Rais Ali Hassan Mwinyi katika picha ya pamoja na kamati ya Saidi
Taifa Stars Ishinde aliyoikaribisha Ikulu jijini Dar es salaam kwa kazi
nzuri waliyofanya ya kuwezesha Taifa Stars kunyakua ubingwa wa Challenge
Cup ya Afrika Mashariki mwaka 1994. Toka wakati huo Tanzania
haijashinda tena kombe hilo.
Waliosimama mbele toka
kulia ni Ankal, Brigedia Moses Nnauye, Mwenyekiti wa chama cha soka
(FAT) Alhaj Muhidin Ndolanga, Mhe. Rais, Profesa Philemon Sarungi
(wakati huo waziri wa afya), Mwenyekiti wa kamati Mzee Reginald Mengi,
Mbunge wa Dodoma Mhe. Kuwayawaya S. Kuwayawaya, na mwanahabari Richard
Mwaikenda.
Nyuma kutoka kulia ni Joseph Senga,
Stephen Rweikiza, Deus Mhagale, Kanali Ali Mwanakatwe, Richard Ndassa,
Japhet Sanga, Godfrey Lutego, nyuma yao ni Evarist Mwitumba, James
Nhende, Meja Jenerali Makame Rashid na nyuma yake ni mwanahabari Edmund
Msangi na mwandishi jina limenitoka.
No comments:
Post a Comment