WADHAMINI WETU

WADHAMINI WETU

Saturday, October 29, 2016

BREAKING NEWS : ACT WAZALENDO WALIVYOMJIBU OLE SENDEKA WA CCM. WATAKA SERIKALI IMCHUNGUZE ZITTO KABWE




 ''Sasa ni mwaka mmoja tangu
wachaguliwe, lakini hakuna madawa hospitalini, hakuna mikopo kwa Wanafunzi wa
Elimu ya Juu, hakuna ajira mpya, hakuna kupanda mishahara kwa watumishi wa
umma, hakuna hata jiwe la msingi la Kiwanda kipya lililowekwa tokea Serikali ya
awamu ya tano iapishwe, mzigo imepungua bandarini, magari makubwa ya mizigo
yameamuriwa yapaki tu kwa kuwa sekta ya Usafirishaji imeuliwa, na maisha ya
Watanzania yamezidi kuwa magumu''.



TAARIFA KWA UMMA.

CHAMA cha ACT Wazalendo kimeshtushwa na tuhuma, kashfa, porojo na matusi mbalimbali
yaliyotolewa jana na msemaji wa chama cha Mapinduzi(CCM), Ndugu Christopher Ole Sendeka dhidi ya Kiongozi wa chama chetu, ndugu Kabwe Z. Ruyagwa Zitto.

 Kutokana na hayo chama kina masuala yafuatayo ya kusema kwa wanachama wetu na umma wa Watanzania kwa ujumla:

• Chama chetu kinakaribisha uchunguzi juu ya mali na madeni ya Kiongozi wetu, ndugu Zitto. Tutafurahi uchunguzi huo ukihusisha akaunti zake za benki pamoja na mfumo wa maisha yake binafsi (LifeStyle). 
Tunavitaka vyombo vya uchunguzi vianze kazi hiyo mara moja kwani tunaamini kuwa  Kama kuna Kiongozi ambaye Mali, Madeni, Maslahi na Akaunti zake viko wazi basi ni ndugu Zitto. 
Ikumbukwe kuwa Katiba na Kanuni za chama chetu huwataka Viongozi wote wa chama kuweka hadharani tamko la mali zao na madeni, ndugu Zitto alitekeleza matakwa hayo ya kisheria, na mali pamoja na madeni yake yako hadharani na mtandaoni. Tunatambua chama tawala kinaweweseka na tunataka kiondokane na ugonjwa huo wa  kuweweseka,badala yake  wachukue hatua za uchunguzi dhidi ya ndugu Zitto.



• Ni wajibu wa Viongozi wa chama cha ACT Wazalendo kuupinga ujinga popote pale ulipo, Kiongozi wa Chama chetu, ndugu Zitto, anatekeleza wajibu huo kwa Uzalendo mkubwa kwa Taifa lake. 


Chama chetu kiko pamoja naye katika kupinga Ufisadi mkubwa wa ESCROW ambao chama tawala kimeukalia kimya, ufisadi wa Mabilioni ya HATI FUNGANI na hata sasa anapowapigania Waandishi wa Habari nchini katika Kampeni yake ya kupinga MSWADA MBAYA wa Habari. 

Tunajua kuwa kampeni hii ya kupinga Mswada mbaya wa Habari ndiyo ambayo imezua ubwatukaji huu wa msemaji wa chama tawala.

Ni muhimu Serikali na chama tawala wajue kuwa chama chetu kitaupinga mswada huo ambao utakwenda kuua tasnia ya habari nchini mpaka pale utakaporekebishwa. Porojo, kashfa na matusi havitaturudisha nyuma, tutaisimamia hoja hii mpaka mwisho.

• Tunamtaka msemaji wa chama tawala aache porojo, kashfa, vijembe na matusi. Ni muhimu ajikite katika kukishauri chama chake kutekeleza ahadi zake kwa wananchi. Sasa ni mwaka mmoja tangu wachaguliwe, lakini hakuna madawa hospitalini, hakuna mikopo kwa Wanafunzi wa Elimu ya Juu, hakuna ajira mpya, hakuna kupanda mishahara kwa watumishi wa umma, hakuna hata jiwe la msingi la Kiwanda kipya lililowekwa tokea Serikali ya awamu ya tano iapishwe, mzigo imepungua bandarini, magari makubwa ya mizigo yameamuriwa yapaki tu kwa kuwa sekta ya Usafirishaji imeuliwa, na maisha ya Watanzania yamezidi kuwa magumu.

Hayo ndiyo mambo ya msingi ya Watanzania, chama chetu kitaendelea kuisimamia serikali katika mambo hayo Bungeni kama anavyofanya mbunge na Kiongozi wetu wa Chama.
Mwisho kabisa, tunapenda kujua kama haya aliyoyasema Ole Sendeka ndiyo msimamo rasmi wa Chama chake au ni maneno yake mwenyewe,maana kama ni msimamo wa chama chake,tutakuwa na mengine ya kusema.


"Taifa Kwanza, Leo na Kesho"


Habibu Mchange
Katibu wa Bunge na Serikali za Mitaa
 ACT Wazalendo

Oktoba 29, 2016

Friday, October 28, 2016

BREAKING NEWS: DKT. KIGWANGALA AZINDUA APPLICATION YAKE


Dkt. Hamis Kigwangala
sasa unaweza kumpata kirahisi zaidi, kupata habari zake za kiserikali, za kibunge, habari za jimboni na masuala mbalimbali yanayomuhusu Naibu Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na watoto Dkt Hamisi Kigwangala kwa kutumia simu yako ya mkononi kwa kuingia ama ku download Application inayopatikana katika simu za aina zote yaani android na Iphones kwa kubonyeza hapa chini.

Kindly download Dr Hamisi Kigwangalla's Mobile App here:
https://play.google.com/store/search?q=Dr.%20Kigwangalla&hl=en




ZIARA YA MFALME WA MORROCO YAIBUA TUHUMA NZITO



 Morroco inagonjwa katika sekta zote, raia wake wanaishi katika umaskini wa kutupwa,  kimaadili imefilisika imebakia kuwa ngome ya ukahaba, ikisheheni makahaba kwa maelfu

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

MORROCO INA UPOFU WA TAREEKH YAKE NA MUSTAKBALI WAKE

Mfalme Mohammed VI wa Morroco amemaliza ziara yake rasmi nchini Tanzania.  Pamoja na mambo mengine serikali ya Rabat imeahidi kujenga Msikiti mkubwa jijini Dar es Salaam pia kujenga uwanja wa kisasa wa michezo ndani ya Dodoma.

Kwa bahati mbaya upeo wa siasa za nje za Morroco zimesheheni ufinyu, upofu na ziko mbali na tareekh yake  tukufu.

Morroco kama zilivyo nchi nyingi za ulimwengu wa Kiislamu kilichobakia kwao ni kuficha uovu na dhulma zake nyuma ya amma kujifanya kusimamia misikiti au kujenga mipya.  Katika Uislamu nafasi ya msikiti ni kuliinua juu neno la Allah Ta’ala:
﴿فِي بُيُوتٍ أَذِنَ اللَّهُ أَنْ تُرْفَعَ وَيُذْكَرَ فِيهَا اسْمُهُ يُسَبِّحُ لَهُ فِيهَا بِالْغُدُوِّ وَالآصَالِ
“Katika nyumba ambazo Allah ameamrisha zitukuzwe,na humo litajwe jina lake, wanamtakasa humo asubuhi na jioni”  (TMQ 24:36)
Basi, vipi dola ijenge msikiti ilhali inaendelea kutawala kwa ukafiri?
Jee  Mfalme Hassan II, (baba) na mtangulizi wa mfalme wa sasa hakujenga msikiti mkubwa ndani ya Casablanca  (Morroco), msikiti  wa 13 kwa ukubwa duniani, wenye mnara mrefu kuliko msikiti wowote, akawekeza kiwango  kikubwa cha rasilmali na juhudi isiyo na mithali kwa miaka saba.  Jee baada ya hapo nini kilifuatia?  Jee Morroco na ulimwengu wa Kiislamu ulikomboka na kuhuwika kutokana na mporomoko na idhilali? 
Morroco inagonjwa katika sekta zote, raia wake wanaishi katika umaskini wa kutupwa,  kimaadili imefilisika imebakia kuwa ngome ya ukahaba, ikisheheni makahaba kwa maelfu, nchi iliyowahi kuwa chem chemu ya elimu na ustaarabu, ikiwa na Chuo Kikuu kikongwe zaidi duniani, Chuo Kikuu cha Al-Qarawiyyin, lakini inashindwa hata kujiamini kutumia lugha ya kiarabu katika elimu ya juu. Huku ni kujivika udhalili kwa kiasi gani ? Bila ya kutaja kushiriki kwa serikali ya Rabat katika vita ya ugaidi (Uislamu) kwa niaba ya Marekani na mataifa ya Magharibi, vita ambavyo pia vinahatarisha maisha ya raia wake yenyewe.
Basi lini Morroco itajivua guo la upofu wa tareekh yake na tareekh ya Kiislamu kwa ujumla? Ni ardhi iliyoupokea Uislamu uliowaunganisha raia, kisha kwa uimara wa hali ya juu ikaibeba bendera ya (Uislamu) ikawa chanzo cha ukombozi kwa Waislamu na wanadamu kwa jumla. Kiasi kwamba hata wasiokuwa Waislamu walikuja kutaka msaada kutokana na dhulma na ukandamizaji wa watawala wao. Kama vile wakaazi wa Spain akiwemo mwana wa nyumba
 tukufu (nobleman Visigoth) , Julian, Count of Ceuta, walipowahamasisha Waislamu kuifungua ardhi ya Iberia (Spain na Ureno) kutokana na  madhila na dhulma za Mfalme Roderic. Miongoni mwa ushenzi wa mfalme huyo ni  kumbaka binti wa Julian.

Kwa kupitia ardhi hii, ikafunguliwa Spain chini ya Jemadari Tariq bin Ziad. Basi ukilinganisha tareekh hii  tukufu na hali ya leo, ni umbali wa mbingu na ardhi !

Lau Morroco ingeng’anga’na na tareekh yake tukufu, ingekuwa imeshakomboa kwa Uislamu ardhi zilizobakia Kusini ya mbali zaidi mwa Jangwa la Sahara, lakini wapi ! imekumbatia ubepari ulioigubika upofu wa tareekh yake tukufu, kilichobakia kwao ni kuhangaika kulinda utawala wao tete na kujaza matumbo yao. Kwa hakika, mageuzi ya kimsingi ya Kiislamu yanahitajika ili kuirejesha tena tareekh yetu.

Masoud Msellem
Mwakilishi Kwa Vyombo vya Habari
 Hizb ut Tahrir Tanzania



Press Release
Morocco Blindness of its Past and Future
King Mohammed VI of Morocco has completed his official visit to Tanzania. Among other things, Rabat has promised constructing an ultra-modern mosque in Dar es Salaam and a modern stadium in Dodoma.

Unfortunately, Rabat’s foreign policy scope has a full of shallowness, blindness distant away from her glorious history.

Morocco, like all Muslim lands, has nothing left to it except concealing its evils and injustices behind either pretending to manage or build new mosques. The role of the mosque is to elevate the word of Allah Ta'ala:
﴿فِي بُيُوتٍ أَذِنَ اللَّهُ أَنْ تُرْفَعَ وَيُذْكَرَ فِيهَا اسْمُهُ يُسَبِّحُ لَهُ فِيهَا بِالْغُدُوِّ وَالآصَالِ
“In houses which Allah has permitted to be exalted and that His name may be remembered in them; there glorify Him therein in the mornings and the evenings.” [an-Nur: 36]
Then, how can the state build the mosque while prevails in ruling by disbelief?
Didn’t King Hassan II, predecessor of the current king build a large mosque at Casablanca, the 13th largest mosque in the world, with the tallest minaret than any mosque in the world, exhausting massive resources and efforts of seven years. What came next? Did Morocco and the Muslim world revive and rise from decline and humiliation?
Morocco is suffering in all aspects, its people live below the poverty line, morally bankrupted by becoming a sexual heaven with thousands of prostitutes, a country once a cradle of knowledge and civilization having the world oldest University of Al-Qarawiyyin; does not have the confidence to use the Arabic language at University level. What sort of self-imposed humiliation is this? Not to mention Rabat’s role in the ‘war of terrorism’ on behalf of the US and Western nations, that also endangers the lives of its own citizens.
When will Morocco remove the cloak of blindness of its history, and its Islamic history in general? It is a land that accepted Islam which unified the masses, then became systematic standard-bearers and a source of redemption for Muslims and mankind. Even non-Muslims sought assistance from the oppression of their rulers. As residents of Spain including Visigoth nobleman, Julian (Count of Ceuta) encouraged Muslims to open Iberia due to the sufferings and injustice of King Roderic. Among them was Roderic’s rape of Julian’s daughter.
Through this land, Spain was opened under Tariq bin Ziad. In contrast this glorious history, and today’s situation, is far between the earth and heaven!

Should Morocco stick with its glorious history, it should have liberated the rest of far South Saharan Desert by Islam, instead it embraced capitalism that blindfolded it from its glorious history, rushing only to safeguard their fragile rule and filling their stomachs. Obviously, radical Islamic change is needed to repeat our history.
Masoud Msellem
Media Representative of Hizb ut Tahrir
in Tanzania

Thursday, October 27, 2016

BREAKING NEWS: UFISADI NSSF - RIPOTI YA CAG YAFICHUA SIRI NZITO.



 wakati tuhuma za ubadhilifu wa fedha zikiendelea kusambazwa kwa kasi.
JAMVI LA HABARI limepata nakala ya ripoti ya mdhibiti na mkaguzi mkuu wa hesabu za serikali inayoonyesha kuwa shirika hilo halina ubadhilifu wowote na kwamba limepata hati safi.

taarifa hizo pia zinaonyesha tuhuma zote zilizoibuliwa na ukaguzi wa awali na majibu yake. zaidi unaweza ukajionea mwenyewe.


Tuesday, October 25, 2016

KAMPENI : JUSTICE FOR MUSSA TESHA INAENDELEA



BREAKING NEWS: ALIYEMWAGIWA TINDIKALI ALIA KUTELEKEZWA, AMTAKA RAIS MAGUFULI KUINGILIA KATI

WAZIRI MAMBO YANDANI, MH WAZIRI KATIBA NA SHERIA, MPO WAPI HAKI YANGU, INAPOTEA HIVI HIVI HII NI KWELI
Kijana Mussa Tesha, Mwanachama wa chama cha Mapinduzi CCM amelalamika kutelekezwa na kutokujua hatima ya kesi yake ambayo sasa imefikisha miaka mitano mahakamani huku upelelezi ukiendelea kesi ambayo inamuhusisha yeye kama shahidi wa tukio la kumwagiwa tindikali katika harakati za kampeni za uchaguzi mdogo wa jimbo la igunga mwaka 2011 uliofanyika kuziba nafasi ya aliyekuwa mbunge wa jimbo hilo Rostam Aziz aliyeamua kujiudhulu kwa kile alichokiita kuchoshwa na siasa uchwara

katika ujumbe wake unaosikitisha aliousambaza kwenye vyombo mbali mbali vya habari na mitandao ya kijamii, Tesha amewaomba watanzania washirikiane kusambaza ujumbe huo mpaka umfikie Rais Magufuli ili pengine haki yake ipatikane.

Huu hapa chini ndio Ujumbe wake

''MH RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA MH JOHN POMBE JOSEPH MAGUFULI , AWALI YA YOTEE NAKUPONGEZA KWA KAZI NZURI NA UWELEDI WAKO UNAONDELEA KUTUTENDEA WATANZANIA WANYONGE NA KUTUJALI HONGERA SANA.

NATUNAKUOMBEA UENDELEE HIVYO HIVYO NASISI WATANZANIA TUNAIMANI NAWEWE NA TUNAKUOMBEA ZAIDI UENDELEE NA MSIMAMO  HUOHUO.

MIMI NAITWA MUSSA C.TESHA KADA WACCM NA NI MTANZANIA, NILICHOKUWA NATAKA KULIA NDANI YA SEREKALI HII YAKO YA CHAMA CHA MAPINDUZI CCM NI KUHUSU KESI YANGU,

MNAMO TAREHE 10/9/2011 NILIFANYIWA UKATILI MBAYA NA KUMWAGIWA TINDIKALI UCHAGUZI MDOGO WA IGUNGA MJINI NIKIWA NATOKEA OFSI ZA CCM BILA KUGOMBANA NA MTU WALA KUKOSANA NA MTU YOYOTE NILISHANGA KUVAMIWA NAKUTEKWA KUPELEKWA MWISHONI MWA MJI NABAADAE KUFANYIWA VITENDO VYA NAMNA HIYOO NA BAADHI WALIOVIFANYA NILIWATAMBUA.

                                        Waziri wa Mambo ya Ndani Mwigulu Nchemba
NA BAADA YAKUOKOTWA NA WASAMARIA WEMA USIKU HUO NILITAJA MAJINA BAADHI NA KISHA KUPOTEZA FAHAMU SIKUJITAMBUA TENA MPAKA KUJA KUJITAMBUA NIKIWA KCMC NAKUTOA MAELEZO YALEYALE YA AWALI.

 MH RAIS NA VIONGOZI INASHANGAZA MPAKA NIMEONA NIANDIKE UJUMBE HUU KWAKUWA SEREKALI YA AWAMU YA TANO CHINI YA MH RAIS WETU JOHN POMBE NI SIKIVU NA NINYEPESI KUTATUA MATATIZO YAWANYONGE.

NILIJARIBU KWENDA MAHAKAMANI KUUULIZIA NILIJIBIWA UPELELEZI BADO MH RAIS  UPELELEZI LEO NI MWAKA WA TANO  BADO UPELELEZi  HAUJAKAMILIKA WATUHUMIWAA  WANGU NAWAONA,
                                       Waziri wa Katiba na Sheria. Dkt. Harrison Mwakyembe.

NAOMBA  MH RAIS UGALIE NAHILI  

MH WAZIRI MAMBO YANDANI, MH WAZIRI KATIBA NA SHERIA, MPO WAPI HAKI YANGU, INAPOTEA HIVI HIVI HII NI KWELI
NAOMBA KUWAKILISHA .''

Umeeleza Ujumbe huo wa Mussa Tesha.

Monday, October 24, 2016

BREAKING NEWS: ZAWADI MAALUM KWA MAHARUSI, SEND OFF NA KITCHEN PARTY WOTE

Kampuni ya Tetere Media, imeamua kutoa zawadi maalum ya kufunga mwaka kwa wote wanaoelekea kusherehekea shughuli zao za harusi, sendoff, kitchen party na hafla mbali mbali kwa kuwapatia punguzo kubwa la bei katika shughuli hizi kama tangazo hapo linavyoonyesha.

HONGERA SANA JPM


Sunday, October 23, 2016

UMEYA KINONDONI: CHADEMA KUTINGA MAHAKAMANI KESHO KUPINGA UCHAGUZI

Wanatumia vyombo vya dola kudhibiti, Polisi kwenye uchaguzi wamekuwa wengi kuliko wajumbe ili wawatie hofu wajumbe na wananchi waliojitokeza kushuhudia Uchaguzi huo,
imeripotiwa katika Mtandao marufu wa JamiiForums imeripotiwa hivi.

                                                                 Freeman Mbowe,
 Madiwani wa CHADEMA Manispaa ya Kinondoki kwenda Mahakamani kesho Jumatatu::
Habari kutoka Kwa madiwani na uongozi wa vyama vinavyounda Ukawa kesho kupanda mahakamani kufungua kwa hati ya Dharura kwa kile kilichotokea leo kwenye uchaguzi wa meya wa Kinondoni.

kwa utararibu uliofanyika leo kuna ukiukaji mkubwa wa sheria za uchaguzi na ubabe ulikuwa mwingi sana
nimarumaini yetu kuwa mahakama itayenda haki kwa wote. Mwisho wa kunuku

MWISHO WA CHADEMA KULALAMIKA UMEFIKIA
"CHADEMA ilianzisha Operesheni Umoja wa Kupambana Udikteta Tanzania (UKUTA), hatuwezi kukaa kimya tena, Nyerere alikataza Vijana kuwa wanyonge na waoga, hakutaka Taifa la watu waoga, na sisi tunasema mwisho wa uoga umekwisha, tutakwenda Mahakamani kwa sababu kilichotokea leo kwenye Uchaguzi wa Meya wa Manispaa Kinondoni leo ni uhuni, kanuni na taratibu zinavunjwa waziwazi".

Hayo yamesemwa na Katibu Mkuu wa CHADEMA Taifa, Dkt. Vincent Mashinji, wakati akiongea na waandishi wa habari Makao Makuu ya Chama hicho yaliyopo Kinondoni jijini Dar es salaam, leo Jumapili 23/10/2016 baada ya Uchaguzi wa kumapata Meya wa Manispaa ya Kinondoni kuvunjika.

Wanasheria tegemeo wa Chadema Tundu Lissu na Peter Kibatala walipokuwa mahakani na Saed Kubenea Mbunge wa Ubungo - Picha ya Maktaba .

Wanatumia vyombo vya dola kudhibiti, Polisi kwenye uchaguzi wamekuwa wengi kuliko wajumbe ili wawatie hofu wajumbe na wananchi waliojitokeza kushuhudia Uchaguzi huo, Polisi wamewazuia kuingia ndani Mwenyekiti wa CHADEMA Taifa, Mhe. Freeman Mbowe na Katibu Mkuu wa CHADEMA kushuhudia Uchaguzi huo, vyombo vya habari vinavyoripoti bila kupendelea upande wowote vimezuliwa kuingia, waliozuiwa kuingia ni mwandishi wa Mwananchi, Mtanzania na Tanzania Daima, huku wakiruhusu waandishi wao wa TBC, Uhuru na Mzalendo, unaweza ukaona jinsi nchi inavyoendeshwa na Serikali ya awamu ya tano.

CHADEMA kimesema hakitakuwa Chama cha kulalamika tena, watakwenda Mahakamani, watakusanya ushahidi na kudai haki, Mashinji amesema wameanza kudai Katiba ya Wananchi ndio suluhisho ya kila kitu, ni Katiba ambayo ni ya Wananchi ambayo ikipatikana mambo kama haya ya uvunjaji Sheria,kanuni na taratibu katika nchi utakwisha.

Madiwani wa Ukawa walitoka nje ya ukumbi wa kupigia kura mara baada ya kubainika mbinu chafu zilizokuwa zimeandaliwa ili mshindi atoke CCM, Wajumbe kutoka nje ya Manispaa ya Kinondoni wameingizwa kwenye Uchaguzi huo ikiwa ni kinyume na Sheria na taratibu, huku wajumbe halali wa UKAWA wakitolewa kushiriki Uchaguzi huo, waliotolewa ni Mhe. Susan Lyimo na Salma Mwasa.

Akiongea Mhe. Halima Mdee amesema watakwenda Mahakamani kwa kuwa ni ukiukwaji wa sheria, taarifa ya Uchaguzi hutolewa ndani ya siku 7, ili kutafuta wajumbe, kuangalia mkinzano wa kisheria ili mambo yawekwe sawa, lakini kilichofanyika taarifa imetolewa siku 1 kabla ya Uchaguzi ili wafanye mbinu zao ovu, Madiwani wapo 34, ili akidi itimie lazima kura zipigwe 23,lakini wamepiga kura wajumbe 18 tu, huo ni uvunjaji wa Sheria ndo maana CHADEMA imeamua kwenda mahakamani.
Source : JF

BEN SITA MEYA MPYA KINONDONI. HIVI NDIVYO ALIVYANZA KAZI LEO

                            Meya mpya wa kinondoni katika picha mbalimbali baada ya kuanza kazi


ANTHONY MTAKA : NA HARAKATI ZA KUUFANYA MKOA WA SIMIYU KUZALISHA BIDHAA ZA VIWANDANI ZAIDI YA CHINA.

Chaki zimekuwa zikiagizwa kutoka China,Ujerumani,India na Kenya na sasa bidhaa hii inapatikana kwa uhakika mkoani Simiyu na kwa gharama nafuu.

                                             Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Anthony Mtaka

Mkuu wa mkoa wa Simiyu Mheshimiwa Anthony Mtaka ameonyesha  kwa vitendo namna Tanzania ya Viwanda inavyotafutwa na kutakiwa kuwa baada ya kuanza michakato ya uanzishwaji wa viwanda vya bidhaa mbali mbali ikwemo chaki, maziwa, viatu na kadharika.

JAMVI LA HABARI limebaini kuwa Wastani wa shilingi milioni 25 kwa mwezi zitaenda Maswa Chalk ili kununua chaki za shule za serikali ndani ya Mkoa wa simiyu,kiwanda hiki kidogo kimefungua fursa mpya kwa vijana wa wilaya ya Maswa na Mkoa wa simiyu.
Chaki ya Maswa.
 hii ni kutokana na uhalisia kuwa maana miongoni hao vijana wanaojitokeza wengi ambao wameomba kuwa mawakala wa usambazaji chaki ndani na nje ya mkoa,ni mradi wenye faida kwenye halmashauri katika kujipatia pato la ndani,serikali kupitia kodi,vijana kwenye ajira na vibarua,na kama mkoa kujitosheleza kwa chaki na kuitosheleza mikoa jirani,na sasa soko la Zanzibar ambalo lilitangazwa na Mh.Dr.Shain Rais wa Zanzibar,

kwa muda mrefu sasa Chaki zimekuwa zikiagizwa kutoka China,Ujerumani,India na Kenya na sasa bidhaa hii inapatikana kwa uhakika mkoani Simiyu na kwa gharama nafuu,kiasi kwamba shule zitaneemeka kwa kupata salio kwenye pesa za elimu bure na kuweza kuwasaidia kuzitumia kwa mahitaji matumizi mengine ya kielimu shuleni,katoni moja ya chaki iliuzwa kwenye mashule kati ya shilingi elfu 30 mpaka 65 but simiyu itauza katoni kati ya shilingi elfu 20 mpaka 28 elf kwa katoni.

TUPENDE VYA KWETU-Simiyu :-Wilaya Moja Bidhaa  Moja.

NYUNDO : CHADEMA WAMEZOEA KUDEKEZWA, KUSHINDA WASHINDE WAO TUKISHINDA SIE NONGWA

Mohamed Nyundo.
mwenyekiti wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi mkoa wa Pwani (UVCCM) PWANI ambaye pia ni mjumbe wa Halimashauri kuu ya Chama hicho Taifa kutokea wilaya ya Mafia, Mohamed Nyundo amewatolea uvivu vijana wenzake wa chama cha demokrasia na maendeleo chadema waliokuwa wanabishana mtandaoni kwamba CCM imefanya hujuma katika uchaguzi wa Umeya Manispaa ya kinondoni na kuwataka waachane na hadithi zao za kizamani.

''nyie mkishindwa basi mmehujumiwa, mkienda mahakamani mkishinda kesi basi mahakama imetenda haki, mkishindwa mnasema Mahakama ya CCM na mmeonewa, nyie watu gani hivi''.

Nyundo alionyesha kusikitishwa zaidi na tabia hizo na kuwaambia zama za kujitekenya na kucheka wenyewe zimekwisha na sasa hivi vijana wa CCM kamwe hawataacha waendelee kupotosha kila mara.

''unajua mambo mengine yanachekesha kweli, Kususa mnasusa wenyewe, hivi aliyewaambia mkisusa akidi haitimii nan, kususa kwenu hakuwezi kubadili matokea, mmeshindwa kubalini yaishe jiandaeni na uchaguzi uhao''. amenukuliwa MNEC huyo wa Mafia.