WADHAMINI WETU

WADHAMINI WETU

Wednesday, October 12, 2016

MAMA ATELEKEZA MTOTO WA MIEZI NANE PEMBA

Na Masanja Mabula –Pemba .
 https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEhZBS2IgG_m3WoxPJH_UCAq4k-Wc1TUdYRDVc0iJAs8ZjDyghlLPjmSatOBw-LOgPTHkstmPF-a2L-4ISOGvo57dS8FuU9mIceg2aFN6-7x3MEQ_wgNpbUmDtpVNwbpk8E5RlxRTVFQghK8/s1600/d4ae4170-2107-45d4-a9d0-f93c30a19779.jpg
waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia wazee na watoto Mheshimiwa Ummy Ally Mwalimu.

MTOTO wa kike anayekisiwa kuwa na umri kati ya miezi minane na mwaka mmoja amefikishwa katika Ofisi ya Ustawi wa Jamii Wilaya ya Wete na wasamaria wema baada ya kutekelezwa na mama yake mzazi.
Akizungumza na mwandishi wa habari hizi katika Ofisi ya Ustawi wa Jamii Wilaya ya Wete , Amina Ali Mabrouk mkaazi wa Bopwe Jimbo la Gando ambaye aliachiwa mtoto huyo na mama yake , alisema mama mzazi wa mtoto huyo alimtelekeza mwanawe siku ya Jumatatu jioni kwa madai anakwenda kutelekeza ibada ya sala ya jioni .

Alieleza kwamba baada ya kukabidhiwa kichanga hicho , mama mzazi hakutokea tena ambapo alichukua hatua za kwenda kuripoti kituo cha polisi Wete kwa hatua za kisheria kwa kuwa mtoto huyo alikuwa anahitaji huduma .

“Nilikuwa katika biashara zangu kigengeni , mara alitoa mama mmoja hanijui wala na mimi simjui , alinitaka nimsaidie mtoto ili aende kutekeleza ibada ya sala lakini kuanzia muda huo sikumuona tena ”alieleza.
Aidha aliongeza kwamba “Ilipofika saa nne usiku ilinibidi niende kutoa taarifa kwa sheha na baadaye Polisi ambapo nilitakiwa nimfike leo (jana) asubuhi , nimefika mapema nikaambiwa nije ofisi ya Ustawi wa jamii ”aliongeza.

Afisa Ustawi wa Jamii Wilaya hiyo Salma Suleiman amekiri kupokea kichanga hicho na kusema hatua ya kwanza ni kumpeleka hospitali kwa ajili ya uchunguzi wa afya yake huku hatua nyingine zikiendelea kuchukuliwa .
Alisema katika kuhakikisha mama mzazi anapatikana , Ofisi ya ustawi wa jamii imeanza kuwasiliana na viongozi wa shehia ili kusaidia kupatikana mama yake ambapo kwa sasa ataendelea kuhifadhiwa na Ofisi ya Ustawi wa jamii.

“Jambo la kwanza ambalo Ofisi ya Ustawi itafanya ni kumpeleka Hospitali kufanyiwa uchunguzi w afya mtoto huyo , halafu masuala mengine ya kumtafuta mama mzazi zitafuatia baadaye ”alieleza.
Baadhi ya wanawake waliozungumza na mwandishi wa habari hizi , wameitaka Serikali kumtafuta mama aliyefanya kitendo hicho cha kinyama ili aweze kufikishwa kwenye vyombo vya sheria .
Bishara Mbarawa Mkaazi wa Bopwe Wilayani hapa amesahauri kufanyika uchunguzi wa kina sababu ambazo zimesababisha kichanga hicho kutekelezwa kwani huenda ni ugomvi wa kifamilia au ugumu wa maisha.

Alisema iwapo Serikali itafanya uchunguzi na kubaini ni sababu ya ugumu wa maisha , basi ni vyema wakaingizwa kwenye mpango wa TASAF wa kaya maskini ili aweze kukabiliana na hali hiyo na hivyo kuweza kutunza familia yake .

“Serikali inatakiwa kufanya uchunguzi wa kina ikiwa itabaini ni sababu ni ukali wa maisha basi aingizwe kwenye mpango wa TASAF wa kusaidia kaya maskini ili aweze kulea familia yake ,la kama sababu ni nyingine pia Serikali iangalie jinsi ya kumsaidia ”alisisitiza.

Tukio hilo limekuwa wakati jamii ikiwa katika maadhimisho ya siku ya mtoto wa kike na tukio la kwanza kuripotiwa katika Ofisi ya Ustawi wa Jamii Wilayani hapa katika kipindi cha mwaka huu .

No comments:

Post a Comment