Rais wa Jamhuri ya Tanzania amefuta
hati ya umili ardhi ya shamba kubwa lililokuwa likimilikiwa na waziri
mkuu mstaafu Frederick Sumaye kwasababu zilizoelezwa na serikali wa
mtaa kuwa liliachwa bila kuendelezwa .
Hatua hiyo imekuja baada ya
Tanzania kuzindua kampeni kubwa ya kurejesha ardhi mikononi mwa
watanzania ambayo haijaendelezwa na wawekezaji waliomilikishwa awali na
kuwapa wakulima masikini .Hata hivyo, Frederick Sumaye ambaye aliwahi kuwa waziri mkuu kwa muda wa miaka kumi kuanzia mwaka 1995 na kuamua kuhamia kambi ya upinzani baada ya uchaguzi wa Tanzania mwaka wa jana uamuzi ulioelezwa kuwa na msukumo wa kisiasa.
Sumaye alisema kama lengo la kumnyang'anya ardhi yake ni jaribio la kumlazimisha kurejea katika chama tawala, "wasahau ''.
BBC
No comments:
Post a Comment