UMENISOMESHA na hata KUNIOZESHA, niseme nini ili DUNIA ielewe kuwa kwangu ulikuwa ZAWADI kutoka kwa MUNGU?
Paul Makonda Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam

ASANTE BABA KWA KUNIFUNDISHA UONGOZI.
Siku zote umeniambia nianze na mambo MAGUMU kwanza ndiyo
nifanye mambo MEPESI,
niwe na ngozi ngumu na wala nisikate tamaa.
Hukuacha KUNIOMBEA na KUNITIA MOYO hata wakati unaumwa, hakika wewe ni
MWALIMU MWEMA ambae alama zako hazitafutika kamwe maishani mwangu.
UMENISOMESHA na hata KUNIOZESHA, niseme nini ili DUNIA ielewe kuwa kwangu ulikuwa ZAWADI kutoka kwa MUNGU?
UNYENYEKEVU, UPOLE, na UJASIRI wako ni dira tosha ya kuwatumikia Watanzania ambao mpaka sasa nina uhakika unawaombea.
Nenda Mzee Sitta acha niendeleze VIWANGO na KASI kwani ndiyo urithi ulioniachia.
Mwanao Mpendwa,Paul Makonda

marehemu Samuel Sitta
No comments:
Post a Comment