Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mrisho Gambo, Kushoto akiwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli.
Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mrisho Gambo, amewatoa hofu wakazi wa mkoa huo na watanzania wanaoutakia heri mkoa huo juu ya kusambazwa kwa ujumbe wa kutungwa unaoeleza kuwa mkuu huyo wa mkoa ametenguliwa uteuzi wake na kwamba mkuu mpya wa mkoa atateuliwa hivi karibuni.
taarifa ya sauti ya mkuu huyo wa mkoa iliyosambaa jioni ya jumaatano imesikika ikisema kuwa Mheshimiwa Rais hana shida na hatua anazozichukua mkuu huyo wa mkoa na kwamba ana muunga mkono kwa utekelezaji wake wa majukumu na hana mpango wa kumtumbua hivyo asiwe na hodu na badala yake azidishe spidi katika kufikia kauli mbiu ya hapa kazi tu.
sauti hiyo inazidi kusema kuwa ili kuwathibitishia waliokuwa karibu na mkuu huyo wa mkoa kuwa anamuunga mkono, Rais aliagiza apewe azungumze na mmoja wa watu waliokuwa karibu na RC Gambo kwa wakati aliompiogia simu na kuongea naye.
Zaidi RC gambo amesema Rais anawasisitiza watu wa Arusha kuwa anawapenda sana na anawataka walipe kodi ili kufanikisha makusanyo ya taifa yanayopelekea kupatikana kwa maendeleo ya nchi.
taarifa hii inakuja huku kukiwa na shutuma na malalamiko kutoka kwa mbunge wa jimbo la arusha mjini anayelalamikia kutokupewa haki ya kutambulishwa na RC huyo katika shughuli ya uwekaji wa jiwe la msingi wa hospitali ya wanawake inayotarajiwa kujengwa hivi karibuni kwa ufadhili wa Martenirty Africa.
JAMVI LA HABARI
No comments:
Post a Comment