Wakati Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na
Watoto, Dkt. Hamisi Kigwangalla, akiendelea na usimamizi wa Operesheni
Maalum ya kufuatilia na kuufumua mtandao wa Viroba na Pombe feki na
haramu nchini. Mchana wa jana amelazimika kukifunga kiwanda cha Afro
American kinachozalisha viroba aina ya Zed, Dollars na vinginevyo
ambavyo vimekutwa havina vibali vya TFDA na havina usajili wa TFDA,
havina Batch Number ya kutambua uhalali wa uzalishaji wake, havina
tarehe ya kuzalishwa na wala ya ku-expire.
Hivyo ni ngumu kutambua ubora
wake na idadi yake halisi kwa maksudi ya kulipa kodi ya serikali.
Wenye
kiwanda hawatunzi rekodi za uzalishaji na wamekiri kuwa mitambo yao
haina uwezo wa kuweka batch number. Jana akiendesha operesheni hii
maalum, Dkt. Kigwangalla alibaini uwepo wa bidhaa hizi sokoni na hivyo
aliagiza wataalamu wafuatilie kinyume nyume kujua zinakotoka. Upelelezi
umewafikisha hapa.
''Hivi viroba hauzi Dar kabisa. Anapeleka Mbeya Na Tunduma tu! Kila siku usiku wa manane anasafirisha gari mbili za tani 10 kila moja''. amesema msiri wetu
No comments:
Post a Comment