Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Anthony Mtaka
Mkuu wa mkoa wa Simiyu Mheshimiwa Anthony Mtaka ameonyesha kwa vitendo namna Tanzania ya Viwanda inavyotafutwa na kutakiwa kuwa baada ya kuanza michakato ya uanzishwaji wa viwanda vya bidhaa mbali mbali ikwemo chaki, maziwa, viatu na kadharika.
JAMVI LA HABARI limebaini kuwa Wastani wa shilingi milioni 25 kwa mwezi zitaenda Maswa Chalk ili kununua chaki za shule za serikali ndani ya Mkoa wa simiyu,kiwanda hiki kidogo kimefungua fursa mpya kwa vijana wa wilaya ya Maswa na Mkoa wa simiyu.
Chaki ya Maswa.
hii ni kutokana na uhalisia kuwa maana miongoni hao vijana wanaojitokeza wengi ambao wameomba kuwa
mawakala wa usambazaji chaki ndani na nje ya mkoa,ni mradi wenye faida
kwenye halmashauri katika kujipatia pato la ndani,serikali kupitia
kodi,vijana kwenye ajira na vibarua,na kama mkoa kujitosheleza kwa chaki
na kuitosheleza mikoa jirani,na sasa soko la Zanzibar ambalo
lilitangazwa na Mh.Dr.Shain Rais wa Zanzibar,kwa muda mrefu sasa Chaki zimekuwa zikiagizwa kutoka China,Ujerumani,India na Kenya na sasa bidhaa hii inapatikana kwa uhakika mkoani Simiyu na kwa gharama nafuu,kiasi kwamba shule zitaneemeka kwa kupata salio kwenye pesa za elimu bure na kuweza kuwasaidia kuzitumia kwa mahitaji matumizi mengine ya kielimu shuleni,katoni moja ya chaki iliuzwa kwenye mashule kati ya shilingi elfu 30 mpaka 65 but simiyu itauza katoni kati ya shilingi elfu 20 mpaka 28 elf kwa katoni.
TUPENDE VYA KWETU-Simiyu :-Wilaya Moja Bidhaa Moja.
No comments:
Post a Comment