Mtanzania, Mwanaharakati, Mfanyabiashara na mwanasiasa mwanachama wa chama cha Nccr Mageuzi na aliyepata kuwa Katibu Mkuu wa Taifa wa chama hicho Sam Ruhuza, ametoa ushuhuda juu ya ndege mpya za shirika la ndege Tanzania maarufu kama ndege za magufuli.
Picha siku ya Uzinduzi Rasmi wa ndege
katika ukurasa wake wa Facebook Ruhuza ameandika ifuatavyo
Bombardier Q 400
Asanteni sana kwa michango yenu yenye pongezi nyingi na maswali mengi.
Kwanza niombe msamaha kwa kuchelewa kujibu na kuwajuza juu ya safari nzima Kigoma to Dar.
Nilipofika Dar tu, nimekuwa bize sana tokea Airport. Leo ndio nimepata nafasi muda huu.
Kwanza niombe msamaha kwa kuchelewa kujibu na kuwajuza juu ya safari nzima Kigoma to Dar.
Nilipofika Dar tu, nimekuwa bize sana tokea Airport. Leo ndio nimepata nafasi muda huu.
Majibu ya baadhi ya maswali;
Uwanja wa Ndege Kigoma ni Tarmac ( Lami ) na sio Gravel ( Changarawe ).
Ni vyema tuite ni lami ya Kigoma maana ni tofauti na zingine. Lami haijatulia. Labda aliyekuwa Waziri wa Ujenzi wakati uleee atakuwa na majibu zaidi ya ubora wa hiyo lami.
Ni vyema tuite ni lami ya Kigoma maana ni tofauti na zingine. Lami haijatulia. Labda aliyekuwa Waziri wa Ujenzi wakati uleee atakuwa na majibu zaidi ya ubora wa hiyo lami.
Ndege Bombardier Q 400 nimeiona ni nzuri na nilichopenda
zaidi ni utulivu wake iwapo angani. Inaruka urefu wa futi 27,000 lakini
kwa ukosefu wa screen za kwenye eneo la abiria, inabidi iruke futi
25,000 ambapo Ndege nyingi zinazokuja Kigoma huruka chini ya futi 20,000
ambazo kulingana na hali ya hewa kati ya Kigoma na Tabora kuanzia saa
nne asubuhi inakuwa nzito sana na Ndege inapata shida sana kupambana na
upepo.
Hii Bombardier Q 400 kwa urefu wa kuruka, inapita ule upepo mzito
na hivyo Ndege inatulia angani. Upepo mzito husababisha mafuta ya Ndege
kutumikia zaidi. Hivyo Ndege hii inapunguza ulaji mafuta kwa kiwango
kikubwa.
Muda wa safari ni masaa mawili. Tuliruka Kigoma saa kumi dakika kumi na tukatua Dar saa kumi na mbili na dakika kumi.
Urukaji wake ni wa umbali mfupi sana. Kwa uwanja wa Kigoma hailazimiki kuzunguka uwanja. Inatoka kwenye parking, inaingia lane ya kuruka na kuruka ikiwa haijafika hata nusu uwanja, ni kama mita 400 na 500.
Kutua nako ni inatua na speed inapungua mapema sana. Haihitaji kwenda mbali kugeuza.
Tulitua salama japo utuaji haukuwa wa laini. Ndege iligonga ardhi badala ya kutua. Inawezekana Rubani bado hajaizoea Ndege. Itakapozoeleka, ataweza kutua kwa ulaini. Abiria hatakiwi kusikia kishindo kwenye utuaji wa Ndege.
Mapungufu;
Kawaida Ndege inapoingia nchini kwa mara ya kwanza,
humwagiwa maji ikiwa ni ishara ya heshima kuikaribisha. Tuliona wakati
zilipowasili. Utaratibu huo wa heshima wa kukaribisha hutumika kuwapa
Abiria wa mwanzo toka kwa Ndege mpya inapoanza safari au Shirika la
Ndege linapoanza safari mpya au kurudi angani baada ya kutokuwapo kwa
kipindi kirefu.
Sam Ruhuza.
Kunakuwapo na ukaribisho wa kipekee kwa abiria kupewa
hata juice na vitafunwa kabla ya kupanda Ndege na hata kumualika
Kiongozi wa eneo lile kushirikiana na abiria na waalikwa wengine
kuikaribisha na kujulikana, hii ni kujitangaza kibiashara zaidi.
Ndani
ya Ndege kunakuwa na viburudisho vingi na hata inapotua abiria
hupokelewa na viongozi wakuu wa shirika na kupewa heshima ya kipekee.
Hilo halikuwapo kabisa. Tumepanda Ndege kama vile Ndege hiyo imekuja mara nyingi na ndani ya ndege ni korosho na soda au juice tu. Tulipotua kila abiria na mambo yake. Hakukuwa na Kiongozi yeyote wa shirika. Ndani ya Ndege Rubani hata hakutuata abiria kutukaribisha na kutuelezea uzuri wa Ndege hiyo na kwanini tuendelee kusafiri nayo.
Kwa kifupi hakukuwa na shamrashamra zote kuonyesha safari za Bombardier zimeanza.
Ndege ilikuwa iondoke Kigoma saa mbili na robo asubuhi. Baadae tukaambiwa saa nane na robo. Tukaondoka saa kumi na dakika kumi.
Halafu hatukuombwa samahani na rubani kwa kutuchelewesha. ATCL Kigoma walijitahidi wao binafsi kutupa lugha ya kutuomba msamaha lakini sio Ndani ya Ndege na tulipotua. Business as usual.
Hii sio utaratibu wa shirika la Ndege tena kongwe kama ATCL kufanya makosa kama hayo. Inawezekana ni kufanya kazi kwa uoga. Bodi ya ATCL waelewe hii ni biashara na biashara inahitaji kuvuta mteja.
Nauli iliyotangazwa mitandaoni ya Tshs610,000/- return
Kigoma - Dar - Kigoma sio tuliyolipa. Tumenunua kwa Tshs670,000/- na
ukichelewa zaidi utainunua kwa Tshs810,000/-.
Kawaida shirika la Ndege linapoanza route inaingia na bei ya chini sana (penetration fare), kama ilivyokuwa kwa fastjet ya Tshs32000/- kwa viti vichache halafu baadae inapanda.
Kawaida shirika la Ndege linapoanza route inaingia na bei ya chini sana (penetration fare), kama ilivyokuwa kwa fastjet ya Tshs32000/- kwa viti vichache halafu baadae inapanda.
ATCL imetumia uingiaji mdogo wa nauli kwenye safari za Mwanza, Arusha, Mbeya ambapo nauli Ni Tshs160,000/- return ikiwa Tshs299,000/- lakini sio Kigoma na Tabora.
Ni kwanini Kigoma na Tabora hawamo??!
Wameangalia nauli ya mshindani, nawao ndio wamepitia hapohapo. Hawakumpa promotion abiria wa maeneo hayo.
Kwakuangalia ukubwa wa Bombardier Q400 viti 74 na gharama zote za safari Kigoma Dar, gharama ya kiti haizidi Tshs70,000/- kwa kiti. Wakiweka kiti kwa Tshs150,000/ kuanzia ni faida tosha na wasafiri watakuwa wengi na kuifanya Ndege kuruka ukanda huo hata mara 3 kwa siku ikiwa imejaa.
Nashauri tusikimbilie Airbus bali tuongeze Bombardier zingine 2 ili tutosheleze soko la ndani na nchi zinazotuzunguka.
Tukumbuke Shirika la Ndege ya umma ni kutoa huduma zaidi na
Serikali inapata faida kubwa kwenye huduma zingine zinazochochewa na
uwepo wa Ndege.
Matumaini yangu ni watu tuipende ATCL, tuishauri na
kuitumia kwakuwa ni yetu sote. Muhimu wapate Mkuu wa idara ya biashara
mtaalam na mzoefu mkubwa wa uendeshaji wa shirika la Ndege na
asiingiliwe.
Karibu Bombardier Q 400 .
No comments:
Post a Comment