Matumizi ya dawa za kupunguza maumivu na uvimbe huchangia ongezeko la hatari ya kupata maradhi ya moyo, utafiti umebaini.
Dawa kama vile Ibruprofen, Naproxen na Diclofenac ndizo dawa hutumiwa sana kupunguza maumivu na kuvimba.Jarida la Uingereza la madaktari, linasema watafiti waliwachunguza watu milioni 10 , wenye umri wa miaka 77 ambao walitumia dawa hizo.
Wataalam wa Uingereza wamesema utafiti huo haukuwa na umuhimu sana kwa wagonjwa wenye umri wa chini ya miaka 65 lakini muhimu zaidi ilikuwa kwa wagonjwa wenye umri wa makamo.
Utafiti huo ulifanyiwa watu milioni 10
wanatumia dawa hizo kutoka Uingereza, Uholanzi, Italia na Ujerumani na
kulinganishwa na watu wasiotumia dawa hizo.
'Tahadhari'
Shirika la Uingereza la masuala ya moyo (BHF) limesema wagonjwa wanaougua maradhi ya shinikizo la damu, kisukari na shida za figo wanastahili kutumia dawa hizo kwa kiwago kidogo na kwa muda mfupi.
Mkurugenzi wa shirika la BHF, Profesa Peter Weissberg amesema utafiti huo umesisitiza uchambuzi wa hapo awali kwamba wagonjwa ambao wenye shida za maungio, wamo katika hali ya hatari ya kupata shida za moyo.'Haswa kwa wale ambao hutumia dawa hizo za kupunguza mauamivu kila mara.'
BBC SWAHILI
No comments:
Post a Comment