WADHAMINI WETU

WADHAMINI WETU

Wednesday, November 30, 2016

MWIJAGE AIPONGEZA TRA KWA JITIHADA ZA KUENDELEA KUELIMISHA WAFANYABIASHARA

Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji Mhe. Charles

Mwijage ameipongeza na kuishukuru Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) kwa jitihada za kuendelea kuelimisha wafanyabiashara kutambua umuhimu wa kulipa kodi utakaoiwezesha Serikali kusonga mbele katika suala zima na ukuzaji wa viwanda vya ndani hapa nchini.

Mhe. Mwijage aliyasema hayo wakati wa ufunguzi wa mkutano wa nne wa mwaka wa Taasisi isiyo ya kiserikali inayotoa Msimbomilia (Barcode) za bidhaa (GS1); uliofanyika tarehe 29 Novemba 2016 katika ukumbi wa mikutano wa Karimjee jijini Dar es Salaam. 

Mkutano huo uliandaliwa kwa ushirikiano kati ya GS1 na TRA kwa lengo la kujadili masuala mbalimbali yanayowahusu wadau wao, kujadili mambo muhimu ya kodi yanayohusu umuhimu wa Namba ya Utambulisho wa Mlipakodi (TIN) katika kuweza kupata msimbomilia (barcodes 620) na kuweza kuzitambulisha bidhaa za Tanzania kimataifa pamoja na kuadhimisha miaka mitano tangu kuanzishwa kwa taasisi hiyo.


Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji Mhe. Charles Mwijage wa tatu kulia akikata keki kuadhimisha mwaka wa nne wa Taasisi isiyo ya kiserikali inayotoa Msimbomilia 620 (Barcode) za bidhaa (GS1) uliofanyika jijini Dar es salaam. Wa kwanza kushoto ni mwakilishi kutoka TRA ambaye ni Afisa Mkuu wa Elimu kwa Mlipakodi Bi. Rose Mahendeka na wa kwanza kulia ni Mwenyekiti wa bodi ya GS1 Bw. Gideon Mazara wakishuhudia tukio hilo.

Waziri Mwijage aliliagiza Shirika la Viwango Tanzania (TBS) kuhakikisha kila mfanyabiashara anayemiliki viwanda vidogo na vya kati kuhakikisha anakuwa na TIN na namba ya msimbomilia 620 inayotolewa na GS1 Tanzania kabla ya kuhuisha vyeti vyao vya biashara.
 
Aidha Waziri Mwijage amesema kuwa uchumi wa viwanda

unatakiwa kukua nchini ili kuweza kuzalisha bidhaa bora

zitakazouzwa ndani na nje ya nchi na kukusanya kodi stahiki

itakayoiwezesha Serikali kutoa huduma bora za kijamii kwa

maendeleo ya wananchi wa Tanzania .


“Ifike wakati wafanyabiashara muwaelewe vizuri TRA na kulipa

kodi stahiki ya Serikali, ili nchi iweze kusonga mbele” alisema

Mhe. Mwijage.


Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji Mhe. Charles Mwijage (katikati) akielezea na kumpongeza Mkurugenzi Mkuu wa kampuni ya Shear Illusions Bi. Shekha Nasser (aliyeshika zawadi) kwa kulipa kodi stahiki ya Serikali ya kati ya Milioni 9 na 12 kila mwezi kupitia kampuni yake ambayo pia imeweza kutoa ajira kwa vijana zaidi ya12. Pongezi hizo alizitoa wakati wa ufunguzi wa mkutano wa mwaka wa nne wa Taasisi isiyo ya kiserikali inayotoa msimbomilia (Barcode) za bidhaa (GS1) uliofanyika jijini dar es salaam.
 
Kwa upande wake Afisa Mkuu wa Elimu kwa Mlipakodi kutoka TRA Bi. Rose Mahendeka alisema kuwa wafanyabiashara wote ambao wanahitaji kutumia mfumo wa kuuza bidhaa kwa kuweka msimbomilia (Barcode 620) wanapaswa kupitia TRA kwa ajili ya usajili na uhakiki wa Namba ya Utambulisho wa Mlipakodi (TIN) kabla ya kwenda kupata huduma ya msimbomilia 620.

Bi. Mahendeka aliwasisitiza wadau hao kuhakikisha wanajisajili na TIN na wale waliojisajili kuhakikisha wanahakiki taarifa zao ili kurahisisha upatikanaji wa Msimbomilia 620 na kuiwezesha TRA kupata takwimu sahihi za wafanyabiashara wazalishaji na wanaouza bidhaa zao nje ya nchi.



Baadhi ya wadau wa Taasisi isiyo ya kiserikali inayotoa Msimbomilia (Barcode 620) za bidhaa (GS1) wakimsikiliza kwa makini Afisa Mkuu wa Elimu kwa Mlipakodi kutoka Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Bi. Rose Mahendeka akitoa elimu ya kodi wakati wa mkutano wa nne wa mwaka wa Taasisi hiyo uliofanyika katika ukumbi wa mikutano wa Karimjee jijini Dar es Salaam.

“Wafanyabiashara wote ambao wanahitaji kutumia mfumo wa kuuza bidhaa kwa kuweka Msimbomilia(Barcode 620) wanapaswa kupitia TRA kwa ajili ya usajili na uhakiki wa Namba ya Utambulisho wa Mlipakodi(TIN) kabla ya kwenda kupata huduma” alisisitiza Bi. Mahendeka.

Aidha Bi. Mahendeka alisema kuwa wafanyabiashara ambao wanahitaji kuuza bidhaa zao kwa kutumia msimbomilia wanapaswa kulipa kodi bila ya kukwepa ili kuiwezesha Tanzania kupiga hatua kufikia uchumi wa viwanda na vilevile kuweza kutoa huduma bora kwa maendeleo ya jamii.

Naye Mwenyekiti wa bodi ya GS1 Bw. Gideon Mazara alitoa rai kwa wafanyabiashara wanaozalisha bidhaa kutumia Msimbomilia 620 wa Tanzania na kuweza kutangaza bidhaa za hapa nchini ili kupata soko la kimataifa litakalowezesha nchi kufikia uchumi wa kati .

Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji Mhe. Charles Mwijage akiwa katika picha ya pamoja na baadi ya wadau wa Taasisi isiyo ya kiserikali inayotoa msimbomilia (Barcode 620) za bidhaa (GS1) mara baada ya kuhitimisha mkutano mkuu wanne wa Taasisi hiyo uliofanyika katika ukumbi wa mikutano wa Karimjee jijini Dar es Salaam.

NAIBU WAZIRI DR. KOLIMBA ALIPOTEMBELEA UBALOZI NAIROBI

Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Dkt. Susan Kolimba, ambaye yuko Nairobi kuhudhuria kikao cha Bunge la Afrika Mashariki, ametumia fursa hiyo kutembelea Ubalozi wa Tanzania nchini Kenya na kuzungumza na watumishi.Katika kikao na Mhe. Waziri, watumishi wa Ubalozi walielezea changamoto mbalimbali wanazokabiliana nazo katika utendaji wa kazi, ikiwa ni pamoja na ufinyu wa bajeti. 

Hata hivyo watumishi hao walisema wameweza kukusanya maduhuli ya kuridhisha na kuhudumia Watanzania wanaopatwa na matatizo kwa kuchangishana wakati mwingine.Mhe. Kolimba alieleza kuridhishwa kwake na utendaji wa watumishi wa Ubalozi wa Nairobi na kuwapongeza kwa moyo wa kujitolea.

Alisema Serikali itajitahidi kupatia balozi fedha na vifaa vya kazi kwa kadri ya uwezo wake, lakini akasisitiza watumishi wawe wabunifu na wajitolee kufidia pale upungufu unapojitokeza.Kikao cha Bunge la Afrika Mashariki kinachofanyika kwenye Bunge la Kenya kinatarajiwa kumalizika kesho.

Baadhi ya watumishi wa Ubalozi wakijipanga kumpokea Mhe. Naibu Waziri


 Mhe. Kolimba akisalimiana na baadhi ya watumishi wa Ubalozi.



 Naibu Waziri, Dkt. Kolimba (kushoto) akifurahia bidhaa za Tanzania kwenye ofisi za Ubalozi wa Nairobi akiwa na Kaimu Balozi, Bi. Talha Mohamed Waziri. 



Naibu Waziri akiongea na watumishi wa Ubalozi. Kushoto ni Kaimu Balozi, Bi. Waziri na Mkurugenzi wa Sera na Mipango wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Bw. James Lugaganya.

AIRTEL YAJIIMARISHA VIJIJINI LINDI

AIRTEL YAPELEKA MAWASILIANO VIJIJINI, YAWEKA MNARA KIJIJI CHA CHELEWENI MKOANI LINDI




Meneja Uhusiano wa Kampuni ya Airtel Tanzania, Jackson Mmbando (kushoto) akimueleza jambo Mkuu wa wilaya Lindi, Shaibu Ndemanga (wapili kulia) juu huduma zitakazotolewa na mnara wa Airtel uliojengwa katika kijiji cha Cheleweni mara baada ya kuzindua mnara huo. katikati ni Meneja Mauzo wa Airtel Mkoa wa Lindi, Saleh Safy. Airtel imejenga mnara huo ambao utatoa mawasiliano katika vijiji vya Ng’apa ngapa, Cheleweni, Nchee, Nantumbya, Nanyuru pamoja na maeneo yanayowazunguka vijiji hivyo. Airtel imezindua huduma hiyo ili kuboresha , huduma za kifedha kwa njia ya mtandao Airtel Money na kuwaweza wananchi wa Lindi kupata mawasiliano ya uhakika katika kuendesha shughuli zao za kila siku kiuchumi na kijamii.



Mkuu wa Wilaya Lindi, Shaibu Ndemanga akizungumza na wananchi wakati wa uzinduzi wa mnara wa Airtel utakaotoa huduma ya mawasiiano katika vijiji vya Ng’apa ngapa, Cheleweni, Nchee, Nantumbya, Nanyuru pamoja na maeneo yanayowazunguka vijiji hivyo. anaefuata ni diwani wa viti maalum Lindi Bi, Somoe Pamui na Meneja Mauzo wa Airtel Mkoa wa Lindi, Saleh Safy.

Frederick Sumaye anyang'anywa ardhi

TanzaniaWaziri mkuu mstaafu wa Tanzania katika awamu ya tatu Fredrick Sumaye.

Rais wa Jamhuri ya Tanzania amefuta hati ya umili ardhi ya shamba kubwa lililokuwa likimilikiwa na waziri mkuu mstaafu Frederick Sumaye kwasababu zilizoelezwa na serikali wa mtaa kuwa liliachwa bila kuendelezwa .
Hatua hiyo imekuja baada ya Tanzania kuzindua kampeni kubwa ya kurejesha ardhi mikononi mwa watanzania ambayo haijaendelezwa na wawekezaji waliomilikishwa awali na kuwapa wakulima masikini .
Hata hivyo, Frederick Sumaye ambaye aliwahi kuwa waziri mkuu kwa muda wa miaka kumi kuanzia mwaka 1995 na kuamua kuhamia kambi ya upinzani baada ya uchaguzi wa Tanzania mwaka wa jana uamuzi ulioelezwa kuwa na msukumo wa kisiasa.
Sumaye alisema kama lengo la kumnyang'anya ardhi yake ni jaribio la kumlazimisha kurejea katika chama tawala, "wasahau ''.
BBC

Binadamu mzee zaidi Emma Morano asherehekea siku ya kuzaliwa

Emma Morano, 116, akiwa nyumbani kwake Verbania, Italia KaskaziniEmma Morano ndiye binadamu mzee zaidi aliye hai.
Binadamu pekee aliye hai, ambaye inatambuliwa kwamba alizaliwa katika karne ya kumi na tisa, leo anasherehekea sikukuu yake ya 117 tangu kuzaliwa kwake.
Emma Morano, alizaliwa katika jimbo la Piedmont karibu na mji wa Milan, Italia tarehe 29 Novemba, 1899.
Wakati huo, kampuni ya magari ya Fiat ilikuwa tu ndiyo imeanzishwa. Klabu ya soka ya Milan nayo ilikuwa imeanzishwa wiki chache awali.
Ameshuhudia wafalme watatu wa Italia wakitawazwa na kuondoka, alizaliwa wakati wa utawala wa Mfalme Umberto wa Kwanza.

Aidha, katika maisha yake, kumekuwepo na Baba Watakatifu kumi na mmoja.
Isitoshe, alishuhudia Vita Vikuu vya Kwanza na vya Pili vya Dunia.
Mwaka huu, alitambuliwa kuwa mwanamke mkongwe zaidi aliye hai baada ya kifo cha Mmarekani Susannah Mushatt Jones mwezi Mei. Ndiye pia binadamu pekee aliye hai ambaye alizaliwa miaka 1800.
Bi Morano anasema sana amekuwa na maisha marefu kutokana na jeni.

Mamake aliishi hadi miaka 91. Dadake wengi pia walifariki wakiwa na umri mkubwa.
Anasema kwa kiwango fulani, lishe yake imechangia. Anasema amekuwa akila mayai matatu - mawili yakiwa mabichi, kila siku kwa zaidi ya miaka 90.
Alianza hayo alipokuwa mwanamke kijana, baada ya madaktari kugundua alikuwa na ugonjwa wa anaemia, ambapo mgonjwa hupungukiwa na seli nyekundu za damu au haemoglobini, muda mfupi baada ya Vita Vikuu vya Kwanza vya Dunia.
Siku hizi amepunguza na hula mayai mawili pekee, na biskuti kadha.
Hilo linaenda kinyume kabisa na ushauri wa sasa wa madaktari kuhusu jinsi ya kuishi maisha marefu na yenye afya, daktari wake wa miaka 27 Carlo Bava ameambia AFP.
"Emma hula mboga chache sana, na hali matunda sana. Nilipokutana naye alikuwa anakla mayai matatu kila siku, mawili mabichi kila asubuhi na moja la kupikwa mchana saa sita na kisha anakula kuku chakula cha jioni."
Licha ya haya, Carla anasema, mwanamke huyo anaonekana kuwa na "maisha tele".

'Nioe au nikuue'
Jambo jingine ambalo Bi Morano anasema huenda limechangia maisha yake marefu, ni hatua yake ya kumfukuza mumewe mwaka 1938 baada ya mtoto wake wa kiume kufariki akiwa na miezi sita pekee.
Ndoa yao ilikuwa inaendelea vyema kwa mujibu wa Bi Morano.
Alikuwa amempenda mvulana aliyeuawa wakati wa Vita Vikuu vya Kwanza vya Dunia na hakutaka kumuoa mtu mwingine.
Lakini aliambia gazeti la La Stampa, alipokuwa na miaka 112, kwamba hakuna na namna nyingine ya kufanya ila kuoa mtu mwingine.
"Aliniambia: 'Ukiwa na bahati utanioa, la sivyo nitakuua'. Nilikuwa na miaka 26. Niliolewa."
Baadaye, ndoa yao ilianza kuvurugika na akamfukuza mumewe ingawa hawakuvunja ndoa yao hadi mwaka 1978 mumewe alipofariki.
Bi Morano alifanya kazi hadi alipotimu miaka 75 na aliamua kutooa tena.
"Sitaki kudhibitiwa na yeyote," aliambia gazeti la New York Times.

Ili kusherehekea siku hii muhimu, wakazi wa eneo la Pallanza karibu na Ziwa Maggiore, ambapo amekuwa akiishi, wanaandaa maonyesho ya mitindo yakiangazia karne tatu katika historia.
Profesa wa masuala ya msambojeni George Church ambaye hufanya kazi katika chuo cha matibabu cha Harvard pamoja na kundi lake la watafiti ambao wamekuwa wakifanya utafiti kuhusu umri wa kuishi, ameambia BBC kwamba binadamu wataendelea kuongeza muda wa kuishi.
"Nafikiri tutashuhudia ongezeko kubwa la muda wa kuishi katika miaka michache iliyopita kutokana na teknolojia, na pia utafiti unaofanyiwa watu wa kipekee kama vile Emma."
Emma bado yuko buheri wa afya.
Hata hivyo, hajaondoka nyumba yake ya vyumba viwili kwa miaka 20.
Carlo anahisi shinikizo kuhusu majukumu ya kumtunza mwanamke huyo mkongwe, ambapo anasema ni kama kuutunza Mnara wa Pisa.
"Ile siku utaanguka, kuna mtu atalaumiwa," aliambia AFP. "Emma atakapofariki, mimi ndiye nitakayewajibishwa."
Mtu aliyeishi muda mrefu zaidi duniani kwa mujibu wa Guinness alikuwa Mfaransa Jeanne Calment, aliyeishi miaka 122 na siku 164. Alifariki Agosti 1997.

BBC

Bashir: Ni rahisi kufanya kazi na Donald Trump

Rais Omar el Bashir wa SudanRais Omar el Bashir wa Sudan.
Kiongozi wa Sudan Omar el Bashir amempongeza rais mteule wa Marekani Donald Trump akisema kuwa itakuwa rahisi kushirikiana naye, kulingana na gazeti la Emirati al Khaljee.
''Bw Trump anaangazia maslahi ya raia wa Marekani, ikilinganishwa na wale wanaozungumzia kuhusu demokrasia ,haki za kibinaadamu na uwazi'',alisema rais Bashir katika mahojiano na gazeti hilo.
Aliongezea kwamba: Tunaweza kushirikina na watu wenye sura mbili lakini huyu hapa mtu mwenye uwazi wa anajua anacholenga.
''Nina hakika itakuwa rais kushirikiana na Trump ikilinganishwa na wengine kwa sababu ni mtu anayeangazia maswala moja kwa moja na mfanyibiashara ambaye anaangazia maslahi ya anaoshirikiana nao'',alisema Bashir.
Bashir ambaye anasakwa na mahakama ya ICC kutokana na mashtaka ya mauaji ya kimbari katika eneo la Drafur amekana mashtaka hayo.
Alichukua mamlaka mwaka 1989 kupitia mapinduzi na ameshutumiwa kwa kuwa na uongozi wa kiimla tangu wakati huo.

Trump kutangaza baraza lake la mawaziri

Donald Trump

Rais mteule wa Marekani Donald Trump anajiandaa kutangaza mawaziri zaidi watakaohudumia utawala wake.
Ripoti zinasema kwamba Trump atamteua mshirika wake wa kibiashara wa zamani Steven Mnuchin kama waziri wa fedha.
Wawili hao walikuwa wanamiliki Goldman Sachs, kampuni ambayo Trump aliikashifu wakati wa kampeni zake.
Pia ameshiriki mazungumzo na Mitt Romney, ambaye anakisiwa kuwa mwaniaji wa wadhfa wa waziri wa mambo ya kigeni.
Donald Trump afanya uteuzi wa mapema
Bwana Romney aliyewania urais kwa tiketi ya chama cha Republican mwaka 2012, kwa wakati mmoja alimwita Trump mtu muongo.
BBC

DC KIGOMA:AWAJIBU MADIWANI WA ACT WAZALENDO - ''NISIPOFANYA KAZI YA CCM NIFANYE KAZI YA NANI?''

Mkuu wa wilaya ya Kigoma Bwana Samson Anga amethibitisha kwamba ni kweli anafanya kazi ya CCM katika kutimiza majukumu yake ya kila siku akijibu shutuma zilizotolewa na mwenyekiti wa Madiwani Mkoa wa Kigoma bwana Yunus Ruhomvya ambaye pia ni diwani wa Manispaa ya Kigoma Ujiji.
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEh9K3Hv6dJWlZ2kJyRTe-3_NZXW-IuJShPZWza7Kqxfu8TUZ2nPnaCFtXKFlcpTR_jUeu4BOfIs-EghevjObNtUb8fMtAOgXe29XLm8g2mv3us8s1ZOHLrjABr4B6NVk34D0KAllDyWpmWe/s1600/DSC_0259.JPG
 picha ya maktaba inamuonyesha  Katibu Tawala Mkoa wa Kigoma, Charles Pallangyo (kulia) akiteta jambo na Mkuu wa Wilaya ya Kigoma, Samson Anga.

juzi JAMVI LA HABARI liliripoti juu ya kauli ya mwenyekiti huyo wa madiwani akisema kuwa mkuu wa wilaya na ofisi yake wanakwamisha maendeleo ya manispaa hiyo kwa kufanya kazi za CCM badala ya kufanya kazi ya kiserikali na hivyo kuwakwamisha.

''Ngoja nikujibu ..wewe kwa mtazamo wako ulitegemea mimi nifanye kazi za nani?, kwa mtazamo wako wewe,...kawaulize mlitaka afanye kazi za nani?, nyinyi mlitaka afanye kazi za nani, nenda kawaulize?''. alijibu DC Anga.
                                           
Rashid Yunus Ruhomvya.
Mwenyekiti wa Madiwani wa chama cha ACT WAZALENDO mkoani kigoma

''naomba ukawaulize hao wanaolalamika kwamba  mimi nafanya kazi za CCM, Kawaulize walitaka nifanye kaze za nani?, unategemea nisipofanya kazi za CCM nifanye kazi za nani?.'' aliongeza DC huyo.

Tuesday, November 29, 2016

BREAKING NEWS: RC MAKONDA ASHITAKIWA KUDHALILIISHA WANAWAKE NA KUKOSA MAADILI

https://i2.wp.com/millardayo.com/wp-content/uploads/2016/03/Makonda.jpg?resize=536%2C368
  •  Ni na NGOME YA WANAWAKE YA CHAMA CHA ACT WAZALENDO
  • Ni kutokana na Matusi aliyoyaporomosha Mkutanoni dhidi ya Afisa Ardhi
  • Yawataka Watetezi wa wanawake wasimame kidete kutetea wanawake wenzao

Na. Mwandishi wetu
Ngome ya Wanawake ya chama cha ACT WAZALENDO imemshtaki mkuu wa mkoa wa Dar es salaam Mheshimiwa Paul Makonda kwa kitendo chake cha kumuita mtumishi wa halimashauri ya kinondoni kichaa hadharani.

taarifa ilisosambazwa na Afisa habari wa chama hicho Abdallah Khamisi iliyosainiwa na Katibu wa Taifa wa Ngome hiyo ya wanawake ya ACT wazando Bi. Ester Kyamba, inasema kuwa ngome yao imesikitishwa, kufedheheshwa na kuudhunishwa na kauli hiyo isiyo ya kiungwana na isiyoendana na maadili ya watanzania na utanzania.

zaidi, tafadhali karibu uipitie taarifa yao. 

NGOME YA WANAKE - ACT WAZALENDO.

                                                             TAARIFA KWA UMMA
---------------------------------------------------------------------------------------------------
Ngome ya Wanawake ya Chama cha ACT Wazalendo imeshtushwa na kuhuzunishwa na kauli zisizo za kiuongozi na zisizozingatia kanuni za Maadili ya Utumishi wa Umma zinazoendelea kutolewa na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda.

Jana, katika mkutano anaouita wa kutatua kero, Bwana Makonda ameendelea kushindwa kutatua kero na badala yake kuongeza kero ya kudhihaki, kukejeli na kutukana hadharani wananchi anaowaongoza na watumishi anaowasimamia kitendo ambacho ni kinyume na maadili ya Watanzania.

Kitendo cha Mkuu wa Mkoa Makonda  akiwa katika eneo la Mabwepande, Wilaya ya Kinondoni Mkoani Dar es Salaam kumtolea lugha ya udhalilishaji Afisa Ardhi wa Manispaa ya Kinondoni Bi Rehema Mwinuka kwa kumtamkia kuwa; "Hawa ndio vichaa tunaohangaika nao, toka hapa". kimetusikitisha Sana na tunakilaani kwa nguvu zetu zote. 

Kauli kama hii sio tu haikupaswa kutolewa na kiongozi mkubwa katika ngazi ya Mkoa lakini pia ni kauli mbaya ambayo ililenga kumdhalilisha na kumvunjia heshima yake mbele ya umma Bi Rehema Mwinuka.

Ngome ya Wanawake ACT Wazalendo, Leo tarehe 29.11.2016 imepeleka mashtaka rasmi dhidi ya Mkuu wa Mkoa huyo mbele ya Tume ya maadili ya viongozi wa umma na utawala bora kuwataka wamuwajibishe kwa kitendo chake hicho cha utovu wa maadili. 

Ngome ya Wanawake ACT Wazalendo inamtaka pia Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam atambue kuwa kwa kuzingatia Sheria ya Utumishi wa Umma ya mwaka 2002 pamoja na Kanuni za Maadili ya Utumishi wa Umma, kanuni ya 65(1) inamtaka mtumishi wa umma;

_"kuepuka kufanya vitendo viovu au kutamka maneno yanayolenga kuwaaibisha watumishi wa ngazi moja, za chini yao au wa vyeo vya juu"._

Alichofanya Mkuu wa Mkoa ni kumuaibisha na kumtolea lugha ya udhalilishaji Bi Rehema Mwinuka kinyume cha Sheria na Kanuni za Utendaji katika Utumishi wa Umma.

Ngome ya Wanawake ACT Wazalendo inaitaka Tume ya Maadili na Utawala Bora ifanye uchunguzi na kuchukua hatua dhidi ya matamshi mbalimbali yaliyotolewa na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam ambayo yalikiuka sheria ya Maadili ya Utendaji katika Utumishi wa Umma.

Ngome ya Wanawake ACT Wazalendo inayataka pia Mashirika na Asasi mbalimbali zinazosimamia Haki za Binaadamu, Haki za Jinsia na Utawala Bora kupaza sauti dhidi ya kauli isiyo ya kiuongozi iliyotolewa na Mkuu wa Mkoa dhidi ya Afisa Ardhi wa Manispaa ya Kinondoni Bi Rehema Mwinuka.

Kadhalika,  Ngome na Chama kwa ujumla tutaendelea kuwasemea wanyonge wote popote walipo kwa kadri ya uwezo wetu. 

Imetolewa na:
Esther Kyamba,
Katibu,
Ngome ya Wanawake
 ACT Wazalendo
Ester Kyamba Katibu Ngome ya wanawake ACT WAZALENDO

.

Saturday, November 26, 2016

BREAKING NEWS:- MADIWANI ACT WAZALENDO WAWAVAA MKUU WA MKOA, WILAYA KIGOMA


 Meya wa Manispaa ya Kigoma Ujiji Hussein Ruhava Kushoto akiteta jambo na Mbunge wa Jimbo hilo Zitto Kabwe katika picha ya maktaba

 Rashid Ruhomvya.
Mwenyekiti wa Madiwani wa chama cha ACT WAZALENDO mkoani kigoma
 Hussein Ruhava Mstahiki meya Manispaa ya kigoma ujiji akiongea na wananchi.
Hussein Ruhava Mstahiki meya Manispaa ya kigoma ujiji akiongea na wananchi.

Na. Mwandishi Wetu, Kigoma
Mwenyekiti wa Madiwani wa Chama cha ACT WAZALENDO mkoani ambaye pia ni mwenyekiti wa kamati ya Elimu,Uchumi na Afya katika Halimashauri ya manispaa ya Kigoma Ujiji ambayo inaongozwa na chama hicho mheshimiwa Rashid Ruhomya, leo amewashtaki kwa wananchi wa Manispaa hiyo Mkuu wa wilaya ya Kigoma mheshimiwa Samson Anga kuwa anampotosha mkuu wa mkoa na mkurugenzi mtendaji wa halimashauri hiyo kwa kujikita katika kuitetea CCM na kuacha kufuata maamuzi halali ya halimashauri.

akiwahutubia wananchi waliojitokeza kwa wingi katika mkutano ulioitishwa katika kata ya Kigoma mjini uwanja maarufu wa Kigoma Sinema kuzungumzia utekelezaji wa ilani ya uchaguzi ya chama chao kwa kipindi cha mwaka mmoja tangu wachaguliwe..

''kwa kipindi kirefu sasa Mkuu wa wilaya amekuwa akifanya kazi ya CCM, sisi baraza la madiwani tunapanga mipango ya maendeleo, tunaipitisha halafu yeye anakaa na wana CCM wenzake wanazuia utekelezaji''. alisema Ruhomvya.

''mpaka hivi sasa, baada ya mkuu wa wilaya kumvuruga mkurugenzi, na kuzuia mipango ya maendeleo, 
sisi baraza la madiwani tumempigia Kura ya kutokuwa na imani mkurugenzi wa Manispaa na tumeamua kumng'oa ili akakae na CCM wenzake''. aliongeza
 https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEh9K3Hv6dJWlZ2kJyRTe-3_NZXW-IuJShPZWza7Kqxfu8TUZ2nPnaCFtXKFlcpTR_jUeu4BOfIs-EghevjObNtUb8fMtAOgXe29XLm8g2mv3us8s1ZOHLrjABr4B6NVk34D0KAllDyWpmWe/s1600/DSC_0259.JPG
picha ya maktaba inamuonyesha  Katibu Tawala Mkoa wa Kigoma, Charles Pallangyo (kulia) akiteta jambo na Mkuu wa Wilaya ya Kigoma, Samson Anga.

''Manispaa ni Serikali inayojitegea (is an aotonomous), maamuzi yake hakuna mamlaka ya kuyatengua, si mkuu wa wilaya wala mkuu wa mkoa, sasa namshanga huyu mkuu wa wilaya wakuja hapa anataka kutuharabia mipango yetu ya maendeleo. nawahakikishia ndugu zangu wa kigoma tutawapigania kufa na kupona na tutamshinda. maslahi ya wana kigoma lazima tuyaweke mbele kuliko vyama vyetu''. aliongeza Ruhomvya

naye Mstahiki Meya wa Manispaa hiyo Hussein Ruhava amewahakikishia wananchi hao kuendelea kuwatumikia kwa moyo mkunjufu na nguvu zote na kusisitiza hawatakatishwa tamaa.

''mkuu wa mkoa ameunda kamati maalum kushughulikia mradi wa Mgebuka Square, hiyo haituzuii sisi kuendelea na mradi huo, mkandarasi anaendelea kuweka Pavements na tunahakika mradi hautasimama''. alisisitiza Meya Rugava


STRAIGHT BOOK: SULUHISHO LA WAFANYABIASHARA TANZANIA

 
Bi. Maua Rubibi.
umoja wa wafanya biashara ndogo ndogo mikoa ya kigoma,tabora, mwanza na Dar es salaam wamefurahia elimu ya mfumo mpya ya utunzaji wa kumbukumbu za kibiashara zao unaohusisha mauzo na bakaa (stocks) waliyopewa kwa njia ya mtandao wa Whatsapp na Afisa masoko wa taasisi ya Straightbook bi. Maua Ramadhani Rubibi hivi karibuni.

bi maua ameelimisha kuwa Straight ni huduma nafuu yenye  bei tofauti tofauti kulingana na uwezo na uhitaji wa mtumiaji,
 ''Ukitumia online utalipia 20elfu Kwa mwezi, utajiregister Kwenye website yetu www.straightbook.com ila ukifanyiwa installation kuna malipo ya aina tatu, Moja utalipia 25elfu kwa mwezi for single user ila njia ya pili kwa yule hataki kulipia mwezi mwezi atalipia laki5 kisha atatumia mfumo na kulipia laki moja moja kwa ajili ya upgrades na supports kila mwaka Njia ya mwisho ni kununua package na kutumia bila malipo mengine, hii utalipa mill 1.9 (million moja na laki9) utapata free supports na upgrades Kwa kipndi chote na Kwa idadi yeyote ya watumiaji, straightbook haina limit ya users na pia mnaweza kushare kwnye local network moja, karibu sana''.

MAKALA: SERIKALI ILITAFAKARI UPYA SUALA LA KAGERA



Na, BARAKA NGOFIRA
0763580901
 http://fullshangweblog.com/home/wp-content/uploads/2016/09/3-29.jpgwaziri Jenista Mhagama akiwa na Mwenyekiti wa kamati ya maafa mkoani kagera mkuu wa mkoa huo Mustafa Kijuu.
Septemba kumi mwaka huu tetemeko la ardhi lilikumba mikoa ya kanda ya ziwa huku janga kubwa likiwa limeachwa mkoani Kagera ambapo zaidi ya watu 17 walipoteza maisha papo hapo. Mbali na maafa hayo nyumba zaidi ya 2000 zilibomoka na kuharibiwa vibaya na kuwaacha wakazi wengi wa mkoa huo wakiwa hawana makazi.

Serikali na wadau mbalimbali walifanya kila liwezekanalo ili kupeleka misaada ya kibinadamu ikiwemo chakula na mablanketi kwa waathirika ili waweze kujihifadhi. Huku serikali na wadau wengine wakikusanya nguvu ili kuwasaidia wanakagera kurudi kwenye hali yao waliyokuwa wameizoea kabla ya kukubwa na tetemeko la ardhi.

Miundombinu ikiwemo barabara, umeme, maji, shule na mingi iliharibiwa vibaya na tetemeko hilo. Shule kongwe za Ihungo na Nyakato ni moja ya taasisi ambazo ziliharibiwa vibaya sana na tetemeko la ardhi. Hali iliyosababibisha serikali kuwahamisha wanafunzi katika shule nyingine ili waweze kuendelea na masomo huku juhudi mbalimbali zikifanywa na serikali kurudisha shule hizo katika hali yake ya kawaida.

Salamu za pole kutoka kwa viongozi wan chi mbalimbali zilitumwa nchini, na msaada kidogo kama kifuta machozi kwa waathirika wa Kagera. Mashirika mbalimbali ya ndani ya nchi, taasisi za umma na watu binafsi walitoa misaada mbalimbali ili kuwasaidia waathirika wa tetemeko la Ardhi.
 http://mtembezi.com/wp-content/uploads/2016/09/DV2A3561.jpgsehemu ya madhara ya tetemeko la kagera.
Mbali na juhudi zote hizo vyombo vya habari havikuwa nyuma kuuhabarisha umma kwa kila hatua iliyokuwa inaendelea juu ya makusanyo mbalimbali ya kuchangia waathirika wa tetemeko la Kagera. Viongozi mbalimbali hasa kutoka Ofisi ya waziri mkuu kitengo cha maafa, walipewa muda mwingi na vyombo vya habari ili Kutoa tathmini yao na wapi walipofikia bila kusahau Kutoa msisitizo kwa raia watanzania na wadau mbalimbali wajitokeze kuchangia janga hili.

Kwa kufanya hivyo jamii na mashirika mbalimbali yalijitokeza kwa wingi huku baadhi ya wadau na wataalam wakiwemo wale kutoka chuo kikuu cha Dar es salaam na vyuo mbalimbali walijitolea kufanya tathimini bure kabisa. Ambapo walitumia pesa zao wenyewe kutathimini na kutoa ushauri kwa serikali juu ya nini kifanyike ili kuirudisha Kagera na wakazi wake katika hali ambayo waliizoa.

Wakati hayo yote yakiendelea mwanzoni kabisa mwa zoezi hili kasoro iliingia kwa baadhi ya watumishi wa umma ambao hawakuwa waamini ambao walitaka janga hili kwa ajili ya kujishibisha. Ambapo baada ya kugundulika kufungua akaunti feki iliyokuwa na jina sawa na ile ya kupokea misaada ya Kagera walitumbuliwa mara moja na kupelekwa mahakamani ili kupambana na sheria.

Mbali na hao kutumbuliwa lawama nyingi zilisikika kuwalalamikia viongozi hao kugawa misaada hiyo kwa watu kulingana na itikadi za vyama. Ambapo wafuasi wa chama tawala walionekana kupewa upendeleo huku wenzao wa vyama vya upinzani wakibaki kula kwa macho. Jambo ambalo lilikemewa mara moja na viongozi wa ngazi ya juu ya serikali japo sina uhakika kama lilikisha au la!

Huku hayo yote yakiendelea serikali iliwatangazia wakazi wa Kagera kuwa wajijengee nyumba kwani serikali haina pesa za kujenga nyumba kwani tetemeko halikuletwa na serikali. Kauli hii iliibua maswali mengi miongoni mwa wadau na wakazi wa Kagera ambao walikuwa ni walengwa wa kauli hiyo. Lakini wajipa moyo na kupiga moyo konde na kuendelea na ujenzi japo wana hali mbaya. Ambapo mpaka leo wengi bado wanasubiri usiku uishe ndo waanze kujenga huku hawana mbele wala nyuma na kukaa pasipo kujua wapi wataanzia kujenga na chakula kubaki kukisikia  na kukiona kwa majirani.

Huku wakiwa wanaendelea na shughuli zao za kujijenga kisaikolojia, mwanzoni mwa mwezi huu serikali kupitia mkuu wa mkoa huo ilipigilia msumari wa moto kwenye donda ambalo halijapona. Baada ya kuutangazia umma kuwa misaada iliyotolea na wadau na nchi wahisani zitatumika kwenye ujenzi wa miundombinu mbalimbali ya mkoa huo. Ambapo alikaririwa akisema kuwa ni maamuzi ambayo yamefikiwa kwenye kikao cha kamati ya maafa ya Mkoa huo.

Lakini pia Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania alilibariki jambo hilo na kusema kuwa pesa hiyo ya maafa itatumika kujenga maghorofa mkoani humo ambayo anaamini kuwa hayatabomoka hata tetemeko la aina gani lipite. Jambo ambalo lilizua maswali mengi miongoni  mwa watanzania na kuzua gumzo kubwa mitandaoni ndani na nchi za jirani. Swali kubwa likiwa ni kwa nini serikali imeamua kuimarisha miundombinu ya mkoa huo huku watu wengi walioathirika wakiwa hawana chakula na malazi.

Ambapo wadau mbalimbali waliona ni uonevu na utapeli wa wazi wazi na kutojali wanyonge ambako kunafanywa na serikali ya Tanzania nchini ya Rais Magufuli. Itakumbukwa kuwa misaada yote iliamuliwa ikusanywe kwa mkuu wa mkoa wa Kagera ili iwe rahisi kugawanywa kwa wananchi lakini hali imekuwa tofauti na matarajio ya wengi. Kwani serikali imeamua kutumia nguvu na kuaamua kutumia nguvu na kubadilisha matumizi ya misaada ya kibinadamu kwenda kwenye matumizi ya maendeleo.

Jambo ambalo lingeweza kungoja bajeti ya mwaka mpya wa fedha au miradi ambao nchi wahisani wangeweza kusaidia nchi kama wanavyosaidia miradi mingine ya maendeleo. Kilichofanywa na serikali na sawa na msemo usemao aliyeshiba hamujui mwenye njaa, maana hata nguvu za kumsumbua hana.

Sikatai kuwa kilichofanywa na serikali ni kibaya la hasha bali naweza kusema ni kupungukiwa kwa ubinadamu na kuangalia ni nini kifanyike kwanza, maisha ya wakazi wanao lala nje na kukosa chakula au kuwajengea barabara na maghorofa ambayo wenye hela zao ndiyo watayafaidi na kupitisha magari yao. Huku maskini wanaotembea kwa miguu au wenye baiskeli zao wakiwa hawana mbele wala nyuma.

Hivyo basi ni vyema serikali ikatazama upya kuhusu misaada hiyo na kutoa misaada ya kibinadamu kwanza ikiwemo chakula na malazi kwa familia ambazo hazina uwezo au zina uwezo duni wa kipato cha kumudu kujenga nyumba na kununua chakula.

Makala hii imeandikwa na mwanafunzi wa mwaka wa tatu wa shahada ya kwanza ya mawasiliano kwa Umma katika Chuo kikuu cha Dar es salaam. Anapatikana kwa barua pepe ya barakangofira@gmail.com au simu 0763580901

MAKALA: PROF. NDALICHAKO ONDOA PAMBA MASIKIONI UWASIKIE WANAO WANAVYOTESEKA KWA KUKOSA MIKOPO ELIMU YA JUU.



NA, BARAKA NGOFIRA
0763580901
Tatizo la mikopo kwa wanafunzi wa elimu juu limekuwa likipigiwa kelele kila siku na wadau mbalimbali wa elimu, huku wanafunzi wa vyuo vikuu wakiwa wahanga wakubwa wa mikopo. Hata wale wanaonufaika na mkop huo ambao hutolewa na bodi ya mikopo ya elimu ya juu HESLB. Kwa uzoefu wangu mdogo wa kwenda kuangalia ofisi za bodi ya mikopo zilizopo Mwenge jijini Dar es salaam hakuna siku hata moja ambayo sikukuta wanafunzi kutoka vyuo mbalimbali wakifuatilia mikopo yao.
 https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEjss_lOibdPKmM35Ac8hu4kdHh0kAgfAqUQZ_fPns51ESqIBsxv0Mtfz5FeUDjakjFf2Mcv8CB8S0deJIV7lPDTTfOHMmUIqzrw4uThPl4UP1Y8CuD1JCLwy8gZiBxX7ePe9Qfr-bmGotU/w1200-h630-p-nu/NDALICHAKO.jpgProf. Joyce Ndalichako waziri wa Elimu
Wengi wao ni watoto wa maskini na wakulima ambao wametoka mikoani na kuchaguliwa vyuo vilivyo Dar es salaam na maeneo ya jirani. Lakini pia wapo wale ambao huingia gharama za kuja Dar es salaam kufuatilia mikopo lakini kwa masikitiko huambulia kupoteza nauli na muda wao bure na kuamua kusitisha masomo ambayo ndiyo njia pekee ya kuishi ndoto zao.

Tangu serikali itoe majina ya wanufaika wa mkopo wa elimu ya juu ambayo mpaka sasa ni zaidi ya wanafunzi elfu ishrini na moja wa mwaka wa kwanza ambao wamepewa mkopo kati ya waombaji zaidi 58000 walikuwa wameomba mkopo. Huku lengo la serikali kwa mwaka huu likuwa kuwapa mkopo wanafunzi 25,500 tu kwa mwaka huu wa fedha. Kwa idadi hiyo ni sawa na asilimia kama 38 hivi za waombaji wote wa mwaka huu wa masomo 2016/17.

Nimekuwa nikipokea simu na jumbe nyingi kwenye simu yangu za wanafunzi, wazazi pamoja na walezi wa wanafunzi mbalimbali wakilia mizigo mizito na msongo wa mawazo walionao kwa kukosa mkopo wa elimu ya juu huku sifa zote wakiwa nazo. Lakini mkopo wamenyima hivyo kuwalazimu watoto wao kusiotisha masomo na kurudi nyumbani kulima na kuchunga ng’ombe maana ndizo kazi pekee ambazo zimewakuza na kuwasomesha. 

Kwa taarifa zisizo rasmi zaidi ya wanafunzi 10,000 wa mwaka wa kwanza kwa mwaka huu pekee bado hawajaripoti kwenye vyuo walivyopangiwa. Idadi hii ni kubwa sana kwa taifa na ni aibu kwa taifa ambalo serikali inajigamba kuwa ni tajiri kwa kuwa na maliasili nyingi, madini ya kila aina, gesi na mbuga na hifadhi nyingi za wanyama wa kila aina. Lakini cha ajabu  imeshindwa kutoa elimu bure au kuchangia pesa ya kujikimu kwa kila mwanafunzi wa elimu ya juu.
 https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEguEIREjMkRYAPV5I9T6a40Nc31vA5Yj_24PQsTbcIyVPjwK-vbP_5dZiLx_tJ3Xx6rHhciOMBHvu4USIFZEb3GaZJ6yg3uiYAb93G_eIf5CyDe3NJQk8gbsbKD42hkBFdH6dYq75_-3uyH/s1600/udsm.jpg
wanafunzi wa chuo kikuu.
Kwa muda sasa nimekuwa nikitiwa kichefuchefu na kauli za viongozi wa serikali hasa walionufaika kusomeshwa na serikali. Bila hata ya aibu husubutu kusema hadharani hata bila ya aibukuwa enzi wao wanasoma serikali ilikuwa ikiwahudumia kila kitu, kazii yao ilikuwa ni kusoma tu.
Na cha kushangaza hadi magari walikuwa wakipanda bure, kalamu, sabuni, chakula, malazi, posho, yaaani kila kitu kwao kilikuwa ni bure. Lakini leo baada ya kupata elimu wamesahau yote ambayo serikali iliwatendea badala yake wameondoa kila kitu na kuweka elimu ya kujitegemea ili wao na wanao waendelee kufaidi matunda ya nchi hii.

Inasikitisha sana pamoja na vilio vyote vya wanafunzi maskini na hoe hae ambao kwa sasa hawana mbele wala nyuma lakini kwa sasa wako vyuo vikuu wamebaki njia panda. Na hivyo kuamua kufanya ofisi za bodi ya mikopo kuwa shule yao ambapo kila kukicha wao huenda na kurudi lakini bado serikali imeziba masikio. Haisikii haioni na wala hata haijali maana watoto wao wanasoma vyuo vikuu vya nje na kama wapo vyuo vikuu vya ndani mkopo wamepewa kwa asilimia mia moja maana wao ni watoto wa mabosi.

Agness Leonard mwanafunzi aliyechaguliwa kujiunga na shahada ya kwanza ya ualimu Chuo Kikuu cha Dar es salaam na kupewa namba ya usajili ya 2016-04-00782. Ni miongoni mwa maelfu ya  wanafunzi waliokosa mkopo kwa mwaka huu huku akiwa anatokea familia maskini. Ambao wanandoto ya kupata elimu ya chuo kikuu lakini kwa sababu ya kukosa mkopo huku wakiwa na ufaulu mzuri ameamua kusitisha masomo yake huku hata nauli ya kurudi nyumbani kwao Tabora hakiwa hana.

Amesoma kwa shida sana na kwa bidii huku akiamini kuwa akifaulu na kujiunga na elimu ya chuo kikuu walau uchungu wa maisha utapungua. Lakini zilikuwa ni ndoto za mchana kwake ambazo kwa sasa hana tena matumaini na kubaki kufutwa machozi na rafiki zake.

Maisha ya kushindia mkate wa shilingi mia tano kila siku yamemshinda maana kwa sasa hata hiyo 500 ya kununulia mkate hana. Haya ndiyo maisha ya watoto wengi wa maskini na makabwela wanaosoma vyuo vikuu.
Inatia hasira sana kuona serikali inaweka vipaumbele vya mikopo kwa wanafunzi wa masomo ya sayansi na mengine yakiachwa bila kipaumbele huku wanaosoma masomo ya biashara na sanaa wakiachwa. Na cha kushangaza zaidi wanaosoma masomo ya sayansi wenyewe mara baada ya kumaliza vyuo hawathaminiwi na serikali yao.


Ndiyo ni jambo zuri kuwekeza kwenye masomo ya sayansi lakini mbona hata wanasayansi waliosomeshwa na serikali tena kwa gharama kubwa faida yao haionekani. Nasema haionekani kwa sababu hatuna unachokitengeneza cha kwetu, viberiti, chumvi, kalamu, pamba za kutolea uchafu maskioni na hata njiti za kutolea mabaki ya chakula tunaagiza nje? 

Japo sera na mikakati ipo ya kuboresha viwanda vya ndani ili nasi tuwe na vya kujivunia, ni bora serikali ikaweka mipango mikakati ya mikopo kwa wanafunzi wote wa elimu ya juu pasipo kuwa na ubaguzi.
Rais Magufuli alisisitiza kuwa mikopo ya elimu ya juu itakuwa kipaumbele ikiwa atachaguliwa. Lakini leo imekuwa danganya toto kwa wanafunzi wa vyuo vikuu na kuongeza uchungu zaidi kwao kwa kuwacheleweshea mkopo ambapo hadi waandamane na kupiga kelele kwenye vyombo vya habari ndipo wapewe.

Cha kushangaza zaidi ni baadhi ya watu ambao hata hawakuwahi kusoma au kunufaika na fedha za mkopo wa elimu ya juu majina yao kuonekana kwenye orodha ya wadaiwa sugu. Jambo ambalo linatia shaka kwa utendaji na usahihi wa taarifa na utunzwaji wa kumbukumbuku za wanafuika wa mikopo kwa elimu ya juu.
Chonde chonde waziri wa elimu wasaidie watoto wa maskini wapate mkopo wasome elimu ya juu kama wewe na wenzako mlivyonufaika na elimu ya bure mliyopewa na serikali kwa kipindi chenu. Ni haki yao kupata mkopo maana ni kodi za wazazi wao na babu zao waliowawekea ninyi mazingira mazuri ya kusoma na kushikia nyazifa mlizonazo.

Lakini kama mmeamua kuendelea kuweka pamba maskioni ili watoto wenu waendelee kusoma ili waje kuongoza taifa ili haina shida lakini tambueni kuwa ipo siku Mungu atajibu maombi yao. Maana machozi yao hayapotei bure.

Makala hii imeandikwa na mwanafunzi wa mwaka wa tatu wa shahada ya kwanza ya mawasiliano kwa Umma katika Chuo Kikuu cha Dar es salaam. Anapatikana kwa mawasiliano ya barua pepe ya barakangofira@gmail.com au 0763580901.

Maisha ya Fidel Castro katika picha

Picha za maisha ya Amri jeshi mkuu Fidel Castro,aliyeongoza mapinduzi ya kikomunisti na kuiongoza Cuba kwa miaka 50.
(PICHA HIZI NI KWA MUJIBU WA MTANDAO WA BBC SWAHILI.)
 Fidel Castol 

Fidel Castro alizaliwa mwaka wa 1926, azaliwa mkoa wa kaskazini mashariki wa oriente nchini Cuba na tajiri wa ukuzaji wa miwa. Alijiunga na siasa za mapinduzi akiwa na umri mdogo.Fidel Castol 
Baada ya miaka miwili jela kwa kuongoza mapinduzi yaiyotibuka, alienda mafichono nchini Mexico. Mwaka 1956 alirudi na chama chake cha mapinduzi kikaongoza.Castro mwishowe akapata mamlaka ya kuiongoza Cuba tarehe 1,mwaka 1959,kama waziri mkuu kwa kumshinda Fulgencio Batista
Fidel Castol 

Mwaka 1961,Castrol aliongoza kikosi chake cha jeshi dhidi ya raia wa Cuba 1,500 waliokuwa uhamishoni. waliohamishwa walikuwa wanafadhiliwa na CIA, walivamia Bay of Pigs ili kuishinda serikali yake Kennedy 

Alipata majaribio kubwa mwaka 1962 , pale rais wa Marekani John Kennedy alipomuonya kuondoa makombora yake kutoka cuba
Nikita Khrushchev na Castrol 

Mwishowe,viongozi Nikita Khrushchev na Castro waliondoa makombora na tishio la vita vya nyuklia vikazuiwa

Castrol
 Amri jeshi mkuu huyo alipenda kushiriki mchezo wa baseball. Hapa anaonekana akicheza katika chuo cha ualimu huko Sierra Maestra mwaka wa 1962.

CastrolWacuba wengi walimchukulia kama dikteta wa ukandamizaji??

 Raia wa Cuba 

Mamia ya raia wa Cuba walikimbia makwao,kuelekea Marekani,kwa kutumia maboti yaliokuwa hatari

Castrol
Castrol 

Baada ya kufanyiwa upasuaji wa utumbo, alimkabidhi rasmi madaraka ya urais kakake Raul.Alioneka mara chache,kabla ya kung’atuka madarakani mwezi Februari mwaka 2008 
 Castrol 

Mwezi Septemba, Fidel Castrol alihutubia umma kwa mara ya kwanza baada ya miaka minne. Hotuba yake ilikuwa ya kwanza tangu mwezi Julai mwaka 2010 alipotoka kufanyiwa upasuaji wa utumbo. Alionekana kwa umma alipokuwa akisherehekea mwaka wa 90 wa kuzaliwa kwake mwezi Agosti

NOTE: BBC ni shirika la habari la Uingereza na pengine waliyoyaandika yanaweza yakatofautiana na msimamo wa kijamaa.