hali ya ukata wa kifedha inayolikabili taifa sasa imehamia katika Ofisi za Bunge la jamhuri ya muungano wa Tanzania amefichua Mbunge wa Kigoma mjini na kiongozi wa chama cha ACT WAZALENDO Zitto Kabwe , kiasi cha kushindwa kutoa photocopy nakala za mapendekezo ya muswada wa sheria ya habari.
Spika wa Bunge Job Ndugai.
mbunge huyo ameyasema hayo katika andiko lake alilokuwa akimjibu waziri wa habari vijana utamaduni sanaa na michezo Nape nauye aliyeandika andiko la kumtak aache unafiki kuhusiana na msimamo wake katika muswada huo.
hapa chini ni sehemu ya maandiko ya mbunge huyo kijana kutoka kigoma.
Kanuni za Bunge ( kanuni ya 84 ) zinataka kwamba Muswada
ukishasomwa Kwa mara ya kwanza Bunge lifanye MATANGAZO Kwa umma ili
kuhakikisha kuwa umma unaelewa maudhui ya muswada na kuwezesha Wananchi
kutoa maoni Yao.
Wabunge wakiwa kazini Bungeni.
Muswada huu kwanza Bunge halikutoa matangazo yeyote (
Kwa Taarifa tu Ni kwamba Hata Kamati ya Bunge ilishindwa kutoa photocopy
nakala za uchambuzi wa muswada kutoka Kwa wanasheria wa Bunge Kwa
sababu Bunge halina Fedha. Bunge halina Fedha kutoa photocopy ya nyaraka
za Wabunge kufanyia Kazi ).
Wadau wote waliokuja mbele ya Kamati ya
Bunge walitamka dhahiri kwamba wamepewa Taarifa ya kutokea mbele ya
Kamati Siku 2 kabla ya vikao Na hivyo wameomba muda zaidi wa kutoa maoni
Yao. Labda Ni kutokana Na uchanga wa shughuli za Bunge,
Mbunge wa kigoma mjini Zitto Kabwe
Waziri anajenga
Hoja kwamba Ushiriki ulianzia kabla. Mtu yeyote anayejua namna Bunge
linafanya Kazi atakwambia muswada Ni muswada pale ambapo umechapishwa
kwenye gazeti la Serikali Na kusomwa mara ya kwanza Bungeni.
limenukuliwa andiko hilo la Zitto Kabwe
No comments:
Post a Comment