WADHAMINI WETU

WADHAMINI WETU

Tuesday, October 11, 2016

DONALD TRUMP ATELEKEZWA

Mkuu wa Republican asema hatamtetea tena Donald Trump

 

BBC.
Afisa mkuu zaidi wa chama cha Republican aliyechaguliwa amesema hatamtetea tena mgombea urais wa chama hicho Donald Trump, baada ya matamshi yake kuhusu wanawake ambayo yamezua utata.
Spika wa Bunge la Wawakilishi Paul Ryan ameapa kuangazia sasa kuhakikisha wagombea wa chama hicho wanatetea viti vyao katika Bunge la Congress.

Hata hivyo, hajabatilisha uamuzi wake wa kumuidhinisha mgombea huyo.
Bw Trump naye amemjibu Bw Ryan kupitia mtandao wa Twitter na kusema hafai kupoteza wakati akimpigania.

Awali, mpinzani wa Bw Trump kutoka chama cha Democratic Hillary Clinton ametilia shaka hatua ya Bw Trump kuomba radhi kutokana na matamshi hayo aliyoyatoa miaka 11 iliyopita.
Kwenye kadha hiyo ya video, Bw Trump anaonekana akisema alivyoomba kushiriki mapenzi na mwanamke aliyeolewa. Aidha, anatoa matamshi ya kudhalilisha kuhusu wanawake.
Lakini Jumapili, Bw Trump alisema maneno yake kwenye kanda hiyo ya video yalikuwa "mazungumzo ya mzaha faraghani".
Hata hivyo alisema anajutia kuyasema.

Akizungumza wakati wa mdahalo wa urais Jumapili, Bw Trump hata hivyo alisema hakumnyanyasa mwanamke yeyote kingono.
Bi Clinton aliandika kwenye Twitter Jumatatu kwamba iwapo Bw Trump anasisitiza msimamo wake, bado inaonesha wazi kwamba "hajajutia matamshi hayo".


 Bw Paul Ryan akiwa kwenye kampeni Wisconsin, Marekani

Bw Trump alipoulizwa kuhusu kanda hiyo ya video kwenye mdahalo Jumapili, badala yake alimgeukia mpinzani wake Bi Clinton na kusema mumewe Bill Clinton alikuwa "anawadhalilisha wanawake"
Bi Clinton alikataa kuzungumzia hilo.
Takriban maafisa 38 wakuu wa chama cha Republican, wakiwemo masene, wabunge na magavana, wameondoa uungaji mkono wao kwa Bw Trump, tangu kutokea kwa ukanda huo wa video Ijumaa.
Lakini Jumatatu, mwenyekiti wa Kamati ya Kitaifa ya Republian Reince Priebus alisema hakuna kitu chochote kimebadilika kuhusiana na kampeni.

 Mike Pence Ohio - 7 OktobaBw Pence awali alisema matamshi ya Bw Trump "hayawezi kutetewa"

Mgombea mwenza wa Bw Trump, Mike Pence, hata hivyo amesema ataendelea kumuunga mkono na kumtetea. Hata hivyo awali alikuwa amesema matamshi ya Bw Trump kwenye kanda hiyo ya video "hayawezi kutetewa".
Lakini akiongea na CNN Jumatatu, bw Pence alisema "ni heshima kubwa" kwake kumuunga mkono Bw Trump na akakanusha madai kwamba alitafakari wazo wa kujiondoa.

No comments:

Post a Comment