Rais anayalalamikiwa kutokufuata katiba Joseph Kabila
Ujumbe wa mabalozi 15 wa Baraza la Usalma umetembelea miji ya Goma na
Beni JUmapili baada ya kukutana na rais Joseph Kabila naviongozi wa
serikali na upinzani pamoja na viongozi wa kidini huko Kinshasa siku ya
Jumamosi.Balozi wa Ufaransa kwenye Umoja wa Mataifa Francois Delattre, anaeongoza ujumbe huo amesema, watu wanadhamira ya kupatikana suluhisho la kisiasa.
“Katika ziara hii ya tatu ninataka kueleza bila ya shaka kwamba kuna hali ya maridhiano kutaka kutafuta shuluhisho la kisiasa litakaloheshimu katiba”.
Balozi wa Angola Ismael Gaspar Martins anasema hakuna anaekubaliana suala la muhula wa tatu wa Kabila.
“Hivi sasa CENO itaongoza majadiliano kati ya pande zote zilizopo na ninadhani kutokana na utaratibu huo watafikia makubaliano juu ya mpango wa kuendelea mbele kuhakikisha utulivu nchini”.
Baada ya mazunguzmo yao na viongozi mbali mbali wa kisiasa na kidini wawakilishi wa upinzani wanasema wanataka uchaguzi upangwe katika muda wa siku 120 baada ya muda ya Kabila kumalizika. Eva Bazaiba katibu mkuu wa chama cha MLC anasema wanataka kufuata katiba.
“Tunataka kifungu cha katiba cha kuchelewesha uchaguzi kwa siku 120 kitekelezwe na hivyo lazima uchaguzi wa rais ufanyika kabla ya April 17 mwakani yani siku 120 baada ya muda wa Kabila wa Disemba 19 kumalizika. Na tumesisitiza bayana kwamba hakuna njia yeyote kwa rais anaeondoka yani Kabila kubaki Madarakani kupida muda wake halali”.
Katibu mkuu wa mungano wa serikali PPRD Henry Mova anapinga pendekezo hilo, akisema ujumbe wa Baraza la Usalama una wasi wasi.
“Wana wasi wasi kuna kundi moja la upinzani linachukua msimamo mkali, lakini tumekua tukijaribu kutuliza mambo. Kama historia inatufundisha kuna daima wale wanaotaka kujiunga mwishoni, lakini nchi hii haitowasubiri, imeshasonga mbel”.
Vyama vya upinzani vinapinga kura ya maoni juu ya kubadili katiba kukata uchaguzi kufanyika baada ya miaka miwili lakini serikali inaeleza itaendelea na makubaliano yaliyofikiwa Kinshasa.
No comments:
Post a Comment