WADHAMINI WETU

WADHAMINI WETU

Saturday, October 15, 2016

MGOGORO CUF: MAUZA UZA YAIBUKA BODI YA WADHAMINI.

Huku mgogoro wa uongozi wa chama cha wananchi Cuf ukiendelea na sasa ukionekana kuelekea mahakamani ambapo wanaodaiwa kuwa wajumbe wa Bodi ya wadhamini wa chama hicho wamekwenda mahakamani kumshitaki msajili wa vyama vya siasa na Mwenyekiti wa Chama hicho Prof. Ibrahim Lipumba, imebainika kuwa Bodi hiyo ya wadhamini haipo halali kisheria kwa mujibu wa katiba ya chama chao.

taarifa zilizozagaa mitandaoni zinasomeka kama ifuatavyo hapa chini kama zilivyoandikwa na wana mtandao wanaomtetea Prof. Lipumba
.Prof. Ibrahim Lipumba, Mwenyekiti wa CUF TAIFA.

"HIZI NDIZO "HOJA" ZETU,  KWA NINI "PROF. LIPUMBA NDIYE MWENYEKITI HALALI "CUF". 

 Hakuna "SHAKA" KUJIUDHURU kwake hakukuwa kumekamilika Baada ya yeye mwenyewe kuiandikia Barua "OFFICE" Ya katibu mkuu wa chama cha CUF. 

Sababu za kutokamilika kwa "KUJIUDHURU" Kwa PROF IBRAHIM LIPUMBA ni hizi zifuatazo..
1) Kwa mujibu wa "KATIBA" Ya CUF kujiudhuru kwa kiongozi wa Ngazi ya PROF IBRAHIM LIPUMBA ni "MCHAKATO" unaopitia Ngazi NNE 

a) Kiongozi anayetaka "KUJIUDHURU" Ataandika Barua kwa katibu wa Mamlaka iliyomchagua. 

b)Katibu wa "MAMLAKA" Husika kuipokea Barua hiyo. 

c) Katibu wa "MAMLAKA" Husika kuiwasilisha "BARUA" Hiyo kwa Mamlaka iliyomchagua au kumteua ( Ambayo kwa Prof Lipumba ni Mkutano mkuu wa Taifa ). 

d) Barua Kusomwa Mbele ya "MAMLAKA" Husika na kujadiliwa. 

f) "MAMLAKA" Husika kufanya "MAAMUZI" Juu ya "BARUA" Husika ya "Amma "KUKATAA"Au "KUKUBALI" Kujiudhuru kwake. 

Hii ni kwa Mujibu wa ""KATIBA" Ya CUF Ibara YA 117 (2). 

NUKUU :
117 (2) - Kiongozi atajiudhuru kwa kuandika barua kwa katibu wa Mamlaka iliyomchagua au kumteua na kiongozi huyo atahesabiwa kuwa amejiudhuru ikifika Tarehe aliyoainisha katika barua yake kuwa atajudhuru Pindipo  akikubaliwa na mamlaka iliyomchagua au iliyomteua ,  Au kama hakuainisha Tarehe ya kujiudhuru kwake Basi atahesabiwa amejiudhuru mara baada ya katibu wa Mamlaka kupokea Barua hiyo na Mamlaka iliyomchagua au kumteua kukubali.
MWISHO WA NUKUU. 

"CUF" Ni Chama Imara Katiba yake iliona Mbali ndiyo Maana haikusema Kutamka kwenye vyombo vya habari kama wengi wanavyo Jaribu kuwaaminisha Watanzania kwamba kutamka kwake tu,  Kwenye mkutano wa wanahabari ingetosha kuwa "AMEJIUDHURU" Vipi kama angejiudhuru  Baada ya Kufanya Ubadhirifu ? 

"Wala Hatuwezi kulinganisha "MAMLAKA" YA "KUCHAGULIWA" Na Zaidi ya WATU Mia Saba sawa sawa na "AJIRA" Ya Muhindi au Ajira ya Chombo Chochote kile Ambayo imetolewa kwa MAMLAKA ya mtu mmoja tu ambaye KISHERIA akipokea Barua ajira hiyo itakuwa imekoma. 

(2) Katiba ya CUF iko kimya kuhusu "KUTENGUA" Maamuzi ya kujiudhuru, Hivyo hapakuwa na kizuizi kwa PROF IBRAHIM LIPUMBA kutengua Barua yake kwa kuzingatia "UKIMYA" Huo ( In action )  kwa upande wa uongozi kuchukua hatua pindi walipopokea "BARUA" yake ya kujiudhuru,  Na hivyo kutoa mwanya kwa Muhusika kuitengua Barua yake ya kujiudhuru. 

"Kwa mujibu wa katiba ya "CUF " haizungumzi lolote amma kukataa au kukubali mtu aliyeandika barua ya "KUJIUDHURU" kutengua maamuzi yake..  hii inamaanisha haijaruhusu Wala haijakataza - kosa la PROF IBRAHIM LIPUMBA kutengua maamuzi yake linatoka wapi? 

Kwa hiyo wanataka Profesa Lipumba asiwe Mwenyekiti wa CUF wanapaswa waje na hoja nyingine na siyo hizi zinazosemwa kwa kuwa kitendo chake cha kuandika barua ya kutengua kujiudhuru kinamaanisha Barua hiyo haipo tena na imekufa KIFO cha kawaida ( Natural Dearth ). 

Hizo HOJA za kunulika na COM ni za kitoto  sana na hazina mashiko.
Profesa Lipumba si mwenyekiti "CUF" Kwa Amri ya Msajili wa vyama vya siasa Bali ni Mwenyekiti Kwa Mujibu wa Katiba ya CUF ya Mwaka 1992 Toleo la 2014 Ibara ya 117 (2). Kilicho kwenda kuombwa kwa Msajili wa vyama ni Tafsiri na Muongozo na Si Haki ya Kutambuliwa kwa kuwa Katiba hii Bado inamtambuwa.

No comments:

Post a Comment