WADHAMINI WETU

WADHAMINI WETU

Saturday, February 25, 2017

Manufaa ya kuwala wadudu kama chakula

Mwigizaji mashuhuri Angelina Jolie alizua mjadala mkali alipokuwa akivumisha filamu yake mpya nchini Cambodia alipokaanga na kuwala buibui akiwa pamoja na watoto wake.
Mwigizaji huyo alisema walikuwa na "ladha tamu sana".

Kula wadudu ni jambo lililohusishwa kwa muda mrefu na uigizaji, katika vipindi vya runinga kama vile I'm a Celebrity... Get Me Out Of Here.
Lakini je, tunafaa kuwa kama Angelina na kuanza kuwala wadudu?
Kwanini tunafaa kula wadudu? Insects on a plate
Inakadiriwa kwamba kufikia mwaka 2050, idadi ya watu duniani itafikia bilioni tisa.
Ndipo tuweze kuwalisha, itabidi uzalishaji wa chakula uongezeke maradufu.

Idadi ya watu duniani inapoopanda, kuna juhudi za kutafuta njia mbadala za kupata chakula - hasa protini - badala ya vyakula vya kawaida kutoka kwa mifugo na samaki.
Kula wadudu ni moja ya njia hizi mbadala.
Hili linasifiwa sana kwani wataalamu wanasema ni endelevu kimazingira, wana virutubisho vingi na wanaweza kupatikana kwa urahisi, kwa gharama nafuu na katika hali nzuri.
Maanufa ya kula wadudu ni gani? pizzaWadudu wanaweza kuliwa na vyakula vingine, mfano pizza.

"Wadudu ndio chakula halisi chenye virutubisho karibu vyote," anasema Shami Radia, mwanzilishi mwenza wa Grub, duka linalouza wadudu wanaoliwa.
"Wana protini, madini mengi na asidi za amino na kwa hivyo ni faida sana kuwala."
Wadudu pia huwa bora kwa mazingira ukilinganisha na ufugaji.

Wanaweza kula taka, hawatoi gesi zinazochangia ongezeko la viwango vya joto duniani, hawahitaji maji mengi na huhitaji eneo kubwa la shamba kuwafuga.
Wadudu pia wana kiwango cha juu sana cha kubadilisha mali ghafi kuwa kawi au chakula kwa sababu hawahitaji kudhibiti joto katika miili yao kwa kutumia damu kama wafanyavyo mifugo na wanyama wengi.
Kwa kawaida, wadudu wanaweza kubadilisha kilo 2 za lishe kuwa sehemu ya mdudu.
Ng'ombe atahitaji kula lishe ya kilo 8 ndipo aweze kuongeza kilo 1 katika uzani wake.

Ni wadudu wa aina gani wanaoliwa?

Kuna karibu wadudu aina 1,900 ambao wanaweza kuliwa duniani, kwa mujibu wa Shirika la Chakula Duniani (FAO).
Wengi wa wanaoliwa ni mende, viwavi, nyuki, nyigu, nzige, kumbikumbi, nge, vipepeo na kerengende.
Licha ya kwanda wadudu hawa wanapatikana kwa wingi, ni aina chache sana ya wadudu hawa wanaoliwa na jamii Afrika Mashariki.

Wabunge waidhinisha kilimo cha bangi Uholanzi

Amsterdam, NetherlandUholanzi hukuruhusu ununuzi wa vipimo vidogo vya bangi.\

 

Mswada huo ulioidhinishwa, utawakinga wakulima wa bangi ambao wanatimiza masharti fulani dhidi ya kuadhibiwa.
Mswada huo bado haujaidhinishwa kuwa sheria, kwani utahitaji pia kuungwa mkono na Bunge la Seneti.
Ununuzi wa viwango vidogo vya bangi katika 'migahawa' unakubalika nchini Uholanzi.
Hata hivyo upanzi wa mmea huo na kuuzia kwa wingi migahawa ni kinyume cha sheria.
Migahawa hiyo hulazimika sana kununua bangi kutoka kwa walanguzi.
Mswada huo wa Jumanne ulifikishwa bungeni na mbunge wa chama chenye msimamo wa kutetea uhuru wa raia cha D66, ambacho kwa muda mrefu kimetetea kuelegezwa kwa masharti kuhusu kilimo cha bangi.
Mswada huo uliungwa mkono na wabunge 77 dhidi ya 72, licha ya mwendesha mashtaka wa umma kueleza wasiwasi kwamba kuhalalisha kilimo cha bangi kutaifanya Uholanzi kukiuka sheria za kimataifa.
Wizara ya Afya pia ilikosoa mswada huo.
Hata hivyo, wengi wanasema huenda ikawa vigumu kwa mswada huo kupitishwa katika Seneti, iwapo maseneta watapiga kura kwa msingi wa vyama.
Lakini licha ya shaka kuhusu hatima ya mswada huo, wadau katika sekta ya bangi wamesema wamefurahishwa na ufanisi huo.
"Ni habari njema kwa sekta ya migahawa kani hatimaye - iwapo itapitishwa na Bunge la Seneti - itafikisha kikomo mambo mengi ambayo hatuwezi kuyafanya kwa mpangilio na kwa uwazi," Joachim Helms, mwenyekiti wa Chama cha Wamiliki wa Migahawa, aliambia shirika la habari la Associated Press.
BBC SWAHILI

 

Friday, February 17, 2017

WASSIRA, BULAYA BADO NGOMA MBICHI

Wafuasi wa Steven Wassira Waendelea Kumng'ang'ania Ester Bulaya....


Wapigakura wanne wa Jimbo la Bunda waliofungua shauri kupinga matokeo ya Uchaguzi Mkuu uliopita wameendelea kumng’ang’ania mbunge wa jimbo hilo, Ester Bulaya kwa kukata rufaa kupinga uamuzi wa Mahakama Kuu wa kutupa maombi yao.

Msajili wa Mahakama Kuu Kanda ya Mwanza, Francis Kabwe alisema jana kuwa rufaa ya wapigakura hao, Magambo Masato, Matwiga Matwiga, Janes Ezekiel na Acetic Malagila iliyosajiliwa kwa namba 199 ya mwaka 2016, itasikilizwa mfululizo kuanzia Februari 20.

Alisema rufaa hiyo itasikilizwa jijini Mwanza na jopo la majaji watatu wa Mahakama ya Rufani, Salim Mbarouk, Augustine Mwarija na Shabani Lila.

Katika maombi ya msingi waliyofungua Mahakama Kuu, wapigakura hao wanaowakilishwa na Wakili Constantine Mutalemwa, wanaiomba Mahakama kutengua ushindi wa Bulaya dhidi ya aliyekuwa mgombea wa CCM, Stephen Wasira kwa madai kuwa uchaguzi wa Oktoba 25, mwaka 2015 haukuwa huru na wa haki.

Pamoja na madai mengine, Masato na wenzake wanadai kuwa mchakato wa kampeni, upigaji kura na utangazaji wa matokeo uligubikwa na ukiukwaji wa sheria na utaratibu wa uchaguzi, vikiwamo vitendo vya rushwa, msimamizi wa uchaguzi kumnyima haki Wasira kwa kukataa ombi lake la kura kuhesabiwa upya.

Hoja nyingine ni msimamizi wa uchaguzi kutangaza matokeo bila Wasira kuwapo ukumbini na kuchanganya tarakimu za idadi ya wapigakura walioshiriki uchaguzi.

Novemba 17, mwaka jana, Jaji Noel Chocha wa Mahakama Kuu alimtangaza Bulaya kuwa mshindi halali wa uchaguzi huo baada ya kutupilia mbali maombi ya wapigakura hao.

TUNDU LISSU AMVAA MWAKYEMBE SAKATA TLS


Tokeo la picha la tundu lisu
Waziri wa Katiba na Sheria, Dkt Harrison Mwakyembe jana alisema kuwa atakifuta Chama cha Wanasheria Tanganyika (Tanganyika Law Society (TLS)) kwa madai kuwa kimesahau misingi yake na kuanza kufanya kazi kama chama cha siasa.

Waziri Mwakyembe alisema kuwa, kama wanataka kufanykazi kama chama cha siasa, basi yeye ataongea na msajili wa vyama vya siasa nchini ili cha hicho kipya kisajiliwe.

Kufuatia kauli hiyo, Mwanasheria Mkuu wa CHADEMA, Mbunge wa Singida Mashariki na mgombea Urais wa TLS, Tundu Lissu ameandika waraka huu kwenda kwa wanasheria wenzake.

Mawakili wenzangu. Mimi binafsi sijashangazwa na kauli ya Dkt. Mwakyembe kwamba ataifuta TLS kama itajiingiza katika harakati za kisiasa. Hii sio mara ya kwanza kwa viongozi wa serikali ya Tanzania kutoa vitisho vya kuifuta TLS.

Waziri Mkuu hayati Edward Sokoine aliwahi kutishia hivyo katika kilele cha vita dhidi ya wahujumu uchumi miaka ya mwanzo ya ’80. Na hata kabla ya hapo katika miaka ya ’60 na ’70 watangulizi wa Sokoine walijaribu kufanya hivyo hivyo. In fact, kuanzishwa kwa Tanzania Legal Corporation kipindi hicho kulikuwa driven in part na jitihada za kuondoa the private bar.

Vitisho dhidi ya TLS vilirudi miaka ya ’90 wakati wa Lyatonga Mrema. Kitu kimoja kiko common katika vitisho hivyo vyote. Vitisho hivi vimetolewa kila wakati TLS na private bar wanapo-assert their independence na wanapoanza kutetea utawala wa sheria na kupinga state lawlessness and impunity of the rulers.

Mawakili wakiwa kimya na TLS ikiwa mfukoni mwa serikali na wasipohoji matumizi mabaya ya madaraka basi wanakuwa darlings wa serikali.

Kuna kitu kingine ambacho ni common katika vitisho hivi. Havijawahi kufanikiwa na havitafanikiwa. Sheikh Abeid Amani Karume alipiga marufuku private legal practice mara baada ya Mapinduzi ya Zanzibar ya ’64. Tanzania ya leo sio Zanzibar ya miaka ya ’60 na ’70, hatutakubali udikteta wa aina ya Karume au wa aina nyingine yoyote kwenye Tanzania ya leo.

Inaelekea Dkt. Mwakyembe hafahamu au anajisahaulisha jinsi ambavyo TLS na mawakili binafsi walivyo embedded kwenye mfumo wetu wa kikatiba na kisheria. Simply put, ukifuta TLS maana yake ni kwamba hakuna wakili binafsi hata mmoja nchi nzima. Mfumo mzima wa kimahakama unategemea uwepo wa mawakili na kwa hiyo uwepo wa TLS. Mahakama karibu zote zitashindwa kufanya kazi kusipokuwa na mawakili binafsi. The same applies to various tribunals and other judicial and quasi judicial bodies.

Aidha, kuna taasisi nyingi zilizoundwa na Katiba yetu kama vile Judicial Service Commission na Law Reform Commission ambazo zinakuwa properly constituted kukiwa na uwakilishi wa TLS. Kuna taasisi nyingine nyingi ambazo zimeanzishwa na sheria za kawaida ambazo composition yake inakamilika kukiwa na representation ya TLS. Hiyo legal, constitutional and political upheaval itakayotokana na kufutwa kwa TLS will be unprecedented and unimaginable kwa mtu mwenye akili timamu.

Dkt. Mwakyembe ana akili timamu. He must be joking. Hawezi kufuta TLS. Anachotaka kufanya ni kuwatisha mawakili ili wachague watu wale wale wa miaka yote kuongoza TLS. Anatutisha ili tuendelee na status quo katika uongozi wa TLS. Hataki tufanye mabadiliko yanayohitajika ili TLS yetu isichukue nafasi yake stahiki katika kuamua mustakbala wa nchi yetu na wa taaluma yetu.

Nawataka viongozi na wanachama wa TLS wamkemee Dkt. Mwakyembe in the strongest possible terms. Nawataka wagombea wenzangu wa nafasi mbali mbali za uongozi katika TLS wajitokeze hadharani na kulaani kauli ya Dkt. Mwakyembe in no uncertain terms. Wakinyamaza tutawajua wako upande wa nani: status quo au mabadiliko. And I’ll ask you all to vote accordingly.

 Tundu Lissu

ZITTO KABWE NA KUFUNGIWA KWA WIMBO WA NICK MBISHI

  •   Afunguka kuhusu kufungiwa kwa wimbo ‘I’m Sorry JK’ wa Nikki Mbishi

Wimbo mpya wa rapper Nikki Mbishi, I’m Sorry JK umefungiwa.

Uamuzi huo umekuja saa chache baada ya rapper huyo kuitwa na Baraza la Sanaa la Taifa, BASATA Jumatano hii kujielezea kuhusiana na wimbo huo. Kupitia Instagram, Nikki amewaonya watu dhidi ya kuusambaza wimbo huo kwakuwa mkono wa sheria utawaangukia.

“Naomba niombe radhi kwa vyombo vyote vya habari kuwa sitoweza kuwapa ushirikiano wowote kuhusu wimbo wangu wa “I’M SORRY JK” uliositishwa na hii ni kwa usalama wao na wangu pia,” ameandika kwenye Instagram. 
“Napokea simu nyingi sana zikihitaji maelezo juu ya suala hilo ila kiukweli kwa watakaohitaji taarifa kamili wanaweza kufika ofisi za BASATA,naomba nisiwe msemaji tena juu ya jambo hili,” ameongeza.

Pia ameonya, “Kwa yeyote atakayeendelea kuusambaza au kuucheza popote pale mimi sitohusika naye maana technology iko huru popote duniani na siwezi kuzuia watu wasiupate kwa kuwa ushasambaa,hivyo chukua tahadhari ili usijikute mikononi mwa sheria. Asanteni sana,naomba msubiri ujio wangu mpya wa #SINGELI na aina nyingine za muziki kama #NAIJA #MCHIRIKU n.k.”

Mbunge wa Kigoma Mjini Zitto Kabwe ameandika kwenye Facebook:Serikali imepiga marufuku wimbo wa msanii Nikki Mbishi. Wallah nilidhani ni utani kumbe Kweli? Serikali hii inachoogopa ni nini? Dah kua uyaone.”

KAmati Kuu ya CHADEMA Yabariki Mbowe Amshitaki Makonda kwa Kumdhalilisha


Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kimesema kimejipanga na kitampatia mawakili wa chama Mwenyekiti wake, Freeman Mbowe katika hatua yake ya kumfungulia kesi ya kikatiba na ya madai Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda.

Februari 8 mwaka huu Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda, alitaja majina 65 kwa tuhuma za kujihusisha na biashara ya dawa za kulevya akiwamo Mbowe na kuwataka kuripoti Kituo Kikuu cha Polisi Dar es Salaam kwa ajili ya kuhojiwa.

Lakini siku moja baadaye Mbowe aliitisha mkutano na waandishi wa habari akiwa mjini Dodoma ambapo alieleza kutofika polisi kwa wito wa Makonda akisema hana mamlaka hiyo isipokuwa pale tu taratibu za kisheria zitakapofuatwa.

Mbowe ambaye pia ni Kiongozi wa Kambi ya Upinzani bungeni aliweka bayana nia yake ya kumfungulia mashtaka ya madai Makonda kwa kumkashifu na kumchafulia jina.

Akitoa maazimio ya kikao cha kamati ndogo ya Kamati Kuu ya Chadema jijini Dar es Salaam jana, Makamu Mwenyekiti wa chama hicho, Profesa Abdalah Safari alisema kamati hiyo inaunga mkono hatua ya Mbowe kumfungulia kesi ya kikatiba Makonda.

“Katika hili tumejipanga kweli kweli…tutaungana na Mbowe katika kesi hii na tutampatia mawakili wa chama akiwamo mimi na tuko wengi,”alisema.

Profesa Safari aliwataka wote ambao walitajwa na wanaamini kuwa walionewa kujihusisha na biashara au utumiaji wa dawa za kulevya wafungue mashauri mahakamani.

 “Tunatoa wito kwa wale wengine wote ambao walitajwa na wanaamini kuwa walionewa, kuchafuliwa majina na au kudhalilishwa wafungue mashauri mahakamani, kwani hii ndio njia pekee ya kuzuia wengine wasifanyiwe uonevu kama huu siku zijazo,”alisema Profesa Safari.

Pamoja na mambo mengine, Profesa Safari alisema tangu kumalizika kwa Uchaguzi Mkuu 2015 viongozi na wanachama wa Chadema wamekuwa wakikamatwa na kushtakiwa kwa makosa ya kubambikiziwa kwa kisingizio cha uchochezi.

Alisema mpaka sasa jumla ya wanachama na viongozi 215 wamefunguliwa kesi zaidi ya 78 nchi nzima.

“Kati ya hao wengi wao wamenyimwa dhamana bila sababu za msingi huku wale ambao walipatikana na hatia walipewa adhabu za vifungo bila kupewa fursa ya faini.

“Kutokana na hilo, hivi sasa tunaandaa orodha kamili itakayoainisha kesi zote za jinai ambazo ziko mahakamani na kuonyesha aina ya mashtaka na vifungo vilivyotolewa ambayo itawekwa wazi kwa vyombo vya habari na taasisi za ndani na nje ya nchi kuthibitisha kuwa kuna mpango wa kuwafunga viongozi wa upinzani kwa kusudi ili kuwadhoofisha,”alisema Profesa Safari.

Katika hatua nyingine Profesa Safari aliwaomba marais wastaafu, mawaziri wakuu wastaafu na majaji wastaafu kuzungumza na Rais John Magufuli kutokana na yanayoendelea na kwamba wasiogope kwani wao hawatatumbuliwa.

 “Marais wastaafu Ali Hassani Mwinyi, Benjamin Mkapa na Jakaya Kikwete wanaogopa nini? Kwanini wasimwambie Rais Magufuli kuwa na wao waliapa kuilinda Katiba ya nchi hivyo na yeye afanye hivyo.

“Mawaziri wakuu wako wapi? Cleopa Msuya, Jaji Joseph Warioba, Dk. Salim Ahmed Salim huyu amekuwa kimya kabisa na alikuwa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa (UN), Majaji wastaafu nao wako kimya. Tunaomba waache uoga wajitokeze wao hawatatumbuliwa,”alisema Profesa Safari

TRA Yakusanya Sh Trilioni 8.4 Kwa Miezi Sita


Mamlaka  ya Mapato Tanzania (TRA), imekusanya Sh trilioni 8.41 kuanzia Julai mwaka jana hadi Januari mwaka huu.

Taarifa iliyotolewa kwa vyombo vya habari jana na Mkurugenzi wa Huduma na Elimu kwa Mlipakodi, Richard Kayombo, inaonesha makusanyo ya Januari mwaka huu ni Sh trilioni 1.14.

Kayombo alisema pamoja na juhudi za kukusanya kodi mbalimbali, hivi sasa wameelekeza nguvu katika kukusanya kodi ya majengo kwa kutoa ankara kwa wamiliki wa majengo katika mikoa mbalimbali.

“Wamiliki wa majengo wanakumbushwa kwamba kodi ya majengo inakusanywa na TRA kuanzia Julai mwaka jana, hivyo tunawaomba watoe ushirikiano kwa kulipia ankara zao kwa wakati,” alisema Kayombo.

Kuhusu zoezi la uhakiki wa Namba ya Mlipakodi (TIN), alisema kuna mafanikio makubwa na kwamba wananchi wa mikoa ya Arusha, Mwanza, Kilimanjaro, Dodoma, Mbeya, Morogoro, Tanga na Pwani waitikie wito huo mapema kuepuka usumbufu.

Tuesday, February 14, 2017

GENERALI ULIMWENGU NA DAWA ZA KULEVYA


DW wanaripoti kuwa

Vita dhidi ya madawa ya kulevya Tanzania vitaishia wapi?

Wakati Tanzania ikionekana iko kwenye vita vikubwa dhidi ya madawa ya kulevya, mwandishi wa habari mkongwe nchini Tanzania, Jenerali Ulimwengu, anasema hakuna jipya la kuwashangaza watu 
fungua link hiyo hapo chini kufuatilia

http://dw.com/p/2XUel

Balozi wa Kenya nchini Tanzania Chirau Mwakwere ajiuzulu

http://ichef-1.bbci.co.uk/news/660/cpsprodpb/16988/production/_94625529_97cddfec-0537-41df-8a6b-af4247ecf14f.jpgRais mstaafu wa Tanzania Jakaya Mrisho Kikwete na Bw Chirau Ali Mwakwere Februari 2015. 


Balozi wa Kenya nchini Tanzania Chirau Ali Mwakwere amejiuzulu.
Bw Mwakwere, ambaye amekuwa balozi wa Kenya katika nchi hiyo jirani tangu mwanzoni mwa mwaka 2015, alijiuzulu rasmi Ijumaa kumuwezesha kuwania katika uchaguzi mkuu utakaofanyika Agosti mwaka huu.

Watumishi wa umma kikatiba wanafaa kujiuzulu kufikia 15 Februari.
Bw Mwakwere, ambaye mwishoni mwa wiki alitangaza rasmi kuhamia chama cha upinzani cha ODM, alikuwa awali mwanachama wa chama cha URP, moja ya vyama vilivyounda muungano wa Jubilee ulioshinda uchaguzi mkuu mwaka 2013.
Aliwania wadhifa wa seneta katika uchaguzi huo lakini akashindwa na Boy Juma Boy wa chama cha ODM.

Bw Mwakwere ni miongoni mwa waliotangaza nia ya kuwania wadhifa wa ugavana katika kaunti ya Kwale, baada ya gavana wa sasa Salim Mvurya kuhama chama cha ODM na kujiunga na chama Jubilee chake Rais Uhuru Kenyatta na Naibu Rais William Ruto.
"Nimekuwa balozi, wadhifa muhimu sana wa kutumikia maslahi ya wananchi wa Kenya katika ngazi ya kibalozi. Kazi yangu sasa ni kuimarisha hali ya maisha ya watu wa Kwale," alisema Jumapili, kwa mujibu wa gazeti la Daily Nation la Kenya.

"Ninataka kuweka mambo wazi, nimejiondoa chama cha Jubilee na sasa niko na watu wangu katika National Super Alliance (muungano wa wagombea wa upinzani."
Mwakwere, 71, alihudumu kama waziri wa mambo ya nje wa Kenya kati ya 2004 na 2005 na baadaye akateuliwa waziri wa uchukuzi Desemba 2005.

Alipoteza wadhifa wake wa uwaziri Februari 2010 baada ya kushindwa katika kesi ya kupinga kuchaguliwa kwake kama mbunge wa Matuga lakini alishinda uchaguzi wa marudio baadaye mwaka huo dhidi ya mpinzani wake Hassan Mwanyoha.

ZUMA NA BUHARI, MARAIS WA KWANZA WA AFRIKA WALIOZUNGUMZA NA TRUMPAT

Donald TrumpDonald Trump

Rais wa Nigeria Muhammadu Buhari leo hii akiwa mjini London amezungumza kwa njia ya simu na Rais wa Marekani Donald Trump, kufuatia ombi kutoka kwa rais huyo wa Marekani.

Wakati wa mazungumzo hayo, Rais Buhari ambaye yuko mjini London kwa ajili ya matibabu, alimpongeza Trump kwa kuchaguliwa kuwa rais wa Marekani.

Viongozi hao wawili walizungumzia njia za kuboresha ushirikiano katika vita dhidi ya ugaidi.
Trump alimshauri Rais Buhari kuendelea na kazi nzuri anayoifanya na pia kumpongeza kwa jitihada alizofanya za kuokoa wasichana 24 wa Chibok na hatua zinazopigwa na jeshi la Nigeria.

Trump alimhakikishia rais huyo wa Nigeria kuwa Marekani iko tayari kuafikiana na Nigeria kuhusu suala la kuisaidia na silaha ili iweze kukabiliana na ugaidi.Rais Trump pia amemualika Buhari kwa ziara nchini Marekani.BuhariBuhari
Baadaye Trump pia alifanya mazungumzo ya simu na rais wa Afrika Kusini Jacob Zuma. Viongozi hao walikubaliana kufanya jitihada za kuboresha zaidi ushirikiano mzuri uliopo kati ya mataifa hayo mawili.
Zuma alimpongeza Trump kwa kuchaguliwa kuwa rais wa 45 wa Marekani.
Kunazo kampuni 600 za kimarekanai nchini Afrika Kusini na pia ushirikiano mzuri wa kibiashara kati ya mataifa hayo.
Marais hao pia walijadili umuhimu wa kufanya kazi kwa pamoja katika masuala kadha ya kuhakikisha kuwepo amani barani la Afrika.Jacob ZumaJacob Zuma

Mshauri wa Donald Trump kuhusu usalama Michael Flynn ajiuzulu

Michael Flynn (kati).Bw Flynn (kati) anadaiwa kuwasiliana na balozi wa Urusi Marekani kabla ya kuteuliwa rasmi.

Mshauri mkuu wa ikulu ya White House kuhusu usalama wa taifa Michael Flynn amejiuzulu kuhusiana na uhusiano wake na maafisa wa Urusi, vyombo vya habari Marekani vinaripoti.
Bw Flynn anadaiwa kujadili vikwazo vya Marekani dhidi ya Urusi akiwa na balozi wa Urusi kabla ya Rais Donald Trump kuingia madarakani.

Anadaiwa kuwapotosha maafisa wa utawala huo mpya kuhusu mazungumzo yake na balozi huyo.
Awali, vyombo vya habari Marekani viliripoti kwamba Wizara ya Haki ilitahadharisha ikulu ya White House mapema kuhusu mawasiliano ya Flynn na maafisa wa Urusi mwishoni mwa mwezi uliopita.
Walisema Bw Flynn huenda akashurutishwa kuwa kibaraka wa urusiMaafisa wakuu wa chama cha Democratic walikuwa wametoa wito kwa Bw Flynn kuachishwa kazi.
Mashirika ya habari ya Associated Press na Washington Post yanasema wizara ya haki Marekani ilitahadharisha kuhusu kile ilichosema ni mambo aliyoyasema Bw Flynn kuhusu mazungumzo yake na balozi wa Urusi.
Ni kinyume cha sheria kwa raia wa kawaida kujihusisha na shughuli za kidiplomasia Marekani.
Mazungumzo kati ya Flynn na balozi wa Urusi yanadaiwa kufanyika mwishoni mwa mwaka jana, kabla ya Bw Flynn kuteuliwa kuhudumu katika uatawala wa Bw Trump.
Bw Flynn, ni luteni jenerali mstaafu.
Awali alikana kuzungumza kuhusu vikwazo dhidi ya Urusi na balozi huyo, na Makamu wa Rais Mike Pence pia alijitokeza hadharani kumtetea.Michael Flynn (L) and Jared Kushner at the White House on 13 February 2017Taarifa zinasema mkwe wa Bw Trump, Jared Kushner, (kulia) tayari anatafuta mtu wa kujaza nafasi ya Michael Flynn (kushoto).
Bw Flynn baadaye aliambia maafisa wa White House kwamba kuna uwezekano yeye na balozi huyo walizungumzia vikwazo hivyo.

Gazeti la Washington Post lilisema Kaimu Mwanasheria Mkuu Sally Yates aliambia White House kwamba mshauri wao mkuu wa usalama wa taifa "alijiweka katika hali ya hatari" kwa kuzungumza na Warusi kabla yake kuruhusiwa kisheria kufanya hivyo na kwamba Wizara ya Haki ilifahamu kwamba alimpotosha Bw Pence.

Mwezi uliopita, Bi Yates alifutwa kazi na Bw Trump kwa kukataa kutetea marufuku yake dhidi ya raia wa mataifa saba yenye Waislamu wengi kuruhusiwa kuingia Marekani.
 Bw Flynn alipigwa picha na kiongozi wa Urusi Vladimir Putin Decemba 2015Bw Flynn alipigwa picha na kiongozi wa Urusi Vladimir Putin Decemba 2015

Monday, February 13, 2017

UBUNGE BUNGE LA AFRIKA MASHARIKI: WATANZANIA WATAKIWA KUTOA MAONI

Wananchi mbali mbali wanashauriwa kuanza kutoa maoni yao juu ya nani na nani wanastahili kuwa wabunge wa Bunge la Africa Mashariki bunge ambalo uchaguzi wake unatarajiwa kufanyika mwezi april mwaka huu katika kikao cha bunge la bajeti kutokana na kanuni za bunge hilo linalowataka wabunge wake kupatikana kwa kupigiwa kura na wabunge wa nchi wanachama.

kwa mtazamo wako nani anastahili kuwa mbunge na nani hastahili?, ili kutoa maoni yako hayo juu ya  mtu unayetaka au unayehisi anastahili kuwa mbunge wa Bunge lijalo la Afrika mashariki tafadhali Tuma email yako katika anuani yetu ya EMAIL: jamvilahabari@gmail.com
nasisi tutakusanya matokeo yote na kuyatoa kwa umma.

MEYA UBUNGO AMVAA RAIS MAGUFULI SAKATA LA UDA



''kama mradi wa UDA ni mradi halali, sasa ilikuwaje wabunge na madiwani wahongwe pesa ili kuuhalalisha(kukubali matumizi ya billion 5.8), unawezaje kuhonga ili upokelewe fedha zako ulizonunulia kitu halali mpaka vyombo vya habari vinaandika?''.........

 

·         Amshangaa kupinga Rushwa lakini anabariki UFISADI UDA
·         Asisitiza  Rais Kapotoshwa Makusudi
·         Amtaka Kujitafakari
Na mwandidhi wetu -  JAMVI LA HABARI
Wakati kukiwa na taarifa kadha wa kadha mkanganyiko juu ya hatma ya Sakata la UDA kuelekea kutekelezwa kwa agizo la Rais Dkt John Pombe Magufuli la kulitaka Jiji la Dar es salaam Kukutana haraka na kupanga matumizi ya mgao wao wa shilingi bilioni 5.8 kama malipo ya mauzo ya Hisa zao asilimia 51 ambazo jiji lilikuwa linazimiliki.

Kumekuwepo na taarifa za uhakika zinazosema kwamba mwenyekiti wa chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA mheshimiwa Freeman Mbowe kuunda kamati maalum ya wataalam wa chama hicho kupitia na kuhakiki mchakato mzima wa uuzwaji wa hisa hizo na ushiriki wa madiwani na wabunge wake katika kile kinachoitwa kupokea rushwa ya kati ya shilingi milioni moja mpaka tano ili kubariki uuzwaji huo.

Mmoja wa wajumbe wa baraza hilo la jiji ambaye pia ni mstahiki meya wa manispaa ya Ubungo Boniface Jacob ameonyesha masikitiko yake namna Rais Magufuli alivyopotoshwa juu ya jambo hilo na kwamba namna alivyohutubia siku ya uzinduzi wa mradi ule hakika Rais ametumika kuhalalisha moja kati ya UFISADI mkubwa kuwahi kutokea katika historia ya taifa letu.

Akizungumza na JAMVI LA HABARI mstahiki Boniface Jacob amesema kuwa haelewi na kwanini Rais Magufuli ameamua kupingana na msimamo, tabia na utambulisho wake mbele ya jamii wa kuwa mpinga Ubadhilifu na mkataa rushwa  huku akitajitanabaisha kama mtetezi wa rasilimali wa Taifa.

‘’ukimsikiliza Rais Magufuli utaona namna gani ambavyo anatamani kuwa katika jumuiya ambayo haina ujanja ujanja, Rushwa , Ubadhilifu na Ufisadi wa aina yoyote, na ndio maana hakuna anayepingana naye kwenye hilo, lakini ukiangalia namna alivyo li-adress suala la UDA unaweza ukajiuliza mara mbilimbili ni Magufuli huyu huyu au mwengine’’. Alisema Mstahiki Boniface
‘’Watanzania wanaomuamini Rais Magufuli sidhani kama wanafahamu Rais wao ametumika Kubariki mradi wa Kifisadi namna hii, Rais amezungukwa na wajanja wachache waliogawana mali za masikini wa Tanzania waishio DSM, (Shirika la UDA), na sasa wanafaidi mali hizo huku waliotoka jasho kuzitafuta wakiendelea kubaki masikini’’. Aliongeza Meya Jacob

Kadharika Meya Jacob alisema kuwa haingii akilini kuwepo kwa taarifa za rushwa na kuhongwa kwa wabunge na madiwani wa vyama vyote vinavyoongoza jiji hilo ili kupitisha mradi huo na wao chadema kuchukua hatua huku chama kinachoongozwa naye Rais kikiendelea kuvuta miguu.
‘’sisi tulipozipata taarifa za kutolewa Rushwa kwa wajumbe wetu, mara moja chama kimeanzisha uchunguzi wa ndani na kamati ya wataalam imeundwa na mwenyekiti wa chama, sasa tunashindwa kuelewa mpaka sasa Rais na mwenyekiti wa CCM amechukua hatua gani’’. Aliongeza

‘’hivi nikuulize swali, kama mradi wa UDA ni mradi halali, sasa ilikuwaje wabunge na madiwani wahongwe pesa ili kuuhalalisha(kukubali matumizi ya billion 5.8), unawezaje kuhonga ili upokelewe fedha zako ulizonunulia kitu halali mpaka vyombo vya habari vinaandika?, maana yake hapo kuna walakini na siamini kama Magufuli aliyejipambanua mpiga madili dili hili halioni’’. Alisema Diwani huyo machachari wa kata ya Ubungo

Alipoulizwa juu ya thamani halisi ya shirika hilo la UDA alisema kuwa anaendelea kujumlisha mali halisi za shirika hilo na kuzitathmini na kesho atatoa taarifa kwa umma inayoonyesha mali halali za shirika hilo na thamani yake ambapo kwa kifupi anasema mali hizo ni zaidi ya mara hamsini mbele ya fedha ambazo Simon Group wamenunulia shirika hilo.

Thursday, February 9, 2017

ZUMA ATUMA VIKOSI VYA JESHI KULINDA BUNGE

Rais wa Afrika Kusini Jacob Zuma, atatoa hotuba kwa taifa leo AlhamisiRais wa Afrika Kusini Jacob Zuma, atatoa hotuba kwa taifa leo Alhamis

Rais wa Afrika Kusini Jacob Zuma, ameamrisha vikosi vya kijeshi vipatavyo 440, kutoa usalama katika majengo ya bunge, wakati atakapokuwa akilihutubia taifa leo Alhamisi.
Vyama vya upinzani vimelaani hatua hiyo na kusema hiyo ni "kutangaza vita".

Hotuba za hapo awali za Bw Zuma, zilikumbwa na maandamano na fujo, huku wabunge wa upinzani wakitoa wito wa kujiuzulu kwake.
Kwa muongo mmoja uliopita, Bw Zuma amekuwa akiandamwa na madai ya kashfa ya ufisadi.
Taarifa kutoka kwa Ofisi ya rais na iliyotolewa siku ya Jumanne, inasema kuwa Bw Zuma aliamrisha kutumwa kwa vikosi hivyo vya wanajeshi, ili kushirikiana na maafisa wa polisi kutoa ulinzi.
Hii ni mara ya kwanza kwa wanajeshi wa nchi hiyo, kudumisha usalama, badala ya kuhusika katika sherehe.
Kwa mujibu wa taarifa zilizochapishwa katika vyombo vya habari nchini humo, duru za kiusalama zimeonya kuwa kutatokea maandamano makubwa katika hafla hiyo.
Duru hizo zilisababisha hofu, kwamba huenda polisi wakashindwa kukabiliana nayo.
Hotuba za awali za kitaifa, zilikumbwa na fujo ndani ya bunge.
Tangu waliposhinda viti katika uchaguzi mkuu mwaka 2014, wanachama wa chama cha Economic Freedom Fighters (EFF), wamekuwa wakitatiza hotuba ya rais Zuma na vikao vingi vya bunge kwa kupiga kelele na kumfokea hadharani rais kuhusiana na madai hayo ya kashfa ya ufisadi.Wanachama wa chama cha EFFwwakikabiliana na walinda usalama wakati wa hotuba ya Rais mwaka 2015
 Wanachama wa chama cha EFFwwakikabiliana na walinda usalama wakati wa hotuba ya Rais mwaka 2015.

Mnamo mwaka 2015, wanachama hao wa EFF waliondolewa katika ukumbi wa bunge na walinda usalama waliokuwa wakijifanya kama wahudumu wa Bunge.
Lakini chama kikuu cha upinzani cha Democratic Alliance (DA) kimelaani vikali hatua hiyo ya Rais, na kueleza kuwa ni "ya kutamausha mno".
"Matamshi ya mara kwa mara ya Rais Zuma 'kudumisha sheria na usalama' kwenye taarifa yake, yanaashiria matumizi mabaya ya vikosi vya jeshi nje ya majukumu yao ya kuhusika katika sherehe za kitaifa ndani ya nchi," tkulingana na chama cha DA imesema.

Wednesday, February 8, 2017

BAADA YA SOMALIA KUPATA RAIS MPYA: Mambo usiojua kuhusu rais mpya wa Somalia

Rais mpya wa Somalia Mohamed Abdullahi MohammedRais mpya wa Somalia Mohamed Abdullahi Mohammed

 Rais mpya wa Somalia Mohamed Abdullahi Mohammed anaitwa 'Farmajo' baada ya chakula cha Kitaliano cha Jibini
Inasemekana kwamba alipenda sana kula Jibini wakati alipokuwa kijana wakati wa ukoloni wa Italiano
Ana uraia wa nchi mbili za Marekani na Somalia na anajulikana kwa kampeni yake ya kupigania haki za kibinaadamu.
Amewahi kuhudumu kwa muda mfupi kama waziri mkuu mwaka 2011 lakini akajiuzulu baada ya miezi michache kufuatia migogoro kati yake na aliyekuwa rais Sheikh Sharrif hassa.

Hakuwa maarufu na wanasiasa wengine kwa kuwa alijionyesha kuwa mtu wa watu akipanda ndege za bei ya chini wakati alipokuwa akisafiri katika mataifa ya ughaibuni.
Miongoni mwa wagombea wote 20 ndiye aliyekuwa maarufu katika mtandao wa kijamii.
Wapinzani wake walikosolewa kwa kuungwa mkono na Kenya na hata Ethiopia.
Wafuasi wake wanapinga mataifa ya kigeni kuingilia kati utawala wa Somalia na wanataka kuona mabadiliko nchini humo.

BREAKING NEWS: HII HAPA ORODHA YOTE YA MAJINA 65 YA PAUL MAKONDA KUHUSU MADAWA YA KULEVYA

 
Orodha ya majina yote 65 yaliyotamkwa leo tarehe 08.02.2017 na Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, Paul Makonda wanaojihusisha na Dawa za kulevya hii hapa.



VITA DAWA ZA KULEVYA: MAKONDA AITIKISA NCHI - MBOWE, MANJI, GWAJIMA NA AZZAN WASABABISHA GANZI



Mbabe wa Vita  kama anavyoitwa na wengi, Paul Makonda, leo tarehe 08 february 2018 amesababisha mtikisiko wa aina yake baada ya kuwatamka washukiwa wa namna moja ama nyingine wa madawa ya kulevya na kuwataka waripoti kituo kikuu cha polisi siku ya ijumaa.
miongoni mwa waliotajwa ni pamoja na Mwenyekiti wa Chadema Freeman Mbowe, Mchungaji Josephat Gwajima, Iddi Azan na Yusuph Manji ambaye ni Mwenyekiti na Mfadhili wa timu ya Yanga wakituhumiwa kuhusika na dawa za kulevya

Mkuu huyo wa mkoa wa Dar es salaam leo ameingia awamu ya pili ya kupambana na madawa ya kulevya na ametaja watu hao wanaotuhumiwa kuhusika na madawa ya kulevya kwa namna moja ama nyingine.

Makonda: ''Awamu ya pili ya kupambana na madawa ya kulevya tumeianza leo''.

Makonda: ''Nina orodha ya watu wengine ambao wanatakiwa kuripoti polisi siku ya Ijumaa''

Makonda: ''Tutapita nyumba kwa nyumba, kila nyumba inayohisiwa, tutaingia, nawashukuru wenyeviti wa mitaa''

Makonda: ''Hii vita tukishindwa, tumeshindwa wote, kuna watu wamekaa wanafikiri Makonda atashindwa''

Makonda: ''Leo nina majina 65, juzi ile walikuwa kumi na kitu, mtasikia mtikisiko kidogo. Nataka tukutane nao''.

Makonda: ''Wa kwanza ni mmiliki wa Slip Way, wenye klabu ya Yatch Klabu, Salehe wa MMI, Mwinyi Machapta''

Makonda:''Kuna dada yangu anaitwa Rose yuko China, kuna Mzee wangu anaitwa Kiboko anaishi Mbezi''

Makonda: ''Kila tunayemuita ajue tunamfahamu kuliko anavyofikiri. Kuna mtu anaitwa Hafidh anaishi Mbezi Mwisho''

Makonda: ''Kuna kaka yangu mpendwa mbunge mstaafu, Idd Azzan, naye namuhitaji''

Makonda: ''Kuna kaka yangu Aikael Mbowe Mbunge wa hai ambaye ni mkazi wa DSM, kuna Bossi Kizenga wa Bunju''

Makonda: ''Nassoro Selem wa Mabibo, kuna ndugu yangu Hussein Pamba Kali, pamoja na Mchungaji Gwajima''

Makonda: ''Pamoja na kaka yangu Yusuph Manji pia namuhitaji, Mmiliki wa Sea Clif pia namuhitaji''

Endelea kufuatilia ukurasa huu tukujuze mengi zaidihttps://i1.wp.com/www.darpost.com/wp-content/uploads/2016/04/paul-makonda.jpg?fit=1200%2C800Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Paul Makonda

Tuesday, February 7, 2017

WAANDISHI WAWILI WAKAMATWA ARUSHA

Tokeo la picha la habariTaarifa kutoka wilayani Arumeru zinasema kuwa Waandishi wa Habari wawili Bahati Chume ambaye ni mwandishi wa kujitegemea anayeandikia gazeti la Kila siku la Kampuni ya Mwananchi Communications LTD la Mwananchi na Dorine Aloyce wa Kituo cha Radio cha Sunrise Radio wamekamatwa na Jeshi la Polisi na Wanashikiliwa katika Kituo cha Polisi cha Usariver.

BREAKING NEWS: ZITTO KABWE KUKAMATWA NA POLISI DODOM

 
Tokeo la picha la zitto kabwe 
Zitto Kabwe
wakati wabunge wote wa upinzani wakisusia kuendelea na vikao vya bunge mpaka washiriki mjadala wa kukamatwa kwa mbunge wa singida mashariki Tundu Lissu ambaye pia Mnadhimu mkuu wa kambi rasmi ya upinzani Bungeni.

kiongozi wa chama cha ACT WAZALENDO, Zitto Kabwe ameutaarifu umma kwamba sasa ni zamu yake kukamatwa baada ya kujuzwa na watu wa ulinzi wa bunge kuwa anatafutwa na polisi kwa tuhuma ambazo hazijawekwa wazi.

''And today it's my turn I've been informed by parliamentary security personnel that police will arrest me for sedition details are not known''. Ameandika Zitto Kabwe katika Ukurasa wake wa mitandao ya Kijamii wa Twitter uliounganishwa moja kwa moja na Facebook.

SPIKA AKATAA TRUMP KUHUTUBIA BUNGE UINGEREZA

Spika wa bunge la Uingereza John BercowSpika wa bunge la Uingereza John Bercow.

Spika wa Bunge la Uingereza John Boscow amekosolewa kwa kupinga hatua ya rais Donald Trump kuhutubia bunge la taifa hilo wakati wa ziara yake.

Mwanachama wa chama cha kihafidhina aliambia BBC kwamba matamshi yake yamesababisha chuki huku mbunge mmoja akisema kuwa hayafai huku wengine wakidai hafai kupendelea upande mmoja.

Bw Bercow alisema pingamizi dhidi ya ''ubaguzi wa rangi na ule wa kijinsia'' zinapaswa kuangaziwa sana na wanachama wa bunge hilo.

Mbunge wa Marekani Joe Wilson alisema kuwa ni pigo kwa chama cha Trump cha Republican.
Mwandishi wa BBC wa maswala ya kisiasa Eleanor Garnier amesema kuwa ni pigo la kidiplomasia kwamba rais Trump hataruhusiwa kuhutubia bunge la nchi hiyo.Theresa May na Donald TrumpTheresa May na Donald Trump
Mwezi uliopita waziri mkuu wa Uingereza Theresa May alisema kuwa rais Trump amekubali mwaliko kutoka kwa malkia wa Uingereza kwa ziara rasmi nchini Uingereza baadaye mwaka huu.
Lakini akizungumza bungeni siku ya Jumatatu bw Bercow alisema kuwa anapinga rais Trump kuhutubia mabunge yote kama ilivyo ada na viongozi wengine wa kimataifa.

''Nahisi kwamba pingamizi yetu dhidi ya ubaguzi wa kijinsia na ue wa rangi na haua yetu ya kuunga mkono usawa na uhuru wa mahakama ni muhimu sana na yanapaswa kupewa kipaumbele na wabunge wa Uingereza'', alisema.
BBC SWAHILI
Amesema kulihutubia bunge sio haki bali ni heshima anayopewa kiongozi wa kimataifa.

BREAKING NEWS: BUNDI AZIDI KUTUA CUF HABIBU MNYAA ATIMULIWA UANACHAMA

Tokeo la picha la habib mnyaa
 Mheshimiwa Habib Mnyaa pichani
Wajumbe wote 112 wamepiga kura za ndio kuazimia kumfukuza uanachama kwa mujibu na mamlaka ya kikatiba yaliyoelezwa katika katiba ya CUF ukurasa wa 29 ibara ya 18(1)(ix) kuhusu wajibu wa Mkutano Mkuu wa Tawi kama ilivyoeleza kuwa;
 
THE CIVIC UNITED FRONT
(CUF –Chama Cha Wananchi)

TAARIFA KWA UMMA

Imetolewa leo Tarehe 7/2/2017

MOHAMED HABIBU MNYAA AFUKUZWA UANACHAMA 

Leo tarehe 7/2/2017 Mkutano Mkuu wa Tawi la Chanjaani, Jimbo la Mkoani wilaya ya Mkoani-Pemba, umefanya maamuzi ya kumfukuza uanachama wa CUF Mohamed Habibu Mnyaa  kutokana na kukiuka katiba ya chama Ibara ya 12 (6)(7)(16) kutokana na kuwa na mwenendo usiofaa wa kuwagawa wanachama, kueneza taarifa za upotoshaji dhidi ya viongozi na Chama, kufanya vitendo vya hujuma za kutaka kukidhoofisha Chama, kudharau na kushindwa kuhudhuria na kutoa ushirikiano kwa tawi lake kila alipotakiwa kufanya hivyo. Mkutano Mkuu wetu wa leo umehudhuriwa na wajumbe halali 112 kati ya wajumbe wote halali 113. 
 
Wajumbe wote 112 wamepiga kura za ndio kuazimia kumfukuza uanachama kwa mujibu na mamlaka ya kikatiba yaliyoelezwa katika katiba ya CUF ukurasa wa 29 ibara ya 18(1)(ix) kuhusu wajibu wa Mkutano Mkuu wa Tawi kama ilivyoeleza kuwa;

 “Kumchukulia hatua za nidhamu mwanachama au kiongozi yeyote wa tawi hilo, ikiwa ni pamoja na kumpa onyo, karipio, karipio kali, kumsimamisha uanachama au uongozi wa Chama kwa muda, na hata kumuachisha au kumfukuza uanachama wa Chama” 

Mohamed Habibu Mnyaa alijiunga na CUF katika tawi hilo tarehe 28 septemba mwaka 1999 na kukabidhiwa kadi yenye Namba ya usajili 029033. Mohamed ambaye amewahi kuwa Mbunge wa Jimbo la Mkanyageni kwa muda wa vipindi viwili 2005-2015, amekuwa na mwenendo huo mbaya na usiofaa kwa Chama na viongozi wake tangu alipokosa ridhaa ya wanachama na Maamuzi ya vikao vya Chama kumpitisha kugombea kwa mara nyingine tena katika nafasi ya ubunge mwezi August, mwaka 2015. Mohamed amefukuzwa uachachama akiwa ni mwanachama wa kawaida wa tawi la Chanjaani asiyekuwa na wadhifa wowote mwingine ndani ya Chama. 

Kwa mujibu wa Katiba ya CUF ibara ya 108(5) kuhusu Nidhamu ya chama na Muda wa kukata Rufaa inaeleza kuwa; 

“ Mwanachama au kiongozi yeyote aliyeamua kukata Rufaa kwa jambo lolote lile, basi atafanya hivyo kwa ngazi iliyo juu ya kikao kilichotoa maamuzi ambayo hakuridhika nayo katika kipindi kisichozidi siku kumi na nne (14) tokea siku uliotolewa uamuzi huo”  ni hiyari yake kuona kama inafaa kukitumia kifungu hiki au kutokitumia.
 
Tunatoa wito kwa wanachama wote wa tawi la Chanjaani, kuzingatia wajibu wao wa kikatiba na kuheshimu taratibu, kanuni na kulinda nidhamu na heshima ya Chama chetu ndani ya Chama na ndani ya jamii kwa ujumla. Uongozi wa tawi hautasita kutekeleza matakwa ya katiba pale itakapobainika kwa mwanachama yeyote kwenda kinyume na maamuzi na misimamo ya Chama.  

HAKI SAWA KWA WOTE

KOMBO MOHAMED MAALIM
KATIBU WA TAWI LA CHANJAANI, JIMBO LA MKOANI-PEMBA
Mawasiliano: 077 815 3414

Monday, February 6, 2017

RAMA DEE : WAUZA UNGA WANAFAHAMIKA WAKAMATWE SI WASANII

Tokeo la picha la RAMA DEEmsanii Rama Dee akiwa na Lady Jay Dee katika picha ya maktaba
 
Rama Dee ni mmoja kati ya wasanii bora wa Rnb ambaye mara nyingi amekuwa na misimamo tofauti na wasanii wengi ambao wanafanya aina hiyo ya muziki.

Katika kile ambacho kinaendelea juu ya sakata la madawa ya kulevya, Rama Dee ameingia katika kundi la wasanii wachache ambao wameweka mitazamo yao hadharani juu ya ukamataji wa wasanii na kuwekwa ndani.

Rama Dee amesema “Mimi kama msanii,Siungi mkono wasanii kuwekwa ndani Ila ninge muunga mkono Kama angeweza kuziba mirija ya Wauzaji Papa kuwafikia wasanii na watanzania kwa ujumla!

"Toka nipo mdogo wauza unga wanafahamika na majina yao yapo kwenye mitandandao lakini sijawahi ona wakikamatwa wala kuonyeshwa kwenye vyombo vya habari! Hata hao polisi pia sijaona picha zao!

"Wasanii ni watu Kama watu wengine tu…so unapo anza kuaribu biashara zao kwa sababu tu upo na power ya uongozi sidhani kama ni busara! :

"Ushauri wangu kaa na viongozi wenzio ambao walikutangulia kwenye uwongozi uliza why walishindwa then anzia hapo!

"Unajuwa haya mambo unaweza ona ya kawaida Ila yanaweza kuharibu maisha ya watu kuliko hata huwo Unga! Haswa wasanii. :

"Namuunga mkono Nape kuwa kuna njia za kutumia ambazo zinalinda sheria ya mtuhumiwa! Ila ukitumia nguvu bila Akili ni sehemu mojawapo ya kuwapatia pesa Wanasheria bila msingi wowote! :

"Kukamata watu kwa kuhisi ni utaratibu mbaya sana! Kumbuka kuna watu wapo na chuki za maendeleo ya watu wengine.Unaweza ukasikia hata Tale anauza unga ambae ni rafiki yako, sijuwi utafanyaje hapo.

"Mimi naona plan yako imeanzia sehemu si sahihi rudi nyuma Anza tena ni hayo tu, halafu hakuna movement nzuri Kama movement ya kutumia power ya wasaniii na jamii kiujumla.

"Fanya kazi yako Mh. makonda waache wasanii watafute mkate wao wa kila siku! Rama Dee!"

RAIS MAGUFULI : MKAMATENI HATA MKE WANGU AKIJIHUSISHA NA BIASHARA YA UNGA

Rais Dkt. John Pombe Magufuli

Rais Magufuli ameviagiza vyombo vya ulinzi na usalama kuwakamata wanaohusika na Dawa za Kulevya bila kuangalia umaarufu au cheo cha mtu.

Magufuli ameyasema hayo leo alipokuwa akizungumza  mara  baada ya kuwaapisha viongozi mbalimbali akiwemo Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi, Jenerali Vanance Mabeyo pamoja na viongozi wengine wa majeshi, na mabalozi.

Katika hafla hiyo iliyofanyika katika ukumbi wa Ikulu jijini Dar es Salaam, Rais Magufuli alianza kwa kumpongeza Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini (IGP), Ernest Mangu kwa hatua nzuri aliyoichukuwa ya kuwasimamisha kazi Askari Polisi 12 waliotuhumiwa kujihusisha na dawa za kulevya ili kupisha uchunguzi.

Rais Magufulia amesema hakuna wa kuachwa hata akiwa mkewe Mama Janet Magufuli, na kuongeza kuwa wakamatwe bila ya kujali majina yao.

"Najua IGP Mangu watu walikupigia simu wanakupa ushauri kuhusu Dawa za Kulevya, ungewasikiliza leo usingekuwa IGP.
"Vita ya dawa za kulevya haina cha umaarufu, haijalishi ni mtoto wa nani anahusika, hata kama ni mke wangu mkamateni.
"IGP nakuagiza kamata watuamiaji wote wa dawa za kulevya hao watakwambia wanapozipata, haiwezekani ziuzwe kama njugu."Amesema Rais Magufuli
Akizungumzia suala la uendeshaji wa kesi za dawa kulevya, Rais Dkt Magufuli amemwambia Kaimu Jaji Mkuu wa Tanzania,  Jaji Prof. Ibrahim Hamis Juma kuwa kesi hizo zinaendehswa taratibu sana huku akitolea mfano wa mfanyabiashara mmoja maarufu wa dawa za kulevya aliyekamatwa mkoani Lindi lakini hakuwahi kufikishwa mahakamani. 
"Kuna mfanyabiashara maarufu wa dawa za kulevya alikamatwa mkoani Lindi lakini sijawahi kusikia amefikishwa mahakamani" Amesema Rais Magufuli.

Rais  Magufuli amesema kuwa vita ya dawa za kulevya si ya Paul Makonda peke yake bali ni ya Watanzania wote huku akivitaka vyombo mbalimbali vya ulinzi na usalama kushirikiana kutokomeza tatizo hili linalopelekea kupoteza nguvu kubwa ya taifa.

Kauli hii ya Rais Magufuli inakuja ikiwa ni siku chache tangu Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda atangaze vita dhidi ya watu wanaohusika na dawa za kulevya akianza kwa kutaja majina yakiwemo ya askari na ya wasanii maarufu wa muziki na filamu akiwemo Wema Sepetu, Chid Benz, Vanessa Mde n.k.

Siku tatu baada ya Makonda kuwataja watuhumiwa hao, IGP Ernest Mangu alichukua hatua ya kuwasimamisha askari  12 waliotajwa na kuahidi kuchukua hatua zaidi, jambo ambalo limepongezwa na Rais Magufuli na kumueleza kuwa endapo asingechukua hatua hiyo, angejua kuwa na yeye anahusika.