WADHAMINI WETU

WADHAMINI WETU

Saturday, October 1, 2016

MASAUNI AZITAKA TAASISI ZA KIDINI NCHINI KUPAMBANA NA MAOVU

AFUNGUA MKUTANO WA 47 WA JUMUIYA YA WAISLAMU WA AHMADIYYA.


https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEj50NyteTJywhmuq9SSiprjc6XJKRBoLTYP289tY8XyTtgPYxnRQg8NVkqEs2hWzmO4GK7ZltKpN3ky1bUl0ah_xWZcUdthBTWJ1EIgrVCfiQy2rUnVaAnb8R_B_IqmTSGWEiyfNDKA8CE/s1600/PIX+1.JPG

 Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (katikati), Rais Mstaafu awamu ya pili, Ali Hassan Mwinyi wakiwapungia waumini wa Jumuiya ya Waislamu wa Ahmadiyya (hawapo pichani) wakati walipokuwa wanawasili katika Ukumbi wa Mkutano wa Jumuiya hiyo, uliopo Kitongoji cha Kitonga, Kata ya Msongola, Ilala, jijini Dar es Salaam. 

Waziri Masaunia ambaye alikuwa mgeni maalum katika mkutano huo wa 47 wa jumuiya hiyo nchini, aliitaka Jumuiya hiyo pamoja na Taasisi zingine za kidini nchini kuendeleza kazi kubwa ya kupambana na maovu katika jamii kwa kuwapatia waumini wao elimu na maarifa ya kuboresha tabia na maadili yao kiroho. Kulia ni Kiongozi Mkuu wa Jumuiya hiyo nchini, Sheikh Tahir Mahmood Chaudhry. Picha zote na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.

https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEhwzN8Gq79yr9fzNxwkma5aFhlMW4qMcT9VTqXoBBnQbIqrmUw7bd-qyPan0k6Pf_0bTfvEbkjVlFfMU2dzgXU8bzyBfSY7v6ZM5HtRCj9F6Ki2gEa7F4Sm5jzds0fxLsPq_b9uY-58r78/s1600/PIX+2.JPG

 Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni akizungumza na waumini wa Jumuiya ya Waislamu wa Ahmadiyya katika Mkutano wa 47 wa jumuiya hiyo nchini unaofanyika katika Ukumbi wa Mkutano wa Jumuiya hiyo, uliopo Kitongoji cha Kitonga, Kata ya Msongola, Ilala, jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Rais Mstaafu awamu ya pili, Ali Hassan Mwinyi, anayefuata ni Kiongozi Mkuu wa Jumuiya hiyo nchini, Sheikh Tahir Mahmood Chaudhry. 
 

https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEjKEVMoCIF3yzmMMHeRrWMnDiV3c4Qe1AUb-aDeS0F0SmeBOwLWwB1KiqvKKhMOjpenhtAMblHDImTfOu45MDvk71O96YY0T9YDUKCWUOGjisz3vhHdv7iKL4MveB-dIdFRUiHSQm1BdW4/s1600/PIX+5.JPG
 Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (kushoto) akipokea zawadi ya vitabu vya dini kutoka kwa Kiongozi Mkuu wa Jumuiya ya Waislamu wa Ahmadiyya nchini, Sheikh Tahir Mahmood Chaudhry wakati Naibu Waziri huyo alipomaliza kuufungua Mkutano wa Jumuiya hiyo wa 47 unaoendelea kufanyika.

Masauni ambaye aliiwakilisha Serikali katika Mkutano huo, katika hotuba yake aliitaka Jumuiya hiyo pamoja na Taasisi zingine za kidini nchini kuendeleza kazi kubwa ya kupambana na maovu katika jamii kwa kuwapatia waumini wao elimu na maarifa ya kuboresha tabia na maadili yao kiroho. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.

https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEgvrnV9q7YYd1maOIUzMJo6-ggK0-Jy7KGNMGYQ_Y6hr80b9aH8t1r3XuhkbdqIgIOZT_ttiKPYNHPfDD2mOCJJVUxDKLSzTZ4u07Yo8tdXxeYaqPWSwwnad8PSKhiVWsfx5ZAcbt7uacc/s1600/PIX+6.JPG

Sehemu ya Waumini wa Jumuiya ya Waislamu wa Ahmadiyya nchini wakimsikiliza Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (hayupo pichani) wakati alipokuwa anatoa hotuba ya ufunguzi wa Mkutano wa 47 wa Jumuiya hiyo .


KITENGO CHA MAWASILIANO YA SERIKALI

WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI.

No comments:

Post a Comment