WADHAMINI WETU

WADHAMINI WETU

Tuesday, November 15, 2016

MEYA MAREKANI AMFANANISHA MICHELLE OBAMA NA SOKWE

Chapisho linalomfananisha bi Obama na 'sokwe' lazua hisia.

 Bi Michelle ObamaBi Michelle Obama.

Chapisho la kibaguzi kuhusu mke wa rais wa Marekani Michelle Obama limezua utata unaomuhusu meya wa jimbo la Virginia.
Pamela Ramsey Taylor ,ambaye anaendesha shirika moja la kihisani katika kaunti ya Clay, alimfananisha Michelle Obama na 'sokwe' .
''Itakuwa vyema kuwa na mtu anayefuata mitindo,mrembo na mke wa kwanza mwenye heshima.Nimechoka kuona sokwe lililovaa viatu'',alisema.
Meya mwengine kutoka eneo hilo Beverly Whaling alijibu kwa kusema ''umeifanya siku yangu nzuri''.

Chapisho la facebook lililomuhusicha bi Obama na sokwe

Bi Beverly Whaling ni meya wa mji wa Clay ambao una idadi ya takriban watu 491.
Mji huo hauna wakaazi wa Marekani wenye asili ya Kiafrika,kulingana na idadi ya watu iliotolewa 2010.
Katika kaunti ya Clay zaidi ya asilimia 98 ya wakaazi 9,000 ni watu weupe.

Licha ya idadi hiyo ndogo katika jimbo hilo ,chapisho hilo la facebook lilisambaa nchini Marekani na katika vyombo vya habari vya kimataifa huku ombi la kuwataka wanawake wote wawili kufutwa kazi likikusanya saini 85,000.

Bi Obama akiwa pamoja na mke wa rais mteule wa Marekani Melania TrumpBi Obama akiwa pamoja na mke wa rais mteule wa Marekani Melania Trump

BBC SAWAHILI. 

No comments:

Post a Comment