Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika
Mashariki, Mhe. Dkt. Susan Kolimba, ambaye yuko Nairobi kuhudhuria kikao
cha Bunge la Afrika Mashariki, ametumia fursa hiyo kutembelea Ubalozi
wa Tanzania nchini Kenya na kuzungumza na watumishi.Katika
kikao na Mhe. Waziri, watumishi wa Ubalozi walielezea changamoto
mbalimbali wanazokabiliana nazo katika utendaji wa kazi, ikiwa ni pamoja
na ufinyu wa bajeti.
Hata
hivyo watumishi hao walisema wameweza kukusanya maduhuli ya kuridhisha
na kuhudumia Watanzania wanaopatwa na matatizo kwa kuchangishana wakati
mwingine.Mhe. Kolimba alieleza kuridhishwa kwake na utendaji wa watumishi wa Ubalozi wa Nairobi na kuwapongeza kwa moyo wa kujitolea.
Alisema
Serikali itajitahidi kupatia balozi fedha na vifaa vya kazi kwa kadri
ya uwezo wake, lakini akasisitiza watumishi wawe wabunifu na wajitolee
kufidia pale upungufu unapojitokeza.Kikao cha Bunge la Afrika Mashariki kinachofanyika kwenye Bunge la Kenya kinatarajiwa kumalizika kesho.
Baadhi ya watumishi wa Ubalozi wakijipanga kumpokea Mhe. Naibu Waziri
Mhe. Kolimba akisalimiana na baadhi ya watumishi wa Ubalozi.
Naibu
Waziri, Dkt. Kolimba (kushoto) akifurahia bidhaa za Tanzania kwenye
ofisi za Ubalozi wa Nairobi akiwa na Kaimu Balozi, Bi. Talha Mohamed
Waziri.
Naibu
Waziri akiongea na watumishi wa Ubalozi. Kushoto ni Kaimu Balozi, Bi.
Waziri na Mkurugenzi wa Sera na Mipango wa Wizara ya Mambo ya Nje na
Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Bw. James Lugaganya.
No comments:
Post a Comment