamii zinaonyesha kuwa kwa jiji la Dar es salaam pekee lina zaidi ya watoto wa mitaani zaidi ya 5600. Hizi zikiwa ni takwimu za mwaka 2012 (Rapid Assessment 2012).

Kwa idadi hiyo inaonyesha jinsi tatizo hili linavyokuwa kwa kasi kubwa, lakini pamoja na kuwepo kwa vituo mbalimbali vya kulelea watoto hawa ikiwemo Dogodogo Center, Kihowede, Child in the Sun na vingenevyo vingi . Lakini bado tatizo la watoto hawa wadogo kuzurura mitaani huku wakiishi kwa kuomba omba, kuosha magari, na kulala mitaroni yakiwa maisha yao ya kila siku.

Kwa upande wa jiji la Dar es salaam watoto hawa wamekuwa wakipatikana kwa wingi katika maeneo ya mwenge, morocco, posta, ubungo, maeneo karibu na daraja la Sarender na maeneo mengine. Itakumbukwa kuwa mkuu wa mkoa wa Dar es salaam kwa wakati wa nyuma alipiga marufuku ombaomba wote kutoonekana barabarani katika mkoa wake lakini halikutekelezeka hata kidogo.

Sababu kubwa za kuongezeka kwa watoto hawa ambao kimsingi walistahili wawe shuleni wakipata elimu zimekuwa zikiongezeka kila kukicha. Lakini kwa mujibu wa utafiti uliofanywa na taasisi ya Child in the Sun ikisaidiana na kituo cha Dogodogo Center zimeonyesha sababu kadhaa zikiwemo za uwepo wa stendi kuu ya mabasi yaendayo mikoani na nje ya nchi ya ubungo, kuvunjika mfumo wa malezi katika familia. Nyingine ni vifo vya wazazi au walezi, ongezeko la watu wanaohamia Dar es salaam kutoka mikoani na maeneo mengine ya vijijini kuja kutafuta ajira na nyingine watoto kufuata misukumo ya watoto wenzao au ushauri mbaya wa watu waonaamua kuwatumikisha kwa faida zao.

Mbali na kuwepo kwa watoto hawa mara nyingi kumekuwa kukiripotiwa kwa matukio mengi ya kiuharifu yakiwahusisha watoto hawa. Mfano mzuri ni lile kundi linalosumbua jiji la Dar es salaam likijulikana kama Panya Road. Ambalo limekuwa likitumia silaha za jadi kufanya uharifu na unyang’anyi wa mali za watu. Na muda mwingine kukata watu mapanga na kuwasababishia maumivu na majeraha makubwa.

Mbali na matukio wanayoyatenda muda mwingi watoto hawa wamekuwa wakitendewa matendo maovu ikiwemo kubakwa, kulawitiwa na wengine kutendewa kinyume na maumbile pamoja na kupigwa na kutumikishwa huku kwa malipo kiduchu au kusaidiwa eneo la kulala au chakula. Matatizo haya ndiyo yamenifanya niandike makala hii ili kama jamii ione kuna haja kubwa ya kuwaokoa watoto hawa waishio mazingira hatarishi.

Nafahamu fika kuwa serikali imefanya jitihada mbalimbali kuwasaidia watoto hawa ikisaidiana na mashirika mabalimbali likiwemo lile la UNESCO, IMF, IOM, AMREF, Family Health International na mengineyo mengi. Lakini bado tatito liko palepale na wengine upelekwa kwenye vituo vya kulelea watoto waishio kwenye mazingira magumu lakini wengi wao hutoroka huku sababu kubwa wanayodai ni manyanyaso wayapatayo huko kwenye vituo hivyo.

Pia miradi mbalimbali imefanyika ikiwemo ile ya Rapid Assesment na mradi wa pamoja tuwalee, ili kusaidia kupunguza watoto waishio mitaani na walio katika mazingira hatarini lakini bado tatizo lipo. Kama jamii tunapaswa kujiuliza tumekosea wapi ili tuweze kujinusuru katika janga ili.

Watoto hawa walipaswa kuwa shuleni wakipata elimu itakayowasaidia kuwakomboa kimaisha na hapo mbeleni baadhi yao wangeweza kuwa hata viongozi wa taifa ili na kuwa tegemeo kubwa kwa taifa.Lakini cha kusitisha jamii imekaa kimya na kuliona hili si tatizo kubwa la kuifanya jamii ishituke.

Baadhi ya watoto hawa wameanza kujiingiza katika matendo ambayo hayafai katika jamii ikiwemo utumiaji wa madawa ya kulevya huku wangali wadogo. Tujiulize kama jamii leo hii mtoto mdogo wa miaka kati ya 10 na 15 anatumia madawa ya kulevya tunatengeneza taifa gani?, Tunajenga taifa la watu wa aina gani?.

Na hapo hapo utawasikia watu wakisema watoto wa siku hizi wameharibika na kusahau kuwa tuna jukuma la kuilinda, kuielimisha jamii na kutunza maadili ya jamii ili tuweze kuwa na taifa lililo imara na bora kwa hapo mbeleni.  Nakumbuka kauli moja aliyowahi kuitoa mama Salma Kikwete kuwa mtoto wa mwenzio ni wako hivyo kama jamii inapaswa kujiweka tayari kusaidiana na serikali kuwasaidia watoto hawa watoke mitaani na kwenda kupata elimu shuleni itakayao wasaidia kujikomboa kimaisha na kujipatia maarifa.

Hivyo basi ni jukumu la jamii kushirikiana kwa pamoja ili kuweza kuunganisha nguvu ili kuikomboa jamii katika janga hili ambalo linakuwa kwa kasi kubwa. Pia ni wakati wa taasisi na Asasi za kiraia kushirikiana na jamii ili kuwasaidia watoto hawa ili tuweze kujenga jamii isiyo na watoto wa mitaani.

0718156595.