katibu tawala (DAS) wa wilaya ya chemba Nyakia Ally kushoto (Picha ya Maktaba)
Katibu Tawala wa Wilaya,ambaye pia ni Mwenyekiti wa Kamati ya Michezo ya Wilaya Ndugu Nyakia Ally,amefungua mashindano ya Diwani Cup wilayani Chemba,huku akiwasihi
vijana kucheza mpira wa miguu wakitambua kuwa kwa sasa ni ajira
inayolipwa kwa pesa nyingi kulinganisha na michezo mingine hapa
nchini.
Ndugu.Nyakia
alieleza kuwa mashindano hayo yameandaliwa na Diwani wa Kata ya Chemba,
Mhe Joseph Saini ambapo yanashirikisha timu sita kutoka katika Vijiji
vitatu vinavyounda Kata ya Chemba.
Mshindi wa mashindano hayo
atajinyakulia zawadi ya Mbuzi beberu,Katika mashindano hayo yatakayokuwa
ya kusimumua wilayani humo,Katibu Tawala wa Wilaya hiyo Ndugu Nyakia
Ally ameahidi kuongeza zawadi ya mipira miwili kwa mshindi wa kwanza,
mpira mmoja kwa mshindi wa pili na watatu.
Vile
vile Katibu Tawala huyo aliwataka vijana kushirikiana katika mashindano
hayo bila kujali Itikadi zao za kisiasa, dini wala rangi kwani michezo
hujenga Udugu, urafiki na upendo miongoni mwa wapenzi wa michezo husika.

Baadhi ya Washiriki na Washabiki wakifuatilia yaliyokuwa
yakijiri kwenye ufunguzi wa mashindano ya Diwani Cup wilayani Chemba
mapema leo,ambapo mashindano hayo yamefunguliwa rasmi na Katibu Tawala
wa wilaya hiyo,ambaye ni Mweyekiti wa kamati ya michezo,Ndugu Nyakia
Ally (hayupo pichani)
No comments:
Post a Comment