Na Mwandishi Wetu
UFISADI
mkubwa umefichuliwa katika pori la akiba la serious Kanda ya Kusini
Mashariki Liwale, baada ya mhifadhi wa pori hiyo kuhusishwa na ufisadi
mkubwa wa mamiilioni ya shilingi, kuchukua kadi za benki za watumishi
pamoja na kutengeneza watumishi hewa.
Profesa. Jumanne Maghembe Waziri wa Maliasili na Utalii wizara inayosimamia Hifadhi za Taifa na mapori ya Akiba.
Taarifa
iliyopatikana kutoka kwenye pori hilo, ilieleza kuwa Mhifadhi Mkuu,
Salum Ramadhan Kulunge amekuwa akifanya malipo hewa pamoja na kuwalipa
watumishi ambao hawajashirikishwa doria pamoja kutumia gari la serikali
yenye namba T. 753 AFA na STL 2497 kubeba mbao zilizokamatwa.
Ilisema
miongoni mwa watumishi wanaoingizwa majina yao katika orodha ya
watumishi wanaokwenda doria ni pamoja na Chiku Kwilasa, ambaye amekuwa
akilipwa fedha bila kufanya kazi zozote huku hata jina lake likiwa
halipo kwenye kitabu cha ukaguzi wa silaha na mahudhurio ofisini.
Nyaraka
zingine zilionyesha kuwa mhifadhi huyo, amekuwa akiajiri watumishi hewa
huku pia baadhi yao akiwa yeye ndie anashikiria kadi zao za benki, kwa
kutoa fedha mbalimbali, ambapo baadhi ya nyaraka zilionyesha zaidi
milioni 20 zilichukuliwa katika kipindi cha miezi minne.
JAMVI LA HABARIi lilibahatika kupata majina ya watumishi kadhaa ambao zilionyesha
akaunti zao ziliingizwa fedha na kutolewa na kampuni mbalimbali
zinahusiana na mambo ya utalii kwenye pori hilo.
Mmoja
wa watumishi hao, aliyekataa jina lake kuwekwa gazetini, alisema
wameshafikisha kilio chao Wizara ya Maliasili na Utalii kueleza tatizo
hilo, ambalo kwa namna moja au nyingine hakuna msaada waliopata.
"Mimi
hapa sina kadi ya benki, lakini kuna hela zaidi ya milioni sita
iliingizwa katika akaunti yangu na taasisi ya uwindaji ya TAWISA, na
baadae ilitolewa bila hata mimi kujua, na nilipogundua baada ya kwenda
benki kuomba taarifa za benki ndio nikagundua kuna kiasi kikubwa cha
fedha kinaingia na kutoka,''alisema.
Aidha,
alisema kuna mbao huwa tunazikamata kwa watu wanaoingia ndani ya
hifadhi, ambapo huwa anazibeba na kuzipakia kwenye magari ya serikali
namba hizi T. 753 AFA na STL 2497 na kuzisafirisha kwenda kuziuza.
Pia,
taarifa zaidi zilieleza mkuu huyo, amekuwa hawalipi watumishi kutopata
stahiki za malipo pindi wanapofanya kazi pamoja na kutoa adhabu kwa
watumishi zisizofuata sheria na kanuni za utumishi wa umma.
Taarifa
hiyo, ilisema kiongozi huyo, anawatimua kazi watumishi huku akishindwa
kuwapa nafasi za kujitetea huku akizuia watumishi kutekeleza wajibu wao
huku akiwa ni miongoni mwa vinara wanaodaiwa kuiba mbao zinazokamatwa
zilizovuna kinyume na taratibu.
Hata
hivyo, tulipowasiliana na Salum alisema hawezi kusema
chochote lakini tuhuma zote anazijua na kuzifahamu na hivi sasa hawezi
kutoa tamko kwa kuwa Wizara inafanya uchunguzi wa suala hilo ili
wachukue hatua.
"Nakuomba usitoe taarifa hadi uchunguzi utoke, yote nayafahamu hayo, nimeshatoa utetezi wangu,''alisema na kuomba aachwe.
Hivyo,
alisema hawezi kueleza chochote kuhusiana na jambo hilo kwa kuwa
anaamini itasababisha tafsiri tofauti kuhusiana na jambo hilo, ambalo
limeonekana kuleta mambo mengi kuhusiana na swali hilo.
No comments:
Post a Comment