- Ni na NGOME YA WANAWAKE YA CHAMA CHA ACT WAZALENDO
- Ni kutokana na Matusi aliyoyaporomosha Mkutanoni dhidi ya Afisa Ardhi
- Yawataka Watetezi wa wanawake wasimame kidete kutetea wanawake wenzao
Na. Mwandishi wetu
Ngome ya Wanawake ya chama cha ACT WAZALENDO imemshtaki mkuu wa mkoa wa Dar es salaam Mheshimiwa Paul Makonda kwa kitendo chake cha kumuita mtumishi wa halimashauri ya kinondoni kichaa hadharani.
taarifa ilisosambazwa na Afisa habari wa chama hicho Abdallah Khamisi iliyosainiwa na Katibu wa Taifa wa Ngome hiyo ya wanawake ya ACT wazando Bi. Ester Kyamba, inasema kuwa ngome yao imesikitishwa, kufedheheshwa na kuudhunishwa na kauli hiyo isiyo ya kiungwana na isiyoendana na maadili ya watanzania na utanzania.
zaidi, tafadhali karibu uipitie taarifa yao.
NGOME YA WANAKE - ACT WAZALENDO.
TAARIFA KWA UMMA
---------------------------------------------------------------------------------------------------
---------------------------------------------------------------------------------------------------
Ngome ya Wanawake ya Chama cha ACT Wazalendo imeshtushwa na
kuhuzunishwa na kauli zisizo za kiuongozi na zisizozingatia kanuni za
Maadili ya Utumishi wa Umma zinazoendelea kutolewa na Mkuu wa Mkoa wa
Dar es Salaam Paul Makonda.
Jana, katika mkutano anaouita wa kutatua kero, Bwana
Makonda ameendelea kushindwa kutatua kero na badala yake kuongeza kero
ya kudhihaki, kukejeli na kutukana hadharani wananchi anaowaongoza na
watumishi anaowasimamia kitendo ambacho ni kinyume na maadili ya
Watanzania.
Kitendo cha Mkuu wa Mkoa Makonda akiwa katika eneo la
Mabwepande, Wilaya ya Kinondoni Mkoani Dar es Salaam kumtolea lugha ya
udhalilishaji Afisa Ardhi wa Manispaa ya Kinondoni Bi Rehema Mwinuka kwa
kumtamkia kuwa; "Hawa ndio vichaa tunaohangaika nao, toka hapa".
kimetusikitisha Sana na tunakilaani kwa nguvu zetu zote.
Kauli kama hii sio tu haikupaswa kutolewa na kiongozi
mkubwa katika ngazi ya Mkoa lakini pia ni kauli mbaya ambayo ililenga
kumdhalilisha na kumvunjia heshima yake mbele ya umma Bi Rehema Mwinuka.
Ngome ya Wanawake ACT Wazalendo, Leo tarehe 29.11.2016
imepeleka mashtaka rasmi dhidi ya Mkuu wa Mkoa huyo mbele ya Tume ya
maadili ya viongozi wa umma na utawala bora kuwataka wamuwajibishe kwa
kitendo chake hicho cha utovu wa maadili.
Ngome ya Wanawake ACT Wazalendo inamtaka pia Mkuu wa Mkoa
wa Dar es Salaam atambue kuwa kwa kuzingatia Sheria ya Utumishi wa Umma
ya mwaka 2002 pamoja na Kanuni za Maadili ya Utumishi wa Umma, kanuni ya
65(1) inamtaka mtumishi wa umma;
_"kuepuka kufanya vitendo viovu au kutamka maneno
yanayolenga kuwaaibisha watumishi wa ngazi moja, za chini yao au wa vyeo
vya juu"._
Alichofanya Mkuu wa Mkoa ni kumuaibisha na kumtolea lugha
ya udhalilishaji Bi Rehema Mwinuka kinyume cha Sheria na Kanuni za
Utendaji katika Utumishi wa Umma.
Ngome ya Wanawake ACT Wazalendo inaitaka Tume ya Maadili na
Utawala Bora ifanye uchunguzi na kuchukua hatua dhidi ya matamshi
mbalimbali yaliyotolewa na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam ambayo
yalikiuka sheria ya Maadili ya Utendaji katika Utumishi wa Umma.
Ngome ya Wanawake ACT Wazalendo inayataka pia Mashirika na
Asasi mbalimbali zinazosimamia Haki za Binaadamu, Haki za Jinsia na
Utawala Bora kupaza sauti dhidi ya kauli isiyo ya kiuongozi iliyotolewa
na Mkuu wa Mkoa dhidi ya Afisa Ardhi wa Manispaa ya Kinondoni Bi Rehema
Mwinuka.
Kadhalika, Ngome na Chama kwa ujumla tutaendelea kuwasemea wanyonge wote popote walipo kwa kadri ya uwezo wetu.
Imetolewa na:
Esther Kyamba,
Katibu,
Ngome ya Wanawake
Katibu,
Ngome ya Wanawake
ACT Wazalendo
Ester Kyamba Katibu Ngome ya wanawake ACT WAZALENDO
.
No comments:
Post a Comment