BREAKING NEWS:
WAZIRI KIGWANGALA AKAMATA VIWANDA FEKI VYA POMBE.
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na
Watoto, Mhe. Dkt. Hamisi Kigwangalla, ambaye anaongoza timu ya Serikali
yenye wataalamu na wanausalama, kusaka viroba feki na pombe nyingine
haramu, amekamata shehena kubwa ya bidhaa hizo feki na haramu kwenye
maeneo mbalimbali ikiwemo kukifuma kiwanda bubu kinachotengeneza
konyagi na Smirnoff feki maeneo ya Sinza.
Kiwanda hicho kinatengeneza vinywaji hivyo kwa kutumia
'spirit' ambayo inachanganywa na 'gongo'; spirit, gongo, chupa tupu na
zilizojazwa, vizibo, vifungashio vimekamatwa.
Polisi inawashikilia watu wawili ambao inasemekana
wanafanya kazi pamoja na bwana Yusuf Abdul Kalambo, ambaye anatafutwa na
polisi mpaka sasa.
JAMVI LA HABARI LITAWAJUZA ZAIDI.
No comments:
Post a Comment