Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe. Mrisho Mashaka Gambo amechangia Lita 600 za mafuta kwa ajili ya greda la Halmashauri ili liweze kutengeneza miundombinu ya barabara kwenye maeneo yote korofi yanayozunguka kata ya Terrati.
Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe. Mrisho Gambo (kwanza kulia)
akizungumza na wananchi wa Kata ya Terrati kwenye Mkutano wa hadhara
uliofanyika kwenye uwanja wa shule ya Msingi Mkonoo.
Rc Gambo amefanya hivyo wakati wa mkutano wa hadhara na wananchi wa Kata ya Terrat uliofanyika kwenye Shule ya Msingi Terrat wenye lengo la kufahamu changamoto za muda muda mrefu zinazowakabili wananchi wa maeneo hayo. Katika Mkutano huo Mkuu wa Mkoa alianadamana na watalaamu wa Taasisi mbalimbali zinazotoa huduma katika Mkoa huu pamoja na menegiment ya Jiji ili kuwezesha upatikanaji wa
majawabu ya kero zote zilizo wasilishwa na wananchi hao ikiwa ni pamoja na utekelezaji wa haraka ili kumaliza kabisa changamoto hizo.
Mkuu wa Wilaya ya Arusha Fabian Gabriel Daqqaro
Wananchiwa Kata hiyo wamesema kwa muda mrefu wamekuwa wakikabiliwa na kero ya ubovu wa miundombinu ya barabara, kukosekana kwa maji safi na salama pamoja na umeme katika eneo hilo na pia walitoa shukrani zao kwa Mkuu wa Mkoa kwa kuwapa kipaumbele katika ziara zake za kutambua changamoto za Mkoa wake.
Sisi wakazi wa huku tumekua kama hatuishi kwenye Jiji la Arusha kwa sababu huduma zote muhimu zimekuwa kikwazo sana kwetu mpaka zinasababisha kudorora kwa uchumi kwa wakazi wa maeneo haya kwa kuwa hapavutii wafanyabiashara kuja kuwekeza wala wanunuzi kutoka
mjini hivyo tumekua tukiuziana sisi kwa sisi ambao wote tuna vipato duni alisema Jumanne Juma Kingu.
Mkurugenzi wa jiji la Arusha Athumani Kihamia
Mmoja wa wananchi hao aliyejitambulisha kwa Jina la Eliakim Mason kutoka Mtaa wa bondeni kati alisema kuwa Gari lakubebea wagonjwa katika kituo cha Afya Mkonoo limeharibika kwa kipindi kirefu sana na wanapata tabu ya kusafirisha mgonjwa hadi kufikia kwenye Hospital za Mjini Arusha inawalazimu kukodi Gari kwa gharama kubwa ili kunusuru maisha ya ndugu zao pia alilalamikia uhaba wa watumishi katika Kituo cha Afya Mkonoo na kudai kwamba inakuwa
vigumu kupata hudma bora wagonjwa wanapokua wengi katika kituo hicho.
No comments:
Post a Comment